Daudi Ballali's Death

Daudi Ballali's Death

Status
Not open for further replies.
Ninaposoma michango mbali mbali ya wana JF na pia nikisoma magazeti mbali mbali napata kigugumizi kuamini kama Balali kweli amevuta.Lakini kwa upande mmoja nalazimika kuamini japo kiduuchu. Nafikiri ipo haja ya mwanaJF mmoja kulobby ili aweze kuhudhuria mazishi na pengine aweze kuona maiti ya Balali live ili aje hapa jamvini atuhakikishie. mtanisamehe ninakuwa Tomaso katika hili!
 
Kwakweli watu hawajui waamini lipi, hili ndo limemfanya MUshi1 kuanza kutafuta data mpaka akaanza kujenga conclution kabla hajamaliza uchunguzi, hakuna mtu anayeamini kuwa amekufa kulingana na trend ya matukio.
 
Ninaposoma michango mbali mbali ya wana JF na pia nikisoma magazeti mbali mbali napata kigugumizi kuamini kama Balali kweli amevuta.Lakini kwa upande mmoja nalazimika kuamini japo kiduuchu. Nafikiri ipo haja ya mwanaJF mmoja kulobby ili aweze kuhudhuria mazishi na pengine aweze kuona maiti ya Balali live ili aje hapa jamvini atuhakikishie. mtanisamehe ninakuwa Tomaso katika hili!

Nakubaliana na wewe mkuu kwani nilipoangalia thread ya conspiracy nami sijui niamini lipi. Nadhani mmoja wa wana JF by friday atakuwa ameshatupa facts1
 
Nyinyi mnafanya juhudi za watu wengine kuwa ngumu kweli. Hivi habari za mazishi mlitangaziwa na nani? Mnafikiri zimetoka wapi? Mnafanya juhudi za watu wengi kuufunua ukweli kuwa ngumu kweli kwa sababu mnatufanya tuwe target isiyoeleweka. Mimi binafsi najitoa kwenye suala hili mwenye kuamini amekufa ataamini na mwenye kuamini hajafa naye ni imani. Hadi hivi sasa sijaweka what I believe and why.. lakini naona watu wameshanichagulia kundi.
 
Still nina wasi wasi isjie ikawa ni chnaga la macho!
Kama kweli kafa wamlete Tz na tumpe heshima zake za mwisho since he was a public figure
 
jamani mnataka mumuone sura yake, pengine hata mkiiona sura yake hamtoijua! kuna athari zitokanazo na sumu ( kama kafa kwa sumu) ambazo itamfanya sura yake tushindwe kuijua.
 
Kufikia Ijumaa kesho, basi muwe mmetuletea picha za jeneza hata kama zina gogo humo ndani lililochongwa kama aliyekuwa Balali..wakati mwingine kutaka kujiaminisha nafsi ktk haya matukio yenye utata ni kutamani kuwa na dhamiri njema lakini pia serikali kwanini iwaache wananchi wake ktk mchanganyiko huu..yaaani taarifa ilivyotolewa na BoT utadhani alokufa ni mfagizi kumbe alikuwa ni kibosile wa hilo dubwasha kwa mwongo mzima!

VIONGOZI WA SERIKALI ya Tanzania, Damu za hawa watu wanaokatika kama Balali zi juu ya vichwa vyenu, na vya watoto wenu hata kizazi cha nne cha wawaungao mkono! Kwani wangesema kwa heshima zote kuwa huyu Bwana kafariki kila mtu akaamini kiuwazi, tusingekuwa tunasugua vichwa humu JF.
 
HAPA KINACHOGOMBA NI NINI? masikitiko juu ya kifo cha balali? au wizi wa pesa za EPA? balali kokote aliko atakumbuka kuwa, kwa kukubali kutumiwa na ccm ndiko kulikomfanya afike hapo alipo, ninaamini kuwa katika mabilioni ya EPA, balali hakuwa peke yake na yeye alitumika kama rubber stamp, wasomi wengine jifunzeni, msikubali kufanywA ZUMBU KUKU NA WANASIASA
 
Jamani mbona tunajitia tuna machungu sana na Kifo cha Balali wakati kuna wengine waliosaini nyaraka kama yeye (Mgonja) bado wako hai? Kwa nini nguvu zetu zote tusizisielekeze kwa Mgonja sasa?

