David Kafulila anakumbukwa na wakulima wa Simiyu kwa kupaisha bei ya Pamba kufikia Tsh. 2200 kwa kilo katika historia ya Taifa letu alipokuwa RC

Kwanini unadhalilisha watu wewe,

Kusugua makalio ndio nini?

Kama mliweza kumfanyia fitna mtu aliyeleta neema kwa wakulima kisa maslahi yenu basi shame on you.

Najua Mama hatakuja kurudia kosa kama hilo kwa Kafulila.

Najua Mama anasoma sana humu Jf namtahadharisha kuna baadhi ya watu kazi kwao ni uongo na fitina tu Wala hakuna kazi wanafanya.

Mtu kama Kafulila anasaidia hata Rais atawale kwa raha kwani ni mtu anajua kuzikabili hoja zote toka ndani na nje ya Serikali,

Lakini pia ni mtu ukimpatia elfu 5 itafika kwenye mradi elfu 5 kama ilivyo.

Vijana tuache kufitiniana sio sawa na Mungu hakubaliani na mtu Mwongo na Mchawi.
 
Napenda sana mtu anayetumia hoja kama wewe ili kujifunza wote. Sasa naomba unisaidie kidogo kile umesema nisome japo ni maelezo yako.
Je Kafulila alianzisha Ushirika au alianzisha mfumo wa Ushirika kushindana na Kampuni binafsi? Kwamba Ushirika ununue na watu binafsi wanunue?
U.esema kamati ya kuthibiti walanguzi. Je kipi ni kipi mfumo wa watu binafsi kununua kama aliuruhusu unautofautishaje na ulanguzi?
Yeye na Mtaka nani alianzisha nini? Kwa Simiyu kama hupajui Mtaka ndio mkuu wa Mkoa alikubalika, bado hajapatikana mwingine.
Ova. Noya du. Iyingi bulongo guke
 
Asante sana mkuu kwa ujio wako humu,
Hawa vijana wa Mtaka naona ni kama wabifu
Kafulila kitu pekee kitambeba kwenye maisha yake ni Zero corruption status.
 
Kila kitu Mtaka Mtaka Mtaka, 🤣🤣

Sasa kama MNEC alikuwa anamiliki Soko la madini na Sheria ziko wazi Soko la madini lazima iwe mali ya Serikali Mtaka alikuwa wapi?

Kama wachina wa CHICCO walikuwa wamebumba barabara zaidi ya KM20 MWIGUMBI -MASWA ndio Kafulila kuwaambia warudie kwa gharama zao na wakafanya hivo kwa zaidi ya 40bl huyu Mtaka alikuwa wapi?

Wakati wakulima hao masikini wanalanguliwa Pamba yao na kuiza kwa TSH 800 au 1000 huyu Mtaka wako alikuwa wapi?

Nimesoma ulichoandika nikacheka sana aisee.🤣🤣🤣

Nikusahihishe tu ndg yangu wanamchukia Kafulila sio masikini na wanyonge ila ni hawa wamiliki wa Masoko ya madini na wazee wa 10% kwa Wachina pamoja na wachuuzi wa Pamba hawa ni kweli wanamchukia sana nakubaliana na wewe 100%✓
 
Huku juu umeanza vizuri sana ila chini umeharibu Kila kitu kuanza kumtaja taja huyo mtakatifu.

Binafsi nahisi shida kubwa ya Simiyu ni huyo huyo Mtakatifu.

So endelea ku-enjoy Jf

 
Kinachokusumbua wewe ni wivu na chuki binafsi tu. Kwanza ungekuwa na akili sawasawa ungejiuliza wapo watanzania wangapi ambao wangeweza kuteuliwa na Mheshimiwa Rais?kwanini hawakufikiriwa hao na badala yake akapewa heshima hiyo ya kuwa mkurugenzi wa PPP? Kwanini hukuteuliwa hata wewe tu au mimi na badala yake akapewa heshima hiyo Mhessimiwa Kafulila? Kufikiriwa tu na Mheshimiwa Rais na kupewa nafasi ni heshima kubwa sana.

