David Kafulila: Mahitaji ya binadamu ni makubwa kuliko uwezo wa Serikali kuyafikia kwa kutegemea kodi na mikopo pekee

#Tuko na Mama
IMG-20250217-WA0123.jpg
 
Itungwe sheria ya kuzuia ongezeko la watanzania. Hiyo ndio muarobaini wa kukuza uchumi na kuondoa masikini.

Kuendelea kuziba masikio na kuendelea kufanya mipango yenu hiyo ya kuongeza kipato ni kiini macho kwa raia maana wafaidika kwa mtindo huo ni Kafulila na familia yake ndugu marafiki na taasisi inayompa ulaji.
Yaani tuko 60m halafu tusiongezeke?
China wako 2bn
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia nchini Tanzania PPPC Bw David Kafulila amenukuliwa akisema " Sasa mahitaji ya binadamu duniani ni makubwa kuliko uwezo wa Serikali za dunia kuyafikia na kuyatatua kwa wakati kwa kutegemea Mikopo na Kodi kama chanzo pekee Cha mapato Cha Serikali hivyo ni lazima Serikali zetu kutafuta njia Mbadala za kuyafikia kwa wakati mahitaji hayo ya binadamu"

Akizungumza kwenye Kipindi Cha DK 45 kinachorushwa na kituo cha utangazaji Cha ITV Kafulila amesema msisitizo wa kutumia Sekta binafsi Kama njia ya kuipa unafuu Serikali yoyote duniani katika kuwahudumia Wananchi wake umetolewa kwenye majukwaa mbalimbali ya Kiuchumi Duniani likiwemo la Energy Summit iliyofanyika Jiji Dar es salaam.

zaidi sana msikilize kwa undani hapa

View attachment 3226930
Kama tumbili hajui akae kimya
 
Yaani tuko 60m halafu tusiongezeke?
China wako 2bn
China imeweza kugeuza population growth kuwa nguvukazi watu wakati sisi tuna population ya watu walio wengi tegemezi wasiozalisha mali.
Hiyo ndio tofauti ya 2bn ya China na 60mn ya Tanzania.
 
Kwanini sisi nasi tunashindwa?
 
Kwanini sisi nasi tunashindwa?
Tunashindwa kwa sababu tuna tafsiri tofauti na mtazamo wa maisha. Tunaamini kwamba tupo Duniani ili tuongezeke,tuzaane na kuijaza Dunia bila kuzingatia ukuaji wa vipato vyetu ambavyo ni duni kwa kuwa hatujishughulishi sana kubuni vingine wala kuongeza vingine.
Mopokeo ya dini pia yanaathiri sana mipango yetu ya maisha na hapa Serikali isiyokuwa na mipango thabiti ya kustawisha watu wake ni mojawapo kati ya vikwazo vinavyoturudisha nyuma.
 
Tufanye nini basi??
 
Tufanye nini basi??
Tunatakiwa kuwa na elimu ya ustawi wa jamii na kuwa na uelewa wa pamoja juu ya kanuni za utajirisho ambazo zinamtaka mtu kuhakikisha kuwa kipato cha mtu au vyanzo vya mapato ya mtu ndio viamue idadi ya walaji au wanufaika.
Wingi wa walaji uende sambamba na uwezo wa kujikimu na hasa uzalishaji. Hakuna sababu ya kuwa na watu wengi kwenye jamii wasiozalisha.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia nchini Tanzania PPPC Bw David Kafulila amenukuliwa akisema " Sasa mahitaji ya binadamu duniani ni makubwa kuliko uwezo wa Serikali za dunia kuyafikia na kuyatatua kwa wakati kwa kutegemea Mikopo na Kodi kama chanzo pekee Cha mapato Cha Serikali hivyo ni lazima Serikali zetu kutafuta njia Mbadala za kuyafikia kwa wakati mahitaji hayo ya binadamu"

Akizungumza kwenye Kipindi Cha DK 45 kinachorushwa na kituo cha utangazaji Cha ITV Kafulila amesema msisitizo wa kutumia Sekta binafsi Kama njia ya kuipa unafuu Serikali yoyote duniani katika kuwahudumia Wananchi wake umetolewa kwenye majukwaa mbalimbali ya Kiuchumi Duniani likiwemo la Energy Summit iliyofanyika Jiji Dar es salaam.

zaidi sana msikilize kwa undani hapa

View attachment 3226930
Kafulila akili zipo
 
Back
Top Bottom