David Kafulila anakumbukwa na wakulima wa Simiyu kwa kupaisha bei ya Pamba kufikia Tsh. 2200 kwa kilo katika historia ya Taifa letu alipokuwa RC

Hata kwetu Songwe alipokuwa RAS alirudisha chenji ya Mradi ya TZS 2.4bil nakubaliana na Uadilifu wa Kafulila
 
Alipewa pesa ili kujenga Makao Makuu ya Mkoa kama Ras baada ya kukamilisha majengo yale kwa BOQ elekezi akasaza 2.4 akamkabidhi Rais Magufuli.
Haya maneno ni ya kweli? Hivi huyu jamaa ni Mshamba au ni Mzalendo na kwani Uzalendo ndio huu?
 
Hata kwetu Songwe alipokuwa RAS alirudisha chenji ya Mradi ya TZS 2.4bil nakubaliana na Uadilifu wa Kafulila
Kweli kabisa alifanya vyema sana. Nakumbuka mwaka 2020 wakati akisoma taarifa mbele ya waziri mkuu na kueleza kiasi walichookoa katika ile Billion 6 kwa kutumia Fosi akaunti .aliongea vizuri sana na bahati nzuri siku ile nilikuwepo pale ofisi za Mkoa zilizopo kata ya Mlowo Eneo la Nselewa. Tena kwa bahati nzuri nilikuwa karibu yake kabisa wakati anasoma taarifa,nilikuwa nimesimama jirani na Mhessimiwa David Silinde ambaye pia alipewa nafasi ya kuzungumza siku ile. watu wa Songwe wanamkubali sana Mheshimiwa Kafulila. Hata Soko la pale Mlowo ni yeye alihakikisha linakamilika kwa haraka na uharaka na kwa muonekano mzuri.hapo pia nilifanikiwa kumuona kwa karibu sana.siku hiyo alikuwa amekuja kukagua na kuangalia kaburi moja pale lililotakiwa kuhamishwa maana walizikaga wakati mji haujawa mkubwa. Kwa hiyo Mheshimiwa Kafulila namfahamu vyema kwa uchapa kazi wake..
 
Binafsi Sina mashaka na Kafulila hata kidogo
 
Unajua mamlaka aliyonayo Mkuu wa Mkoa?
Mkuu wa Mkoa ni Rais wa Mkoa,
Sasa kama Pamba ilitoka kuuzwa TZS 800 hadi 2,200 na Leo hayupo bei ni 1,000 why tusiamini Kuna uhuni kule wakulima wanafanyiwa?
Kwahiyo walaumiwe CHADEMA?
 
Kimsingi serikali kupitia NFRA inapaswa kununua mazao ya wakulima kila wakati wa mavuno ili kudhibiti wafanyabiashara wahuni wanaomkandamiza mkulima. Serikali haiwezi kosa hata 300b ikanunua sehemu kubwa ya mazao kwa bei nzuri. Hakuna haja ya kuwa na vyama vingi vinavyoitwa vya ushirika.. NFRA ikijipanga inatosha kufanya hilo jukumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…