David Kafulila anakumbukwa na wakulima wa Simiyu kwa kupaisha bei ya Pamba kufikia Tsh. 2200 kwa kilo katika historia ya Taifa letu alipokuwa RC

Kafulila tumemchoka na tabia yake ya kulipa watu Ili wamsemee mitandaoni.

Na wewe Dalali punguza njaa itakuponza. Siyo wanaume wote wanaokutumia Wana Nia njema!! Ukishaona wanaanza kukulipia na Kodi ya nyumba basi jiandae kuanza kupika na kufua nguo zao
Hii ya Leo siyo kununua tu watu bali kajiandikia kabisa mwenyewe hii article. Huyu Lucas Mwashambwa ni spika tu.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Uongozi ni kuacha alama zinazoishi katika Maisha na mioyo ya watu, ni kuacha kitu kitakacho simuliwa vizazi kwa vizazi,ni kuacha rekodi ambayo itaimbwa na kuzungumzwa na watu kwa miaka mingi hata kama wewe utakuwa haupo uongozini au Duniani lakini utaendelea kuishi na watu japo hupo Duniani au madarakani.

Uongozi siyo habari ya umeongoza miaka mingapi au umekaa miaka mingapi. kinachomfanya mtu akakumbukwa na watu ni kazi alizozifanya kwa muda alipokuwa na madaraka au hai na faida ya uhai wake kwa watu na uongozi wake ulivyogusa maisha ya watu.

Ndio maana leo hii viongozi na watu kama John F Kennedy, Dr Martin Luther King Junior, BoB Marely, Abraham Lincolin wanaendelea kukumbukwa na watu wengi sana Duniani kwote licha ya kwamba walikufa miaka mingi na waliishi miaka michache Duniani kabla ya kufikia uzee wao. Ndio maana pia viongozi kama Edward Moringe Sokoine wanakumbukwa na Taifa letu japo walikaa madarakani kwa Muda mfupi lakini historia zao na majina yao yameganda na kunasa katika mioyo ya watanzania kutokana na mikono yao na kazi zao kugusa maisha ya watu na kuleta matokeo Chanya.

Hii maana yake nini? Unaweza kuongoza kwa miaka mingi, kukaa madarakani au kwenye cheo fulani kwa miaka mingi na bado usikumbukwe na yeyote yule pale ambapo utaondoka leo. Unaweza kuondoka leo kwenye ukuu wa mkoa au uwaziri au uwaziri mkuu au uspika au ukurugenzi wa taasisi fulani halafu kesho watu wakasahau kabisa kama ulikuwepo kwenye nafasi fulani. Kwanini? Kwa sababu uongozi wako na uwepo wako kwenye kiti haukugusa wala kubadilisha maisha ya watu au mtu yeyote yule, kwa hiyo ulikuwa kama mvuke au moshi tu ambao umekuja na kupita.

Mheshimiwa David Kafulila licha ya kukaa katika nafasi ya Ukuu wa mkoa Wa Simiyu kwa muda mfupi lakini bado anaendelea kukumbukwa na wana Simiyu kama mkuu wa mkoa aliyeleta tabasamu, furaha, matumaini na kuwainua kiuchumi kwa kupaisha Bei ya pamba yao ambayo kwa karibu 70% ya pamba yote Tanzania inatokea Simiyu kufikia bei ya 2200 kwa kilo, bei ambayo haikuwa kutokea tangia Nchi yetu ipate uhuru. Leo anakumbukwa na kusemwa kuwa hapa Simiyu kilipita na kulipita CHUMA David Kafulila aliyeleta Nuru kwa wakulima na maendeleo kwa kaya za wanasimiyu.

Jiulize wewe kiongozi uliyepo kwenye cheo fulani au wadhifa fulani ukiondoka leo kwenye nafasi uliyopo watu watakukumbuka kwa lipi? Umegusa maisha ya watu wangapi? Umeleta tabasamu kwa kaya ngapi? Wangapi wamepata nuru kutoka gizani? Wangapi wamepata matumaini kupitia mikono yako? Wangapi wanatamani urejee au urudishwe au uongezewe muda au kukuombea dua na maombi mema ya kurejea au kupata cheo kikubwa au nafasi fulani? Utakumbukwa kwa lipi ndugu yangu? Au unaisha na kufanya kazi ilimradi tu watoto wako wapate ugali mezani? Umebadilisha maisha ya wangapi?

Wangapi wanaona uwepo wako hapo ulipo ni baraka na mlango wa wao kutokea kimaisha na kuinuka kiuchumi? Wangapi wanakukumbuka kwa mema?

