David Kafulila: Deni la Tanzania ukilinganisha na Mataifa mengine ya bara la Africa ni nafuu

David Kafulila: Deni la Tanzania ukilinganisha na Mataifa mengine ya bara la Africa ni nafuu

Huyu KIMA anatuona sisi hamnaaazo, ndio shida ya mjinga kumkalia kimya, yaani mjinga akiongea ujinga kisha mwerevu akaamua kukaa kimya basi mjinga anajiona kakuweza kweli kweli.

Huu ukimya wetu ndio unawapa bichwa hawa WAPUMBAVU
Kwanini niangalie wajinga wengine? Ili kuuidhinisha ujinga wa taifa langu!???
 
Kwanini niangalie wajinga wengine? Ili kuuidhinisha ujinga wa taifa langu!???
Sikuhizi nimeamua kuwatwanga tu.

Halafu wakitoka hapo wanalaumu wazungu.

Ukisoma asilimia kubwa ya michango ya jukwaa la siasa ni ujinga wa fikra tu. Hawa watu is beyond me.

Shida kubwa zaidi ni hii dhana ya ku evaluate situation kutokana fikra za kichwani, sasa huko shule wamesoma nini; even independently,

Ooh my god, these people thinking.

Binafsi nikishapiga chupa langu la JD sina muda wa ku-entertain feelings zao. Nawapa tu dawa yao sinaga muda wa kusingiliza ujinga nikiwa kwenye zone.

Ujinga wa mada za hili jukwaa, unaakisi; umaskini wetu (uwezo).

Many people are so shallow.

Don’t care about people’s feelings at times.
 
Viongozi mkiwa waongo mnatupa tabu huku mtaani kuitetea CCM yetu jamani
 
sija soma bandiko lote ila huu ujinga wa kulinganisha matatizo yetu na nchi zingine ni ujinga uliopitiliza serikali ipo kwa ajili ya kutu rahisishia maisha lakini cha ajabu inataka tuwe sawa na wengine huu ni upumbafu sisi bado ni masiki ili tufanikiwe ni bora kuji linganisha na nchi zilizo tuzidi na sio tulizo zizidi hatutafika popote
Fikiria mama na watoto wanamuuliza baba mbona madeni yanazidi, baba anajibu sisi tuna afadhali kuliko jirani yetu! Na huyu bwana anapozungumzia ubia na sekta binafsi, anamaanisha sekta binafsi ya nchi gani?
 
Kweli huyu bwana ni "TUMBILI" jaji Werema hakukosea kumwita "TUMBILI " deni linakuaje zuri?? Deni kubwa namna hii 97's Trion??😅😅😅🤔🤔🤔

Siku mtu akijamba USHUUZI , atasema ushuuzi huu mzuri sana😅😅

Unanukia strawberry 🍓😅😅
Ugonjwa wa malaria uliomuua ni mzuri kuliko kisukuri kilicho muua yule😄😄😄
 
Kuwa wa kwanza kwa kuwa na D ya 27.3 wakati wa pili ana D ya 27.2 si ufahali.
 
Kama deni la dunia nzima ni tirion 315 na sisi kama nchi deni ni tirion 97.
Na duniani kuna nchi 195
(97/315) x 100=? Au lengo ni iwe default justification ya Biashara ieleweke kama takwimu ni za ukweli?
 
View attachment 3288330
==
Mkurugenzi wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), David Kafulila amesema serikali inavuta mitaji kutoka sekta binafsi kwasababu kodi na mikopo hayatoshi kufikia matarajio ya wananchi.

Katika mazungumzo maalum na The Chanzo Machi 29,2025, Kafulila amesema deni la Tanzania ambalo ni Sh. trilioni 97 ni himilivu kwa uchumi wa Tanzania.

Amesema takwimu za Oktoba mwaka 2024 za IMF zilionesha kuwa deni la dunia limefika zaidi ya Dola Marekani trilioni 315 wakati uchumi wa dunia ukiwa Dola trilioni 110 ambako ni mara tatu ya uchumi wa duniani.

