Hana hoja, ana hoja gani ni kujipendekeza tu. Kafulila is a spent force.Jibu hoja zake Kama kweli wewe Ni mzalendo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hana hoja, ana hoja gani ni kujipendekeza tu. Kafulila is a spent force.Jibu hoja zake Kama kweli wewe Ni mzalendo
Kwani Lissu ana nini ? Si alisema kwenye suala la madini tutashitakiwa MIGA, je, tulushitakiwa ? Huyo ni wa kawaida sana tu.Sasa kafulila nae anajilinganisha na lissu??
Kumjibu Lissu kunamfanya na yy aonekane alishapotea huyoDuuh hapa naona blah blah za kufukia shimo!Kafulila anatumia ujinga wa watanzania kuwahadaa na hoja nyepesi!
Amini nakuambia kila mtu anaichukia CCM ya sasa anaichuki kwa sababu zake binafsi, either amekosa safari za nje, au amekosa seminar za ndani na za nje, rushwa iliyokua imehalalishwa, au mfumo wa awamu hii umesababisha biashara zake, kazi, au vitega uchumi visivyokua na maslahi kwa taifa kufa, ila wanakuja kuunganishwa na kitu kimoja tuu kwamba sababu ya kukosa maslahi ni Magufuli; ndio maana hata ukiwauliza hawana majibu ya kuridhisha na wengi wanaishia kutoa matusi na kufoka.
Tanzania ni yetu wote hakuna mwenye nchi nyingine, kila mtu akiweza kuongea points wenye takwimu sahihi kama alivyoongea Kafulila itasaidia kuelimishana na kufanya maamuzi sahihi
Ukichunguza kwa makini utagundua kuwa toka Lissu arudi nchini tabia ya mh propesa Magufuli libadilika ghafla; akawa mpoleeeeee.
Huyu jamaa atakuwa mpole zaidi akienda Bukoba kwa Wahaya kuomba kura!! Akidhania wamesahau matusi aliyowatukana baada ya tetemeko.
Mtukufu mwenyekiti wa CCM lazima awe mpole kwani vyombo vya uchunguzi vya kimataifa wakiwemo Scotland Yard, FBI, CIA, wapelelezi wa mahakama ya uhalifu The Hague wapo Tanzania wanamchunguza kwa siri kuorodhesha madhambi yake yote
Njaa mbaya sana.Pumba tupu hivi ya maisha tuliyonayo hapa Tz hali ya duni ya uchumi inajionesha wazi haina hata haja ya hao wadau hadi waseme,yaani huyo kafulila anaingea as if anaishi rwanda hayupo Tanzania.
hivi hii hali ya uchumi wa watu na biashara ndogo hadi kubwa kuanguka tunaziona kwa macho yetu mnadanganya danganya ili iweje,ni muda wa kumwambia magufuli atatue changamoto za kiuchumi.
hata rate ya watu kufa imeongozeka kutokana na chumi mbovu za watu.
Kwa uandishi huu siwezi kukushangaa. Hata hayo maisha unayosema mazuri Ni kutojitambua tu kwamba maisha mazuri yanatakiwa yaweje! Pole !VIJANA WENZANGU HAKUNA MAISHA RAHISI KWENYE NCHI ZINAZOENDELEA NI WAPUUZII PEKEE WANAOFIKILI KUBADALISHA VIONGOZI WA KISIASA KUTABADILISHA MAISHA YAO KATIKA UTAWALA HUU HUU WA MAGU VIJANA TUMEJIAJILI KWENYE UFUGAJI KILIMO NA BIASHARA NDOGONDOGO TUNAISHI MAISHA MAZURI KWANINI SISI TUWEZE NYINYI MSHINDWE SABABU NI UVIVU NA AKILI TEGEMEZE NA KUSUBILI SERIKALI IWAFANYIE KILA KITU VIJANA AMKENI MJITUME MAISHA NI HATUA WACHA KABISA
POROJO TUPU EBU SEMENI KWA MIAKA 60 MUMEFANYA NINI LAAMAANA NA NCHI IMESHEHENI RASILIMALI ZISIZO KUWA NA IDADI POROJO HATUTAKIIIIIIIIIIIIIIIII IVI JIYE NI VIZIWI HAMUSIKIIAliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma kusini kwasasa Jimbo la Uvinza amejibu hoja zilizotolewa jana na Mgombea kiti cha Urais wa JM !-
LISSU APANGULIWA HOJA 7 KWA MIKWAJU 7 YA TAKWIMU NA KAFULILA!