Gusa maisha ya watu, Leta tabasamu kwa watu,washa taa kwenye mioyo ya watu,inua watu,shika mikono ya watu uwainue juu,wape matumaini watu ili siku moja Ukumbukwe kama ilivyo kwa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere,Nelson Mandela,kwame Nkrumah, Keneth Kaunda, Winnie Mandela na wengine wengi sana. Lakini pia ukifanya vyema utaungwa mkono ukiwa bado hai kama ilivyo kwa Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Akili za kibwege kabisa hizi.... Kafulila hakupandisha bei ..bei ilipanda kutokana na nchi nyingi kujifungia Kwa corona na Pamba ikawa chache sokoni...ficheni ujinga wako....kwanza unajua bei ya Pamba inavyopangwa na mgawanyo wake Kwa Wadau wote!??...
 
Naona umepaniki mpaka kuanza kutukana matusi kama mgonjwa.
 
Unajua mamlaka aliyonayo Mkuu wa Mkoa?
Mkuu wa Mkoa ni Rais wa Mkoa,
Sasa kama Pamba ilitoka kuuzwa TZS 800 hadi 2,200 na Leo hayupo bei ni 1,000 why tusiamini Kuna uhuni kule wakulima wanafanyiwa?
Hana uwezo wa kuzuia ..... Hivi mnafahamu utaratibu wa MAZAO ya kimkakati Pamba, kahawa, korosho, n.k a au mnaropoka tu!?
 
Naona umepaniki mpaka kuanza kutukana matusi kama mgonjwa.
Nakwambia Tena akili za kibwege hizo .... Acha ... Mkuu wa Mkoa hapangi bei na hana Mamlaka katika maamuzi ya MAZAO ya kimkakati yenye bodi husika ...Bodi na Wadau wakipanga bei ndio imetoka hiyo ..Kwa MAZAO yanayouzwa Kwa MnadaMtandao (Tanzania Merchantile Exchange) kama korosho na kahawa inawekwa bei dira wanashindania kwenye mnada....Sasa unakuja unafikiri watu hawafahamu.... Ficha ujinga wako
 
Endelea kuweweseka na kutapatapa wakati mzalendo wa kweli na mchapakazi akiendelea kuchanja mbuga katika mioyo ya watanzania.
Now you see?! Huu ndo mwandiko wako, inakuwaga blaa blaa. Sijui jemadari gani kabubujisha machozi ya furaha wasafwa gani huko Mbozi, leo Kafulila amekwepa blaa blaa zako kaamua kujiandikia mwenyewe
 
Huko unakosema wanamlilia huyo kafulila ndo home.Huko mtaje Antony mtaka wanabubujika na machozi maana yule jamaa ni mtu na nusu harafu yuko fiti yule jamaaa hadi raha.
Mnabubujikwa na machozi,

Huku Pamba mnauza 800,

Mnabubujikwa na machozi huku watu wanawalangua wakulima Pamba zao.

Mnabubujikwa na machozi huku CHICCO wanatengeneza barabara ya udongo badala lami,

Nyie mnabubujikwa na machozi tu duuuh.

Simiyu mmetisha.

Endeleeni kububujikwa na machozi mama atamrudisha naamini.
 
Akili za kibwege kabisa hizi.... Kafulila hakupandisha bei ..bei ilipanda kutokana na nchi nyingi kujifungia Kwa corona na Pamba ikawa chache sokoni...ficheni ujinga wako....kwanza unajua bei ya Pamba inavyopangwa na mgawanyo wake Kwa Wadau wote!??...
🤣🤣🤣
 
Nakwambia Tena akili za kibwege hizo .... Acha ... Mkuu wa Mkoa hapangi bei na hana Mamlaka katika maamuzi ya MAZAO ya kimkakati yenye bodi husika ...Bodi na Wadau wakipanga bei ndio imetoka hiyo ..Kwa MAZAO yanayouzwa Kwa MnadaMtandao (Tanzania Merchantile Exchange) kama korosho na kahawa inawekwa bei dira wanashindania kwenye mnada....Sasa unakuja unafikiri watu hawafahamu.... Ficha ujinga wako

Fuatilia kilichokuwa kinaendelea kabla, wakati na baada ya kutumbuliwa kwa Kafulila.
Kafulila alitumbuliwa na kutolewa kuwa RC wa Simayu, akawekwa benchi, akasugua makalio, akaanza uchawa mitandaoni, akakumbukwa na kupewa cheo cha mchongo kwenye uwekezaji. Ni kacheo fulani hivi ka ovyo, sasa jamaa naona hajaridhika nako maana hakampi upigaji wa kingedere, ndio maana kaswaga machawa kibao hapa JF wakumpa promo ili kuboost uteuzi mwingine.
Click to expand...
Kwanini unadhalilisha watu wewe,

Kusugua makalio ndio nini?

