David Kafulila: Mahitaji ya binadamu ni makubwa kuliko uwezo wa Serikali kuyafikia kwa kutegemea kodi na mikopo pekee

Itungwe sheria ya kuzuia ongezeko la watanzania. Hiyo ndio muarobaini wa kukuza uchumi na kuondoa masikini.

Kuendelea kuziba masikio na kuendelea kufanya mipango yenu hiyo ya kuongeza kipato ni kiini macho kwa raia maana wafaidika kwa mtindo huo ni Kafulila na familia yake ndugu marafiki na taasisi inayompa ulaji.
 
Vipi kama hiyo Sheria ingetungwa kabla wewe hujazaliwa sijui kama unge comment leo
 
Vipi kama hiyo Sheria ingetungwa kabla wewe hujazaliwa sijui kama unge comment leo
Dude unajua kasi ya kuzaana tuliyonayo ukilinganisha na uwezo wa uchumi wetu kuhudumia watu wake?
 
Population haijawahi kuwa tatizo china wako karibu 2bn
Kwa hiyo unataka kutumia strategy ya China hapa Tanzania una uwezo huo? na unajua kuwa kuna wakati ilibidi wazuie kuzaana kwa muda ili waweze kujenga uchumi wao? unajua kuwa kulikuwa na amri ya kuzaa watoto wawili tu hadi ilipositishwa miaka ya karibuni? unajua kwa nini?
 
Huduma kama umeme na maji ni vema zikaangaliwa namna ya kuzibinafisisha, siyo kwa 100% lakini angalau kwa asilimia fulani. Mfano serikali inaweza kuwa mzalishaji wa umeme kupitia Tanesco na kuusafirisha kupitia line kubwa hadi vituo vya kupozea. Kutoka hapo sasa, usambazaji kwa wananchi ikapewa sekta binafsi. Nadhani hakuna mtu angekaa kwenye foleni muda mrefu kusubiri kuungiwa umeme na Tanesco, badala yake makampuni binafsi yangeshindana kupata wateja kwa wingi wa kuwaungia umeme kwa haraka na huenda hata gharama za uunganishaji zingeshuka sana. Hivyo hivyo na huduma ya maji, usambazaji ungefanywa na sekta binafsi serikali ikawa mzalishaji tu na kukusanya kodi za mapato kutoka kwa makampuni husika...nawaza tu.
 
Yes umeleta hoja ya Msingi, Tunaweza kuwa na Ubia kwa sehemu tu
 
Dunia ya Watu wastaarabu inaendeshwa na sekta binafsi Serikali inabaki kuwa regulator tu
 
  1. Kwanini mnanunua mashangingi ya anasa kila kukicha?
  2. Kwanini makao makuu ya serikali yako Dodoma lakini 90%+ ya viongozi wanakuwa Dar kwa perdiems?
  3. Kwanini ufujaji wa fedha za serikali hauchukuliwi hatua?
  4. Kwanini tuna bunge kubwa kuliko mahitaji?
 
Ni kwa sababu wanajiita waheshimiwa na wananchi tumebariki hilo. Hawaoni sababu ya wao kutokuishi kiuheshimiwa
 
Hadi aibu kwa rasilimali tulizinazo kusikia kiongozi anasema maneno kama hayo kauli rahisi ni kwamba mmeshindwa kuwaletea watu maendeleo mmeshindwa kuongoza
 
  1. Kwanini mnanunua mashangingi ya anasa kila kukicha?
  2. Kwanini makao makuu ya serikali yako Dodoma lakini 90%+ ya viongozi wanakuwa Dar kwa perdiems?
  3. Kwanini ufujaji wa fedha za serikali hauchukuliwi hatua?
  4. Kwanini tuna bunge kubwa kuliko mahitaji?
Sasa hapa PPP inahusikaje?
 
Hadi aibu kwa rasilimali tulizinazo kusikia kiongozi anasema maneno kama hayo kauli rahisi ni kwamba mmeshindwa kuwaletea watu maendeleo mmeshindwa kuongoza
Acha siasa,

Kwanza unafahamu maana ya PPP,

Unafahamu PPP haitegemei Kodi Wala Mikopo?

Unafahamu PPP ndio inaweza kuleta maendeleo kwa Kasi kuliko kuliko Kodi?

Unafahamu PPP ni njia Bora na salama kwa ukuaji wa Uchumi wa nchi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…