Adiha, amefafanua kuwa deni la dunia ndani yake kuna deni la sekta binafsi zaidi ya Dola trilioni 164, deni la kaya ambalo n idola trilioni 48 na deni la serikali trilioni 102 ambalo ni zaidi ya asilimia 90 ya uchumi.

“Kwa Afrika deni la serikali kwa uchumi ni takribani asilimia 57 kwa Tanzania ni takribani asilimia 47, deni linaongezeka ndio lakini ukifanya malinganisho kuna tofauti kubwa kati ya ukuaji wa deni letu kwa uchumi.
“Rwanda deni limefikia asilimia 71 ya uchumi, Kenya 70, Uganda 54, Malawi 84, Msumbiji 76 na Namibia 67,nchi nyingi zinakabiliwa na shida kubwa ya deni lakini sababu kubwa ni serikali kutaka kukidhi matarajio ya watu kwa kuwapa huduma za maji, umeme, afya na Barabara.”

Amesema mahitaji ya wananchi ndio msingi wa madeni kuongezeka jambo linalofanya agenda ya ubia kati ya serikali na sekta binafsi kuzidi kupata umuhimu kubwa, ili serikali ipunguze majukumu kwenye maeneo ambayo sekta binafsi inaweza kufanya.

Aidha, amesema kwa kushirikisha sekta binafsi mana yake kidogo kinachookolewa na serikali kinatekeleza miradi ambayo sekta binafsi haiwezi kuingia ubia, huku akitolea mfano wa kutoa elimu, lishe na afya kwa kaya maskini ambazo ndio nguzo ya kujenga raslimali watu.

“Raslimali watu ndio sarafu kubwa duniani, ukiwa na watu wengi maskini ukitaka wawe na ubora unahitaji kuwekeza kwenye afya, elimu na lishe yao, sasa utaitoa wapi wakati kidogo hicho ukawekeze kwenye bandari, barabara na reli.Ubia unapunguza ushindani na kuipa nafasi serikali ikawezeke huko ambako hakuna mvuto kwa sekta binafsi kuwekeza,”amefafanua.
Kwa mujibu wa Kafulila, ubia kwenye maeneo ambayo sekta binafsi inaweza kuwa na mvuto kama Barabara, reli. Fedha ambayo ingewekezwa huko inakwenda kwneye huduma za kijamii kwa kuziboresha ili wenye kipato duni kuzipata.

“Ubia unavuta mitaji kutoka sekta binafsi kuweza kuifanya serikali itekeleze miradi bila kutumia fedha yake, ili iokoe hiyo fedha ikaelekezwe maeneo ambayo hayawezi kuwa na mvuto ambayo ni msingi mkubwa kujenga mchumi wenye ushindani na watu wenye ushindani,”amesema.
Kadhalika, amesema mbia akiambia awekeze sehemu isiyo na mvuto kibiashara, hawezi kuwekeza na kwamba atawekeza baada ya kupima na ndio maana hospitali na shule za sekta binafsi zimejengwa maeneo ambayo wananchi watamudu.

“Ila ambao hawana uwezo ni sehemu ya watanzania lazima wapte huduma muhimu kwa wananchi wake, kwa kutumia mtaji wa sekta binafsi inaweza kutekeleza huduma muhimu za kijamii,”amesema.

Amesema ubia ni mkataba wa muda mrefu ambayo mamlaka za serikali zinasaini kwa ajili ya kufanya sekta binafsi itekeleze jukumu lake la kutekeleza miundombinu na huduma mbalimbali.

Lakini serikali inamuita sekta bianfsi kwa mkataba maalum na makubaliano ili atekeleze mradi huo, ambao unakuwa ni ubia kati ya serikali na sekta binafsi ambako kuna mslahi ya pande zote.

“Kwanini tunakuwa na ubia? kuna kwasababu tatu ambazo ni tunataka kuvuta mtaji wa sekta binafsi kufanya majukumu ya serikali, kuvuta teknolojia kwasababu uzoefu unaonyesha sekta binafsi imepiga hatua kuliko serikali, na tatu ni kuleta weledi kwneye menejimenti ambacho kwneye sekta binafsi kipo mbele kuliko serikalini,”amesema.

