By the way nimechanganya madesa hiyo GDP niliyotaja ilikuwa ya robo moja ya mwaka kwa mwaka 2024 kwa dubai.Are you talking about UAE economy au Dubai ?
Dubai ni Nchi ndogo sana Kwa size hiyo ya Uchumi kwao ni maendeleo makubwa sana na waliya plan hivyo wakati Kwa Tanzania ni sawa na tone la maji tuu.
Tatu Kwa Rasilimali zilizopo na Mahitaji ya Nchi na watu wake ,tunahitani Uchumi mkubwa zaidi ambayo ndio huo uliokadiriwa kwenye Dira,sio rahisi ila ni achievable ndani ya mda huo huo.Mifano ya Nchi zilizokuza uchumi Kwa Ukubwa huo Kwa mda mfupi ni Korea Kusini,China,Indonesia,Singapore,Malaysia nk na ndiko Tanznaia imeenda Kujifunza.
Lakini hebu turudi kwenye ukweli mkuu.
Yani turuke tu kutoka gdp ya btilioni 200 kwa mwaka hadi tilioni 1750 ndani ya miaka ishirini. Yani idouble mara 8 ndani ya miaka 25.
Nahisi hata kasi ya ukuaji wa uchumi wetu kwa mwaka haikubaliani na hili.
Hizo nchi ulizotaja mkuu uwekezaji wao ni tofauti kabisa na kwetu. These people were serious, watu wao waliwapeleka wakasoma wakaja kusimamia uchumi wao.
Hebu nipe sababu kwanini mpaka leo mradi mdogo tu wa mwendokasi umeshindwa kuwa efficient. Train ya umeme nayo mara isimame njiani karibu kila mwezi. Njoo umeme unakatika katika mimi hapa nilipo leo umeshakatika na kuwaka mara mbili, kimara nimeona thread humu kuwa hii week wanakata kwa saa 12 bila hata taarifa.
TTCL kampuni zote za simu zimeikuta ila mpaka leo nadhani ndiyo mtandao ambao si famous kuliko mtandao wowote.
Mifano ni mingi. Siwezi kukataa kuwa tutabadilika, ila sasa kwa miaka 20 kuweza kufika uchumi huo sio realistic bado tuna makando na shida nyingi na siasa nyingi kwenye nchi hii.