NIMEONA MATOBO 7 HOJA ZA LISSU!
Na David KAFULILA,
Agosti31, 2020.
Kwanza nashukuru sasa kuona ndugu yangu Tundu Lissu ameanza kuleta hoja zinazoweza kuanza kujadilika kama mgombea, tofauti na mwanzo ambapo ilikuwa ni masimulizi ambayo kwakweli hayakuwa na lolote la kusaidia maamuzi ya mpiga kura.
Jana nilifuatilia hotuba yake iliyokosoa masuala kadhaa ambayo nimeona si busara ayatumie kupotosha Watanzania kufanya maamuzi katika misingi ya upotoshaji.
Ili kurahisisha, nimepanga mawazo yangu katika mafungu 7;
1. Lissu anasema Ripoti ya Benki ya Dunia ya Mwaka huu 2020 kuhusu urahisi wa kufanya Biashara( Easy of Doing Business Report 2020) imeishusha Tanzania kutokana na utawala wa JPM.
Asichokijua Lissu na wenzake wanaotumia hoja hiyo ni kwamba tayari Benki hiyo hiyo ya dunia (WB), katika taarifa yake ya tarehe ya juzi Agosti 27,2020, imeifuta tathimini hiyo ya Mwaka 2020 na ile ya 2018.
Benki ya Dunia imeleza wazi kuwa tathimini hizo zilikuwa na kasoro nyingi za kiuweledi na hivyo kukosa uhalisia. Kwa maelezo zaidi soma ....
Doing Business – Data Irregularities Statement
2. Lissu anashangaa inawezekanaje tuingie uchumi wa kati wakati tathimini ya taasisi ya MOODYS imeonesha Tanzania imeshuka daraja kutoka B1 Mwaka 2017 kwenda B2 Mwaka 2020 katika uwezo wa kukopa! ( credit rating).
# Hili ni suala la uelewa tu kwani, kwanza; hakuna uhusiano kati ya madaraja ya uchumi yanayopangwa na Benki ya dunia na madaraja ya uwezo wa kukopa yanayopangwa na taasisi zinazofanya tathimini hizo (GLOBAL CREDIT RATING AGENCIES) ikiwemo MOODYS.
#Ndio maana Mwaka 2017, Tanzania ilikuwa daraja la juu ( B1) kuliko Kenya (B2) kwenye ripoti za MOODY'S, ilhali Tanzania ilikuwa haijafuzu kuingia uchumi wa kati na Kenya ilikuwa tayari uchumi wa kati.
#Kujua kwamba Tanzania ilipewa daraja la juu kuliko Kenya Mwaka 2017, soma Gazeti la Daily Business la Kenya la Machi4,2017-link
US agency assigns Tanzania higher credit rating than Kenya
#Zaidi ni vema Lissu akafahamu kwamba kufuatia mtikisiko wa uchumi duniani uliosababishwa na mlipuko wa ugonjwa wa korona (COVID-19), nchi nyingi zimetikiswa kutokana na mtikisiko wa mnyororo wa biashara duniani (Global supply chain) ingawa ni kwa viwango tofauti.
# Ndio maana hata Kenya ambayo Mwaka 2017, taasisi ya MOODYS waliwapa daraja la B2 ikiwa na alama chanya (B2 with positive outlook), Mwaka huu 2020, imendelea kuwa na B2 lakini kwa alama hasi (B2 with negative outlook).
#Kiwango hicho ni chini ya Tanzania yenye daraja B2 chanya (B2 with positive outlook).
# Sijui kwa mtazamo wa Lissu huenda Kenya iliyopewa na MOODYS daraja chini ya Tanzania Mwaka huu angesema nayo ishushwe daraja kiuchumi kiasi gani kutoka uchumi wa kati.
# Pia ni vema ikafahamika kwamba serikali zinazoendeshwa kisasa duniani hutumia taasisi hizi kama MOODYS kufanyiwa tathimini. Na kwa Tanzania, kwa mara ya kwanza tumefanyiwa tahimini Mwaka 2017, chini ya JPM.
#.Hii ni kwasababu JPM anaamini katika usasa wa ukweli (real modernization) tofauti na Lissu anayedhani kuendesha uchumi kisasa ni kutozibana kampuni za madini kulipa kodi stahiki.
3.Hoja kwamba deni la Taifa wakati JK anaondoka lilikuwa trilioni 20 na kwamba katika awamu ya tano limeongezeka kufikia trilioni 40.