Kama mliweza kumfanyia fitna mtu aliyeleta neema kwa wakulima kisa maslahi yenu basi shame on you.

Najua Mama hatakuja kurudia kosa kama hilo kwa Kafulila.

Najua Mama anasoma sana humu Jf namtahadharisha kuna baadhi ya watu kazi kwao ni uongo na fitina tu Wala hakuna kazi wanafanya.

Mtu kama Kafulila anasaidia hata Rais atawale kwa raha kwani ni mtu anajua kuzikabili hoja zote toka ndani na nje ya Serikali,

Lakini pia ni mtu ukimpatia elfu 5 itafika kwenye mradi elfu 5 kama ilivyo.

Vijana tuache kufitiniana sio sawa na Mungu hakubaliani na mtu Mwongo na Mchawi.

Kwa hiyo PPP bajeti yake inaombwaje na kuidhinishwa bungeni?
Nani anaiombea? Kafulila?!
PPP iko chini ya Idara ya Fedha ila inajitegemea kama ilivyo TRA.

Soma hii itakusaidia,
👇👇👇

Kafulila alianzisha kitu kinaitwa "Simiyu model" .

Nia ya hii Model ni kutaka Ushirika kushindana na watu binafsi katika ununuzi wa Pamba.

Lakini pia Kafulila alianzisha kamati za pamba kudhibiti Kila hujuma ya walanguzi wa Pamba.

Matokeo ndio hayo bei ikafika mpaka 2200 wakati miaka yote bei ya pamba haijawahi kuzidi 1,200 kwa mkulima.

Ndio Wapo watu kama wewe mnaoweza kusema sababu ni kupanda kwa bei ya pamba katika soko la dunia dine,

Ukweli ni kwamba haukuwa mwaka wa kwanza bei kupanda katika soko la dunia na bado bei haikuzidi 1200/.

Mfano wa miaka ambayo Pamba ilipanda sana katika Soko la dunia ni Mwaka 2011, 2012, 2018 katika miaka hii bei ya pamba katika soko la dunia ilipanda na bado mkulima hakupata zaidi ya 1200/=.

Sasa huyu Kafulila alidhibiti chain ya wapigaji eneo la pamba ndani ya Mkoa mpaka kwenye mfumo wa wanunuzi.

Mimi naombeni watu waje wafanye utafiti alichofanya Kafulila na kilichotokea kwenye bei ya pamba ili kitumike kama mwongozo wa Serikali Kwa manufaa ya Sasa na kizazi kijacho.

Ukiongea na wazee wa pamba hapa Simiyu au mchambuzi wa miaka kama Mzee Joseph Mihangwa watakwambia yule kijana alikata mtandao wote wanaokula jasho la mkulima wa pamba.

Tunaweza kuzungumza mengi lakini Kafulila bado ni mtu mwenye uthubutu na ujasiri mkubwa wa kiuongozi.
 
Kwanini unadhalilisha watu wewe,

Kusugua makalio ndio nini?

Kama mliweza kumfanyia fitna mtu aliyeleta neema kwa wakulima kisa maslahi yenu basi shame on you.

Najua Mama hatakuja kurudia kosa kama hilo kwa Kafulila.

Najua Mama anasoma sana humu Jf namtahadharisha kuna baadhi ya watu kazi kwao ni uongo na fitina tu Wala hakuna kazi wanafanya.

Mtu kama Kafulila anasaidia hata Rais atawale kwa raha kwani ni mtu anajua kuzikabili hoja zote toka ndani na nje ya Serikali,

Lakini pia ni mtu ukimpatia elfu 5 itafika kwenye mradi elfu 5 kama ilivyo.

Vijana tuache kufitiniana sio sawa na Mungu hakubaliani na mtu Mwongo na Mchawi.

PPP iko chini ya Idara ya Fedha ila inajitegemea kama ilivyo TRA.
Soma huu mzigo wote itakusaidia
 
Mnabubujikwa na machozi,

Huku Pamba mnauza 800,

Mnabubujikwa na machozi huku watu wanawalangua wakulima Pamba zao.

Mnabubujikwa na machozi huku CHICCO wanatengeneza barabara ya udongo badala lami,

Nyie mnabubujikwa na machozi tu duuuh.

Simiyu mmetisha.

Endeleeni kububujikwa na machozi mama atamrudisha naamini.
Labda anafikiria wakulima ni wajinga kama yeye kwamba wanapenda sana kuuza pamba zao kwa bei ya chini.
 