Mimi nitaendelea kumuunga mkono Mheshimiwa Rais kwa sababu ni kiongozi na mtu safi, mzalendo,mchapa kazi na mbunifu kazini. Ni kiongozi asiyeyumba kiuongozi.
 
Kwa hoja hizi nzito ulizomjibu huyo asiye elewa kitu chochote kile na mwenye wivu na chuki binafsi na Mheshimiwa Kafulila ,itakuwa huko aliko anatafuta panadol ili anywe kupunguza maumivu ya kichwa na kuishiwa nguvu.
 
Wana Simiyu wanaelewa vyema sana kuwa Mhessimiwa Kafulila ni jembe na chuma kilichowainua na kuwapatia bei kubwa sana katika Historia ya Nchi yetu
 
Mheshimiwa Kafulila ni mzalendo wa kweli kwa Taifa letu.aligona kupokea ma Million kwa mamillioni ili aachane na sakata la Escrow ,Lakini kwa uzalendo wake aligoma kabisa kupokea na kukubali pesa chafu na badala yake akaongeza moto zaidi kwamafisadi na wala rushwa wote.
 
Kwa hoja hizi nzito ulizomjibu huyo asiye elewa kitu chochote kile na mwenye wivu na chuki binafsi na Mheshimiwa Kafulila ,itakuwa huko aliko anatafuta panadol ili anywe kupunguza maumivu ya kichwa na kuishiwa nguvu.
Jamaa anatumika vibaya na huyo Mtakatifu ambae bila huruma anatesa Wanawake wasio na hatia.

Hajui Kama nyota ya mtu inang'aa inang'aa tu.
 
Naona machawa mnapongezana.
Bora hata ile misukule ya Lumumba iliyokuwa inalipwa buku mbili na bundle kuja kupost upupu, kuliko hii michawa ya sasa.
Poor CCM.
Kama umeumia basi wewe kunywa hata sumu tu ndugu yangu ili UFE tu maana huna faida zaidi ya wivu na chuki.
 
Bei ya pamba haipangwi na Mkuu wa Mkoa wewe chawa mchafu
Uko sahihi

Simiyu akiwa mkuu wa mkoa Kafulila aliumiza sana watu huyo Kafulila alizuia magari ya abiria Kwa jina maarafu michomoko yasifanye hiyo biashara siji msahau Usafiri ulikuwa taabu hatari

Baada ya malalamiko ya wananchi na wauzaji vituo vya mafuta kuwa biashara zao zinadoda Raisi akamwondoa ukuu wa mkoa Simiyu haraka haikuchukua hata muda

Mpuuzi huyo alileta mateso sana Kwa wananchi wa Simiyu
 
Jamaa anatumika vibaya na huyo Mtakatifu ambae bila huruma anatesa Wanawake wasio na hatia.

Hajui Kama nyota ya mtu inang'aa inang'aa tu.
Ni ngumu sana kuizima au kuifikisha nyota ya Mheshimiwa Kafulila katika mioyo na akili za watanzania,kwa sababu wanakumbuka na kuziona alama alizoziacha na kazi kubwa aliyoifanya katika taifa letu.
 
Wewe ni liongo sana na mzushi sana.
 
Thread moja bei gani
 
Nenda hata leo kule Simiyu halafu tamka neno Kafulila au mama Samia kama hutatukanwa.

Lakini fika hapo hapo Simiyu halafu tamko Magufuli au Mtaka uone namna utakavyoshangiliwa.

Kwa wana Simiyu, kwa sasa Kafulila ni neno la kulaaniwa.
Mheshimiwa Rais pamoja na Mheshimiwa Kafulila wanakumbukwa sana na wana Simiyu.
 
Thread moja bei gani
Haina bei bali ni uzalendo katika kuwatetea na kuwaunga mkono WAZALENDO,wachapakazi na watu safi aina ya Mheshimiwa David Kafulila Kama ilivyo kwa Mhessimiwa Daktari Samia Suluhu Hasssan.
 
Haina bei bali ni uzalendo katika kuwatetea na kuwaunga mkono WAZALENDO,wachapakazi na watu safi aina ya Mheshimiwa David Kafulila Kama ilivyo kwa Mhessimiwa Daktari Samia Suluhu Hasssan.
Nimeona umetoa single za kafulila za kutosha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…