David Kafulila: Deni la Tanzania ukilinganisha na Mataifa mengine ya bara la Africa ni nafuu

Mwigulu amekopa ila utetezi kaachiwa Kafulila,😂😂
 
Usipojilinganisha utajuae unafaulu au unafeli?
 
Huyu Dalali Hopeless kabisa..., Hawa majirani nao wana maziwa yote makuu, plus Bahari, Mbuga za Wanyama ikiwemo Serengeti, Linchi likubwa na population ya kutosha, Madini mengine yapo Tanzania pekee n.k. (ALL IN ONE) ? Yaani a Cradle of Humanity ?!!!!

Au tuanze kupigana na kuuwana alafu tujilinganishe na Congo kwamba hatujawafikia ? Ni kama unakimbia na vipofu alafu unajinasibu sio kwa kuwashinda, bali kulingana nao au kuwa nao sambamba....


 
Huna hoja
 
Umewahi ona dalili ya 🇹🇿 Kushindwa kulipa deni?

Nchi Ina credit rating kubwa kabisa hapa Africa harafu unaleta ngonjera za hisia?

Kafulira anajua kuwanyoosha Kwa hoja.

GDP ya 🇹🇿 mwaka huu wa 2025 ni USD 90bln kutoka USD 67,miaka 5 iliyopita.
 
Huna hoja
Hii ndio definition ya Vioja na ndio maana humu kumejaa content without context..., Utasikia fulani ana akili sana fulani amefanya sana hili au lile na sio kuongelea kile ambacho amekifanya au kama kimefanyika ipasavyo au kama kingeweza kuwa done better..., Case in Point....

 
Usipojilinganisha utajuae unafaulu au unafeli?
ChoiceVariable wewe unau elewa fikiria ikiwa wewe una jilani yako ni ambae ni masikini zaidi yako sasa ukiendelea kujilinganishanae ikitokea kawa tajiri kukupita utafanya nini? utatafuta masikini mwingine au ndio basi utakubali kuwa wa mwisho ikiwa hakuna masikini mwingine zaidi yako? mimi naona ilitakiwa tuseme angalau nchi flani imetuzi kiasi flani ila gape linapungua tunawakaribia na sio kujilinganisha na nchi fukala zaidi. nchi inaganda kimaendeleo kwasababu inajilinganisha na nchi zisizoendelea miaka na miaka
 
Wapi tumejilinganisha na maskini? Kenya ni maskini?
 
Wapi tumejilinganisha na maskini? Kenya ni maskini?
Naimani wewe sio mgeni kwenye hii nchi sina haja ya kukuelezea sana leo imetajwa kenya zambia, zimbabwe, congo, malawi nk zilisha tajwa pia na zitaendelea kutajwa
 
Nchu zingine pia zina madeni ya ndani. Ndiyo maana nimesema msome vizuri mtoa mada na umuelewe. Wazungu wanasema "read to understand".

Amekuwekea benchmark na nchi rates za mikopo ya dunia, Afrika na kisha dhidi ya nchi za East Africa. Anasema debt/equity ratio ya Tanzania ni 0.47 ina maana kuwa deni letu halifiki nusu ya raslimali tunayoimiliki. Yaani tunaweza kulipa deni na kubaki na akiba.

Kenya wana debt/equity ratio ya 0.70, ina maana 70% ya raslimali yake ikilipa deni watabakia na 30% ya raslimali.

Hakuna dhambi katika kukopa bali kinachopimwa ni uwezo wa kulipa deni. Hadi leo Tanzania haiko katika nchi 10 za Afrika zenye madeni makubwa.

Usipotaka kukopa inabidi ufanye miradi mikubwa ya maendeleo kwa fedha zako. Je Tanzania inaweza kufanya kwa fesha zake? Isije ikawa na wewe ni mhanga wa uwongo wa Magufuli aliyesema tunajenga kwa fedha zetu
 
Ngoja nikupuuze naona nabishana na chawa mtiifu
 
Inakuwaje ukope trilioni 30 ndani ya muda mfupi na bado wananchi wako wengi wanalalamika maisha ni magumu na hamshtuki na mnajificha kwenye kichaka Cha deni kuwa himilivu!

Angalia hapo chini 👇 kuhusu Ujerumani - taifa lenye uchumi mkubwa barani ulaya wanavyopunguza deni lao
 

Attachments

  • Screenshot_20250331-112941.jpg
    97.9 KB · Views: 22
China taifa la pili kwa uchumi mkubwa duniani ingawa deni lao linapanda lakini matokeo yanaonekana bila nguvu kubwa ya machawa
 

Attachments

  • Screenshot_20250331-113258.jpg
    84.1 KB · Views: 16
Dalali Kwenye 1&2.
Kafulila wa IPTL VS Wa Sasa??
 
Inakuwaje ukope trilioni 30 ndani ya muda mfupi na bado wananchi wako wengi wanalalamika maisha ni magumu na hamshtuki na mnajificha kwenye kichaka Cha deni kuwa himilivu!
Ni lini ndugu maisha yamewahi kuwa mepesi Tanzania? Usipojishughulisha hizi fursa zitakupita tu, utabakia kupika MAJUNGU tu hapa.

Hakuna Rais atakayekuwekea hela mfukoni, bali ni wewe mwenyewe kujishirikisha kwenye shughuli za uchumi
 
Ukiona kiongozi Kila mfano analinganisha na nchi zingine

Hana fikra za kujitegemea atauza nchi
Kila nchi Ina Mfumo wake wa uchumi kulingana na resources zake
 
Bado unabisha wewe sio chawa na mjinga? una element za kichawa
 
Bado unabisha wewe sio chawa na mjinga? una element za kichawa
Tatizo wewe huji na point bali unajuwa kusema neno "chawa" tu. Hata mimi naweza kutoa statement kama hiyo. Ubishi mzuri ni kuleta takwimu na hoja. Kama uliishia la saba B, basi sina namna ya kukusaidia
 

View: https://m.youtube.com/watch?v=iEpJwprxDdk
Bloomberg live

Kwanza kuelewa wanachoongea hapo lazima uwe na abc za accounts, MBA, banking economics, stock markets, investment na general finance decisions; vinginevyo unatoka kapa kwenye hiyo TV.

Ni ngumu kwetu kuelewa nafasi ya Kafulila, wakati hana techno skills ya sehemu yeyote on paragraph yeyote huko.

It’s not easy

Ni rahisi kwa sababu kuna wajinga wanadhani ni raisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…