Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Kwa Wafuatiliaji wa siasa za Nchi hii mtakubaliani nami kuwa Mheshimiwa David Kafulila pamoja na Mheshimiwa Zitto Kabwe ndio watu Pekee waliokuwa wanaubeba Upinzani hasa CHADEMA katika masuala na hoja zote zinazogusu na kuhusu Uchumi.Ndio maana CHADEMA mpaka sasa huwezi ukaona au kumuona mtu yeyote akizungumza masuala ya uchumi au sera za uchumi au mbadala wa sera fulani.
Ndio maana ilifika wakati CHADEMA ikawa inashindwa hata kuandaa tu bajeti mbadala Bungeni,na ikiandaa ilikuwa ni bajeti yenye vichekesho vingi sana.kwanini? Kwasababu ilikosa watu wenye uelewa , weledi na wasomi wa masuala ya uchumi.Ndio maana ikabidi wampe Mheshimiwa Halima Mdee kama waziri kimvuli wa Fedha ,Kiongozi ambaye alikuwa hana uelewa mpana wa masuala ya kiuchumi kwa kuwa yeye alikuwa amesomea masuala ya sheria.kwa hiyo mambo mengi ya kiuchumi kwake yalikuwa mageni na magumu kuyatengenezea sera na hoja na kuelezea kwa ufasaha na akaeleweka vyema kwa watu.
Ikumbukwe kuwa Uchumi ni kanuni na wala uchumi hauhitaji siasa siasa au blaa blaa au maneno maneno.ukiukosea uchumi katika kanuni zake ni lazima Ukuadhibu na kukuumbua. kwa sababu kuna mambo unaweza kuficha na kudanganya ,lakini huwezi kudanganya na kuficha matokeo ya sera zako za uchumi ,kwa sababu matokeo yake ya sera zako yataonekana katika maisha halisi ya watu. Ndio maana ya kusema uchumi una kanuni zake ambazo ukikosea tu ni lazima kilio kisikike kutoka katika vinywa na midomo ya watu hata kama hawajasomea Uchumi.
Hivyo basi kuondoka kwa watu aina ya Mheshimiwa David Kafulila na Zitto Kabwe, ndio maana Upinzani hasa CHADEMA umepwaya sana na umeshindwa kuwa na sera mbadala wala hoja zenye kumgusa mwananchi wala kuwa na uwezo hata tu wakumshawishi mwananchi wa kule kijini akawaelewa.ndio sababu unakuta CHADEMA inakuwa inakimbilia sana na kuendesha siasa zake kwa kufuata matukio na kuokoteza vihabari visivyo na mashiko .ndio maana unaweza ukakuta viongozi wa CHADEMA eti wapo Bize na hoja ya kujadili kwanini kiongozi fulani haonekani hadharani.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.