Tuanze mapema kuelekeza nguvu zote kabla polonium -210 atakayowekewa haijaanza kuchanganya.
 
Kuna offer ya tiketi kwa anae taka kuhudhuria mazishi yake, Ingependeza iwapo ungeenda huko... "Ni ushauri tu"

Mimi nitakuwa DC this friday maana kuna long weekend ya memorial day inaanza na nitafanya kazi kwa namna ambayo nimefanya kwenye mengi hapa JF.

Usiwe na wasiwasi kabisa kwa hili.
 
Jamani mbona tunajitia tuna machungu sana na Kifo cha Balali wakati kuna wengine waliosaini nyaraka kama yeye (Mgonja) bado wako hai? Kwa nini nguvu zetu zote tusizisielekeze kwa Mgonja sasa?

Tuanze mapema kuelekeza nguvu zote kabla polonium -210 atakayowekewa haijaanza kuchanganya.

Asante kwa kuwa umeliona hili.

ubishi wa kama Balali amekufa au hajafa unachukua nafasi ya kuwabana kina Mgonja na wenzake waliohusika kwenye wizi huu. Wazo zuri sana hili.
 
Taarifa za kifo hapa marekani ni public info!
Na si familia inayotoa habari hizo kama wanavyodai kina Kishoka!
Habari hizo hutolewa na coroner kwenda kwenye magazet and so forth!
Na hao wenye hiyo funeral home nao wasiwasi sana kwasababu hata wao walitakiwa wawe na database yao ili tuweze kusearch watu waliokufa kama vile funeral home nyingine zinavyofanya!
Habari hizi tayari zingeshakuwa public hadi sasa!
Kwanini zinazuiliwa isivyo kawaida?
Hiyo funeral home nayo tutaichunguza tu!
 
"Mke wa sasa Balali, ni dada wa mume wa dada wa mmiliki wa gazeti la Tanzania Daima, ambalo ndilo limekuwa la kwanza kusema hizi habari.

....wakuu hiyo nayo inaniacha hoi.

Naomba hizo habari hapo juu zifanyiwe uchunguzi la sivyo kama ni za kweli then NI VERY DISTURBING!
 
Taarifa za kifo hapa marekani ni public info!
Na si familia inayotoa habari hizo kama wanavyodai kina Kishoka!
Habari hizo hutolewa na coroner kwenda kwenye magazet and so forth!
Na hao wenye hiyo funeral home nao wasiwasi sana kwasababu hata wao walitakiwa wawe na database yao ili tuweze kusearch watu waliokufa kama vile funeral home nyingine zinavyofanya!
Habari hizi tayari zingeshakuwa public hadi sasa!
Kwanini zinazuiliwa isivyo kawaida?
Hiyo funeral home nayo tutaichunguza tu!

Mushi,

kuna dada na rafiki yangu kutoka Liberia alikufa hapa kwenye state ninayoishi wiki tatu zilizopita anaitwa Fatmatha En-Opong Francis. Hebu tafuta hili jina kwenye state zote za midwest (ninakoishi mimi) uone kama kuna record yoyote.

Nakushauri ufuatilie tena facts za death records ili uone kama ulichosema hapo ni sahihi.
 
Sawa basi.
Balali naye hana rekodi kama huyo Fatmatha En-Opong Francis!
Are you happy now?
 
Halafu kuna mtu alituma posting huko kwa mithupu kuwa eti Mwafrika wa Kike ni back up profile name ya MKJJ!
Is it true ama ni conspiracy theory nyingine? Maana mara zote yeye hujitetea kuwa anapika jikoni!
Maana naona mko bega kwa bega kama mapacha!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom