Hii imekaaje ?
Mtu anachaguliwa nafasi fulani, anafanya baada ya muda anajiuzulu kwenda kutafuta nafasi anayoitaka mwenyewe.
Cha kushangaza mtu huyo huyo teuzi nyingine zikifanyika unamuona kateuliwa tena 🙄
Je, hakuna watu wengine au what's so special na hawa watu ?
Nadhani wakati wa kura za maoni ndani ya CCM mwaka 2024 tutegemee tena style hii hii.
Je, kwanini iko hivi ?
Katiba mpya ilikuwa ufumbuzi sahihi yakiwamo haya ya utitiri wa viongozi wa serikali wasiokuwa na tija wala ridhaa za wananchi.
Tujipange kudai katiba mpya badala ya kuendelea kulalama. Tunaowalalamikia hawasikii wala hawajali.