Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Kuelekea Ujenzi wa barabara za kulipia Tanzania (toll road) David Kafulila, Mkurungezi Mtendaji PPP amewatoa hofu Watanzania kuwa sio lazima mtu apite kwenye barabara ya kulipia kwani kila barabara ya kulipia itakuwa na barabara mbadala isiyo ya kulipia hii inampa mtumiaji uhuru wa kuchagua kulingana na mahitaji yake.
“Barabara za kulipia ni za express. Ukihitaji kufika haraka, utalipa ili kutumia barabara hiyo. Lakini, kama huna haraka, unaweza kutumia barabara ya bure. Hakuna anayelazimishwa kutumia barabara za kulipia, kwani kutakuwa na njia mbadala za bure,” alieleza Kafulila.
Mtakumbuka katika hotuba yake ya kufunga mwaka wa 2024 na kuukaribisha mwaka 2025 Rais Dkt Samia Suluhu Hassan aliahidi mwaka 2025 zitajengwa barabara za kulipia kutoka Bagamoyo Chalinze -Morogoro mpaka Dodoma kwa mfumo wa Ubia kati ya Serikali na sekta binafsi PPP.
Soma: David Kafulila: Barabara za kulipia zitapunguza foleni Dar Es Salaam