# Hili nalo ni suala la ufahamu kwani ingawa kweli deni limeongezeka lakini takwimu hizo sio za kweli. Wakati Lissu anasema JK aliacha deni la Trilioni 20, ukweli ni kwamba deni la nje peke yake Mwaka 2015....lilikuwa zaidi ya dola Billioni 16.4 au zaidi ya Trilioni 30TZS wakati huo, achilia mbali deni la ndani ambalo lilikuwa zaidi ya Trilioni 8.7TZS. (Chanzo- BoT Monthly Economic review).
# Usahihi wa takwimu na taarifa sahihi ni jambo muhimu sana hasa kwa Kiongozi anayetafuta kuaminika. Sijui Lissu hizi takwimu za trilioni 20 kazitoa vyanzo gani?
4.Lissu anasema uwezo wetu wa kuhimili deni umeshuka kwasababu deni limezidi kuwa kubwa.
# Labda nitoe ufahamu wa jumla tu kwamba tatizo la deni kwenye uchumi wowote linapimwa kwa vigezo zaidi ya ukubwa wa deni, bali vigezo vya uhimilivu (debt sustainability).
# Na dalili za wazi ambazo mtu wa kawaida anaweza kuzitumia kujua tuna tatizo la deni au lah!, ni kiwango cha riba unachotozwa kukopa.
#Serikali inapokuwa na hali mbaya kiuchumi (desperate) inakopa kwa riba kubwa kuliko Serikali yenye hali nzuri kiuchumi.
#Ndio sababu Mwaka 2015 kipindi ambacho serikali ilibidi kukopa ili kulipa mshahara watumishi, ilikopa soko la ndani kwa riba ya mpaka asilimia 17% kwa hatifungani za siku 365 Mwaka 2015, kulinganisha na kipindi cha JPM, ambapo Serikali inakopa kwa riba ya asilimia 4.8% kwa hatifungani za siku 365.
# Hiyo ni hali ya kawaida hata kwa maisha binafsi, kwamba ukiwa hoi kiuchumi (desperate) hutojali ukubwa wa riba unapotaka mkopo, lakini ukiwa vizuri kiuchumi huwezi kuchukua mkopo kwa riba kandamizi.
#Ninachojaribu kusisitiza ni kwamba afya yetu kiuchumi kumudu kukopa bado ni kubwa kwa vigezo vyote ndio maana Serikali inakopa kwa riba chini katika rekodi ya zaidi ya miaka10, na kwa vigezo vya tathimini za MOODY'S hakuna anayetuzidi afya hiyo ukanda huu.
5.Lissu anahoji umakini wa Serikali ya JPM kusimamia biashara na Sekta binafsi.
# Kifupi JPM amerejesha biashara na sekta binafsi kwenye reli, kutoka biashara za mishentaun kwenda biashara halisi. Bahati mbaya kila nikiwasikiliza Lissu na Membe naona fikra zao ni turudi uchumi wa 'mishemishe'
# Lissu anataka kupotosha Watanzania kama alivojaribu kwenye sekta ya madini wakati Rais alipoamua kuchukua hatua thabiti. Lissu alisema maamuzi ya madini yangeua sekta ya madini, lakini cha kushangaza mauzo ya dhahabu tu nje ( export) yameongezeka kutoka dola bilioni 1.3 mwaka 2015 mpaka dola bilioni 2.1 mwaka 2019.( BoT-MER)
# Lissu anapotosha Watanzania kuwa biashara chini ya JPM tunafanya vibaya kuliko kabla, nimkumbushe tu kwamba namba hazidanganyi. Mauzo ya Tanzania nje ya nchi Mwaka 2015 yalikuwa dola bilioni 8.9 kulinganisha na dola bilioni 9.7Mwaka 2019.
6. Lissu anahoji uamuzi wa kununua ndege kwamba haukupitishwa na Bunge.
# Labda hili lieleweke tu kwamba uamuzi wa kununua ndege haukupitishwa na upinzani bungeni sio bunge ingawa ilikuwa hoja ya upinzani mabunge yote kabla ya awamu ya tano kuingia na ilikuwa sehemu ya Ilani ya Chadema ya mwaka 2015 (rejea Ukurasa wa 40 Ilani ya Chadema).
#Ukweli kauli ya Lissu kwamba Bunge halikuhusjshwa ununuzi wa ndege ni ya kusikitisha mno kutolewa na mgombea nafasi ya juu kabisa ya nchi.
