David Kafulila: Matumizi mabaya ya fedha za umma yamepungua kipindi cha Rais Samia

David Kafulila: Matumizi mabaya ya fedha za umma yamepungua kipindi cha Rais Samia

Mkurugenzi wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), David Kafulila kwenye mahojiano na Wasafi TV amedai kuwa matumizi mabaya ya fedha za umma yamepungua kipindi cha Rais Samia, ukilinganisha na ripoti za CAG za miaka ya nyuma .

Soma, Pia: David Kafulila: Wakati wa Rais Samia hati safi zimefikia 99% kutoka 89%

Kweli njaa mbaya sana aisee. Huyu jamaa alivyokuwa anaichachafya CCM hasa kwenye ule ufisadi wa IPTL na Tegeta EScrow siamini kama ni yeye leo ndio kageuka chawa pro max mpaka wale wezi kule CCM wanamshangaa. Ukiwa mpiga kelele kuhusu ufisadi wa CCM kwenye fedha za umma wanakuita na kukukaribisha ili mle pamoja na wakati unakula nao huruhusiwi kuongea ongea tena
 
Hivi kweli kwa nini Werema aliwahi kumlinganisha huyu jamaa na tumbili vile? 🤔
 
Sa100 mwenyewe anamshangaa, ina maana amesahau kauli mbiu ya mama kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake?!.
 
Mbwa anayebweka mpe mfupa tu hutaona akiendelea kubweka.


Angalia clip za Kafulila kwenye Bunge la 2011 hadi 2015 kisha angalia mahojiano yake ya miaka hii baada ya kuwekwa sehemu yenye Ulaji

Ni Maji na mafuta🙌
 
Huku ni kukosa mwelekeo. Kafulila toa takwimu na ulinganisho wa u achosema
 
Yamepungua au ni udhibiti wa taarifa na kudhibiti vyombo vya habari?
I can assure you kuwa upigaji hasa fedha za miradi ni mkubwa sana tu!
Tena ni "senior Officers"
 
Pongezi sana kwa kweli.

Lakini, alaaniwe aliyesababisha tukakosa watu wenye weledi kuendesha vipindi vya asubuhi vya habari.
 

Attachments

  • VID-20250403-WA0029.mp4
    12.8 MB
  • VID-20250403-WA0027.mp4
    1.1 MB
  • VID-20250403-WA0023.mp4
    2.9 MB
Kigoma ndio inaongoza kwa kuwa na Chawa wasomi,ni hatari mno.
 
Back
Top Bottom