David Kafulila atolea ufafanuzi wa Adani kuwekeza katika Miundombinu ya Umeme kwa Ubia

Serikali ya CHURA akuna inacho weza zaidi ya udalali TU.
Kenya wanawakataa nyie mnawakumbatia.
Takataka kabisaa
 
Adinani na DP weldi Zote ni wizi, kama nchi kwanini tusiuze hisa au au kama shida ni Sisi wa Bongo na akili zetu za Kibongo , tusiweke Management ya wataalamu kutuendeshea hayo mashirika , baada la kuwapa watu wa nje hiyo Bandari au Umeme au Mwendokasi .maana biashara hizi hazina shida, Sana sana , tatizo ni Uwekezaji na uongozi Bora ambavyo vyote tunaweza kuvipata. Kinyume cha hapo kinacho fanyika ni ufisadi
 
Kwanza unaelewa maana ya Ubia?
 
Napata shida kukosoa au kukubali huu mradi sababu sijui wamekuja na na hoja gani kutofautisha na walipo kwama serikali kwenye usafirishaji umeme.
Huenda wana jipya au hawana jipya ni miradi ya watu waliomo serikalini. i.e 10% au Wana hisa humo.
Kuweka wazi mapema habari hii kunasaidia watu wanao ijua hiyo kampuni kuweka matatizo yao bayana.
 
Kwanza unaelewa maana ya Ubia?
Kwanza unaijua historia ya ubia maana usikimbilie Tu neno ubia. Na historia ya mashirika ya umma na madhumuni yake na nini sababu ya kuwepo DSE na soko la mitaji. Na la Mwisho mahusiano ya jamii. Au ndio tunataka kurudi kwenye matabaka, walio nacho na wasio nacho, rangi na mengineyo. Nini Sera ya Nchi kuhusiana na mahusiano usifikiri yanatokea Tu kama uyoga, Bali Kwa kupitia Sera na uongozi Bora sio Bora uongozi
 
Moderator ni Kafulila au Kafulila?
Bora umewaambia maana nashangaa kwanini hawarekebishi tangia jana.na wao ndio walioandika hivyo wakati wanabadilisha kichwa cha andiko langu .maana kichwa cha awali niliandika David Kafulila Apiga Simu Kutokea Nchini India kutoa ufafanuzi wa kina juu ya uwekezaji wa Adan katika Miundombinu Ya Umeme kwa Mfumo wa Ubia.
 
Moderator ni Kafulila au Kafulila?
Bora umewaambia maana nashangaa kwanini hawarekebishi tangia jana wao ndio walioandika hivyo wakati wanabadilisha kichwa cha andiko langu .maana kichwa cha awali niliandika David Kafulila Apiga Simu Kutokea Nchini India kutoa ufafanuzi wa kina juu ya uwekezaji wa Adan katika Miundombinu Ya Umeme kwa Mfumo wa Ubia.
 
Vifaa baba vifaa, mafundi wapo.ila
Vifaaa.
Jinsi ya kuvifunga
Jinsi ya kuvipata
Mifumo ya uendeshaji ,bila kuwa na PPP hupewi teknolijia ,maana huko pakuvipata wanakwambia ,wasambazaji wao ni asani na hao gridworks ( mfano) ,

Ukisema ukafunge mwenyewe ndio hivyo ujuzi bado .
 
Kwa TZ wala hawakopi,vyote vimeandaliwa twaeni mle. Ukiona mwekezaji kachukua mkopo bank ni kutakatisha hayo mapato bila jasho. Niliwahi kuwa na mazungumzo na dingi mmoja mfanya biashara ana ukwasi wa kutisha kwa sasa. Kipindi cha PSRC alikwapua deal moja tu. Alisema hata cabinet paper aliambiwa aandike yeye.Kuhusu package ya facilitators inatisha.
 
Hawa Adani inatakiwa waje baada ya uchaguzi tukiwa tumepata rais mwenye akili na siyo mwendawazimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…