David Kafulila kuteuliwa kuwa DC baada ya kujiuzulu U-RAS ni uthibitisho kwamba nchi hii kuna watu hawatakiwi kuwa Jobless?

David Kafulila kuteuliwa kuwa DC baada ya kujiuzulu U-RAS ni uthibitisho kwamba nchi hii kuna watu hawatakiwi kuwa Jobless?

Hii imekaaje ?

Mtu anachaguliwa nafasi fulani, anafanya baada ya muda anajiuzulu kwenda kutafuta nafasi anayoitaka mwenyewe.

Cha kushangaza mtu huyo huyo teuzi nyingine zikifanyika unamuona kateuliwa tena 🙄

Je, hakuna watu wengine au what's so special na hawa watu ?

Nadhani wakati wa kura za maoni ndani ya CCM mwaka 2024 tutegemee tena style hii hii.

Je, kwanini iko hivi ?

Katiba mpya ilikuwa ufumbuzi sahihi yakiwamo haya ya utitiri wa viongozi wa serikali wasiokuwa na tija wala ridhaa za wananchi.

Tujipange kudai katiba mpya badala ya kuendelea kulalama. Tunaowalalamikia hawasikii wala hawajali.
 
Hii hali ya watu kuwa Recycled ndani ya CCM inanifikirisha sana! Kuna muda nawaza nguvu za kiganga hutumika kuwapumbaza wanaoteua!
Kuna yule mwana alikuwa anachezea mbususu ya gigi nani sijui naye kapewa utumishi wa umma, hizi nchi zetu kwanini usimuache afanye biashara zake
 
Katiba mpya ilikuwa ufumbuzi sahihi yakiwamo haya ya utitiri wa viongozi wa serikali wasiokuwa na tija wala ridhaa za wananchi.

Tujipange kudai katiba mpya badala ya kuendelea kulalama. Tunaowalalamikia hawasikii wala hawajali.
naitaka sana katiba mpya mkuu sana kuliko chochote, lakini tunatatua vipi matatizo ya ukiukwaji wa katiba na uvunjwaji wa sharia uliyopo sasa na wahusika kutowajibishwa

mfano wabunge wale 19 na mengine mengi
 
Hao mnaotaka wawape katiba mpya hawawezi kuwapa sababu kama ingalikuwa rahisi toka kelele za katiba zilipoanzaga mngalikuwa mshapewa!
 
Imagine, yaani mtu anateuliwa baada ya muda anajiuzulu mwenyewe.

Lakini teuzi nyingine zikitokea tena unamwona yumo🤣
Mbona mtu fulani hajateuliwa mpaka leo? Na mlikuwa mansema huyu ndio mlezi wake?
 
naitaka sana katiba mpya mkuu sana kuliko chochote, lakini tunatatua vipi matatizo ya ukiukwaji wa katiba na uvunjwaji wa sharia uliyopo sasa na wahusika kutowajibishwa

mfano wabunge wale 19 na mengine mengi

Mkuu ni jambo la kheri sana kuitaka katiba mpya.

Wale 19 ni wabunge wasio na chama kinyume cha katiba. Bunge, Mahakama na serikali mihimili yote imeshindwa kuwajibika kwa mujibu wa katiba iliyopo.

Hapa ndipo tunapopaswa kukaa zaidi, kudai katiba mpya sasa yenye meno ya kutosha kuwawajibisha watu bila kujali vyeo vyao kwenye kadhia kama hizi. Hawa 19 ukiwa ni mfano tu.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Hao mnaotaka wawape katiba mpya hawawezi kuwapa sababu kama ingalikuwa rahisi toka kelele za katiba zilipoanzaga mngalikuwa mshapewa!

Ni makosa kudhani kuwa katiba mpya ni ya kuombwa. Kama ni kwa kuomba ni kheri tukaachana na msamiati huu "katiba:"

IMG_20210621_152032_417.jpg

Kelele zilizo kwisha pigwa hazipaswi kuwa zile zile. Kelele mpya ziendanazo na vitendo ni muda wake huu na inawezekana.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Ile nayo ni rubber stamping tu. Rais Museveni anachagua mke wake na wanapitisha tu, how comes first lady ageuke kuwa Waziri at the same time.

Ni sawa na mama Jumong amteue yule mumewe kuwa waziri 😃
samahani. Yule jamaa wa Twitter anatumia hili jina Jumong. Chimbuko lake hili neno ni lipi? I mean jamaa jina kalitoa wapi?
 
Uganda tunawazidi kwenye kubadilisha Rais tu. Wana demokrasia kuliko sisi.

Wanaruhusu mgombea binafsi na wanahoji matokeo ya urais mahakamani.

Hapa kwetu hivyo vitu vimeshindikana.
Hapa kwetu hakuna movement ya dhati ya kudai vitu hivyo muhimu.

“Wanaharakati” wetu wao ni bora zaidi kwao kuanzisha petitions za kupambana na Diamond mitandaoni. Shida kwelikweli
 
Katiba yetu ina makosa sana hasa hivi vyeo vya "ahsante /hisani"

Imagine mtu kama Hery James nae anakua DC mara Niki Wa Pili sujui Minaj
 
Kafulila anao uwezo wa kuelewa dunia inakwenda vipi. Ni mtu wa kuifaa Tanzania siku za baadae. Ana substance siku zote huwa haongei pumba.
 
Bongo ukipata mchongo wako deal nao utoke kimaisha.
Kuna vitu ukifuatilia sana utapasuka kichwa.
 
Hii imekaaje ?

Mtu anachaguliwa nafasi fulani, anafanya baada ya muda anajiuzulu kwenda kutafuta nafasi anayoitaka mwenyewe..,
Uwe na uhakika kwanza na taarifa inayomhusu mtu ambaye ni "real" kabla ya kuiposti.

Mpaka sasà Mimi nashangaa kwanini hujaufuta huu uzi kwa sababu umebeba taarifa zisizo sahihi.
 
Back
Top Bottom