Kafulila ni mwizi tu.
Kafulila angeacha kuendekeza tumbo huenda angefika mbali na kuheshimiwa, lakini pale ni tumbo tu linamtesa. Kajamaa ni kajinga halafu kana tamaa balaa.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Uongozi ni kuacha alama zinazoishi katika Maisha na mioyo ya watu, ni kuacha kitu kitakacho simuliwa vizazi kwa vizazi,ni kuacha rekodi ambayo itaimbwa na kuzungumzwa na watu kwa miaka mingi hata kama wewe utakuwa haupo uongozini au Duniani lakini utaendelea kuishi na watu japo hupo Duniani au madarakani.

Uongozi siyo habari ya umeongoza miaka mingapi au umekaa miaka mingapi. kinachomfanya mtu akakumbukwa na watu ni kazi alizozifanya kwa muda alipokuwa na madaraka au hai na faida ya uhai wake kwa watu na uongozi wake ulivyogusa maisha ya watu.

Ndio maana leo hii viongozi na watu kama John F Kennedy, Dr Martin Luther King Junior, BoB Marely, Abraham Lincolin wanaendelea kukumbukwa na watu wengi sana Duniani kwote licha ya kwamba walikufa miaka mingi na waliishi miaka michache Duniani kabla ya kufikia uzee wao. Ndio maana pia viongozi kama Edward Moringe Sokoine wanakumbukwa na Taifa letu japo walikaa madarakani kwa Muda mfupi lakini historia zao na majina yao yameganda na kunasa katika mioyo ya watanzania kutokana na mikono yao na kazi zao kugusa maisha ya watu na kuleta matokeo Chanya.

Hii maana yake nini? Unaweza kuongoza kwa miaka mingi, kukaa madarakani au kwenye cheo fulani kwa miaka mingi na bado usikumbukwe na yeyote yule pale ambapo utaondoka leo. Unaweza kuondoka leo kwenye ukuu wa mkoa au uwaziri au uwaziri mkuu au uspika au ukurugenzi wa taasisi fulani halafu kesho watu wakasahau kabisa kama ulikuwepo kwenye nafasi fulani. Kwanini? Kwa sababu uongozi wako na uwepo wako kwenye kiti haukugusa wala kubadilisha maisha ya watu au mtu yeyote yule, kwa hiyo ulikuwa kama mvuke au moshi tu ambao umekuja na kupita.

Mheshimiwa David Kafulila licha ya kukaa katika nafasi ya Ukuu wa mkoa Wa Simiyu kwa muda mfupi lakini bado anaendelea kukumbukwa na wana Simiyu kama mkuu wa mkoa aliyeleta tabasamu, furaha, matumaini na kuwainua kiuchumi kwa kupaisha Bei ya pamba yao ambayo kwa karibu 70% ya pamba yote Tanzania inatokea Simiyu kufikia bei ya 2200 kwa kilo, bei ambayo haikuwa kutokea tangia Nchi yetu ipate uhuru. Leo anakumbukwa na kusemwa kuwa hapa Simiyu kilipita na kulipita CHUMA David Kafulila aliyeleta Nuru kwa wakulima na maendeleo kwa kaya za wanasimiyu.

Jiulize wewe kiongozi uliyepo kwenye cheo fulani au wadhifa fulani ukiondoka leo kwenye nafasi uliyopo watu watakukumbuka kwa lipi? Umegusa maisha ya watu wangapi? Umeleta tabasamu kwa kaya ngapi? Wangapi wamepata nuru kutoka gizani? Wangapi wamepata matumaini kupitia mikono yako? Wangapi wanatamani urejee au urudishwe au uongezewe muda au kukuombea dua na maombi mema ya kurejea au kupata cheo kikubwa au nafasi fulani? Utakumbukwa kwa lipi ndugu yangu? Au unaisha na kufanya kazi ilimradi tu watoto wako wapate ugali mezani? Umebadilisha maisha ya wangapi?

Wangapi wanaona uwepo wako hapo ulipo ni baraka na mlango wa wao kutokea kimaisha na kuinuka kiuchumi? Wangapi wanakukumbuka kwa mema?

Gusa maisha ya watu, Leta tabasamu kwa watu,washa taa kwenye mioyo ya watu,inua watu,shika mikono ya watu uwainue juu,wape matumaini watu ili siku moja Ukumbukwe kama ilivyo kwa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere,Nelson Mandela,kwame Nkrumah, Keneth Kaunda, Winnie Mandela na wengine wengi sana. Lakini pia ukifanya vyema utaungwa mkono ukiwa bado hai kama ilivyo kwa Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Kafulila hana doa zaidi ya kuhama Upinzani kuja CCM ila ni kijana mzuri
 
Back
Top Bottom