View: https://www.youtube.com/watch?v=anBdPMBDzGY

Naona na yeye anautafuta Urais wa JMT😆😆
 
(97/315) x 100=? Au lengo ni iwe default justification ya Biashara ieleweke kama takwimu ni za ukweli?
Mkuu hiyo hesabu yako hapo umechanganya parachichi na maembe kwa pamoja. Hiyo 97 ya TZ iko interms of shillings, wakati hiyo 315 ya dunia ni dollars $. Ili upate jibu sahihi badili unit ziwe sawa, either zote ziwe TZS au zote ziwe USD $.
 
sija soma bandiko lote ila huu ujinga wa kulinganisha matatizo yetu na nchi zingine ni ujinga uliopitiliza serikali ipo kwa ajili ya kutu rahisishia maisha lakini cha ajabu inataka tuwe sawa na wengine huu ni upumbafu sisi bado ni masiki ili tufanikiwe ni bora kuji linganisha na nchi zilizo tuzidi na sio tulizo zizidi hatutafika popote
Wewe ni mpumbavu kama huwezi kujilinganisha na nchi zingine. Hata kwenye maisha usipoangalia wenzio wanafanya nini huwezi kuwa bora.
 
Wewe ni mpumbavu kama huwezi kujilinganisha na nchi zingine. Hata kwenye maisha usipoangalia wenzio wanafanya nini huwezi kuwa bora.
OK mimi ni mpumbavu ila wewe ni mpumbavu zaidi kama unajilinganisha na uliowazidi ipo siku watakuzidi maana wao wanajilinganisha na wewe ulie wazidi na siku wakikufikia watataka kujilinganisha na Egypt na sio kapuku kama wewe tena umeelewa?
 
Kuna mahali wataalamu wakileta mada kama hii ya Kafulila ichukulieni ni shule tu. Kubisha hakuwaongezei maarifa yeyote. Wanapoongelea deni la Taifa kuna (1) Deni la ndani na (2) Deni la nje.

Mpaka sasa watu wanaangalia deni la nje tu lililojenga SGR, Mwendokasi, fedha za Covid zilizojenga mashule na hospitali, daraja la Busisi etc.

Ila kuna kitu ambacho mnasahau ambacho ni deni la ndani. Deni la ndani ni pale ambapo taasisi binafsi na za umma za ndani ya nchi zinapoidai Serikali.

Nyie mumekalia kubeza tu wakati vitu hamvijui.

Chanzo cha deni huanzia kwenye makadirio ya Bajeti wakati Waziri wa Fedha anawasilisha makisio. Kwa mfano mwaka 2024/25 Waziri Mwigulu aliwasilisha bajeti ya Tsh 49.34 Trilioni. Lakini wastani wa makusanyo kwa mwezi kwa mwaka 2023/24 ni Tsh 3.0 Trilioni ambayo ni sawa na Tsh 36 Trillion kwa mwaka. Hivyo kusababisha nakisi (deni) ya Tsh 13 Trillioni.

Hiyo nakisi ya Tsh 13 Trillion ndiyo mkopo wenyewe.

Sasa mnaleta kejeli wakati shughuli zinaonekana kama hospitali za wilaya zilizojengwa na zinazoendela kujengwa, mashule, miundombinu ya barabara, Treni ya SGR, Bwawa la umeme.

Hivi Watanzania mnataka nini?
 
Hayo madeni ya ndani ni Tanzania tu ndio inayo? unataka kusema nchi nyingine za africa zilizoendelea kutuzidi hazina deni la ndani? mbona tunaendekeza usomi usiokuwa solution! inajulikana kuna deni la nje na la ndani hii ni karibia kwa kila nchi dunia nzima mpaka kwa Europe mbona sisi kwetu ndio imekuwa kisingizio kikuu? acha ujinga binti
 
Stupid!
Badala ya kupigania kushusha deni la taifa anasema deni ni zuri,
Tumbili ni tumbili tu anafikiria kuvuna bila kulima
Lishuke liende wapi wakati Uchumi na unajua, Umesomea wapi wewe
 
Back
Top Bottom