#Nasema hivi kwasababu bajeti ya ununuzi wa ndege kwa mara ya kwanza imepitishwa katika Bunge la Bajeti la 2016/17 ambapo ilitengwa na kupitishwa kiasi cha Trilioni 1.49TZS
# Naomba ifike wakati ieleweke na tuweke kumbukumbu sawa kwamba tumetoka zama ambazo tulikodi ndege mbovu kwa dola milioni 43 mpaka zama za kununua ndege mpya bombardier kwa dola milioni 32...( Ripoti ya CAG , Aprili 2020).
#Tumetoka zama za kujadili Taifa kukosa ndege mpaka zama za Taifa la kujadili namna ya kununua ndege (kwamba kununua kwa taslimu au kukopa). Huko nyuma hata uwezo wa kukopa hatukuwa nao.
7.Mwisho nihitimishe kwa kujadili hoja ya Lissu kuhusu Bima ya Afya nchini;
# Labda niseme kwamba nilipokuwa Songwe kama Katibu Tawala Mkoa, wananchi vijijini walionesha mwitikio mkubwa sana kuhusu bima ya afya hata ile ya chini kwa maana ya CHF.
# Songwe ulikuwa mkoa wa kwanza kwa kaya zenye bima ambapo asilimia76% walikuwa na bima hiyo.
# Mwitikio wa wananchi kwa bima ni kitu halisi hasa baada ya Serikali kuongeza upatikanaji wa dawa na vifaa tiba. ( kutoka kutengewa billioni 31 mpaka billioni 270).
# Ndio maana idadi ya Watanzania wanaotumia bima iliongezeka kutoka takribani wanufaika milioni 9.8 Mwaka 2015 mpaka zaidi ya milioni 16.7 mwaka 2019..
#Nimshauri Ndugu yangu Lissu awe anafanya tafiti ya anayolishwa na wenzake kabla hajayamwaga majukwaani. Moja ya sifa za kiongozi bora ni kujiridhisha na taarifa kabla ya kuziweka hewani.
Yaa jeska kishoa kule kwa mwiguluHivi aligombea ubunge?
kawaida tumbili hana uwezo kuyaona hayoKafulilla anasahau kuwa "analishwa na mkewe ambaye ni Chadema"!!! Anajifanya ccm ndio inamfuga atakuja kuachwa aaibike
Kafulila is one of the smartest guys waliopo kwenye system ya Nchi yetu. Aliwahi kumuaibisha Profesa mmoja Bungeni siku moja. Huyu mtu yuko smart siyo kawaida,,,,,,, I like smart peopleAliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma kusini kwasasa Jimbo la Uvinza amejibu hoja zilizotolewa jana na Mgombea kiti cha Urais wa JM !-

Shukrani,vipi na Kafulila je hakugombea?Yaa jeska kishoa kule kwa mwigulu
Naunga mkono hoja,japo ana madhaifu yake JPM,ila kwa level za kibongobongo,hasa ukianaglia idadi ya wajinga wengi walio nchini,aliyoyafanya kwa vitendo hii miaka mitano kuna kura ashajiakikishia.Kafulila is one of the smartest guys waliopo kwenye system ya Nchi yetu. Aliwahi kumuaibisha Profesa mmoja Bungeni siku moja. Huyu mtu yuko smart siyo kawaida,,,,,,, I like smart people
Mimi nashauri kuwa JPM wala asijaribu kabisa hata siku moja kujibu hoja za wagombea wenzake, yeye ajikite tu katika kutangaz ilani yake ya uchaguzi tu basi! JPM kama Rais ambaye tayari ameshakaa madarakani miaka mitano, ameshaondoka kwenye hadhi ya majibizano ya hoja za namna hii, hizi atuachie sisi wanachi tutaendelea kuzijadili mitaani kwetu
Ukosefu wa elimu ya ujasiriamali ndiyo tatizo kubwa kwenu, soma kuhusu mjasiriamali na mambo yanayo mzunguka nyie mnadhani mnaokoa pesa wakati mna sababisha watu wawe masikini kodi zinatokana na wafanyakazi na kuchangamka kwa biashara huwezi kupanga muendelezo wa biashara kwa sera za majukwaani ambazo hazidumu na hazina sheria na kanuni za kuzisimamia. Read these two lessons in entrepreneuship 'cost benefit conscious and an entrepreneur and his enviroments'Hiki ndo nnchokataa huwezi kuniaminisha kwamba utapeli ndo njia sahihi ya kuwapa maish bora wananchi. Kumbuka hizo walizookoa zinaenda kufanya sehemu ingine. Hakikisha unafanya kazi kwa bidii upate stahiki yako, panga mahitaji yako, weka malengo yako hiyo ndo njia bora ya kuweza survive.