David Kafulila na Zitto Kabwe ndio watu Pekee waliokuwa wanaibeba CHADEMA katika Hoja zote za Masuala ya Uchumi.

David Kafulila na Zitto Kabwe ndio watu Pekee waliokuwa wanaibeba CHADEMA katika Hoja zote za Masuala ya Uchumi.

Uwezo wa mtu hatupimi Kwa kujua kuongea na kutusomea data ambazo tayari zipo au kuelezea yale ambayo Kila mwenye taalum yake anaweza kuyaelezea/kuyahadithia.

Uwezo wa mtu tunaupima kupitia michango mipya yenye kuleta matokeo chanya mahala, mipango, mikakati, uthubutu na utekelezaji unaoleta matokeo ndio vinaonyesha uwezo wa mtu na si blah blah.

Leo hii ukimuita engineer akuelezee aliyosamoea na kuyafanyia kazi basi utamuona ana akili sana, ukimuita mganga wa kienyezi akuelezee matunguli yake na uganga wake utamuona genius sana, ukimuita Mwanasheria akuelezee Sheria yake kama TL utamuona genius kwelikweli.

Ugenius ni kuyatumia yale uliyosomea kuleta matokeo chanya na pia kuongeza ufanisi kwa kuleta ubunifu wako ambao wengine hawawezi.
Hicho ndicho anachokifanya Mheshimiwa Kafulila kutumia yale aliyosoma darasani kuleta matokeo chanya kwa jamii na katika nafasi anazokuwa amepewa na kuaminiwa .amefanya hivyo akiwa mbunge,Ras Songwe, RC Simiyu na Sasa mkurugenzi wa PPP
 
Ukweli ni kuwa ni Chadema ndiyo ilimjenga Zitto hadi CCM wakamtamani ndiyo wakaipa TISS kazi ya kum recruit ili aifanyie kazi CCM ndani ya Chadema.
 
Anajipigia sana promo na kwa serikali hii atapewa tu. Alafu inakuwaje Katibu Mkuu wa Chama anasema wabadhirifu na majizi yaombewe wakati kuna Mahakama na Magereza. Nchi imekuwa ya hovyo sana awamu hii
Tangu kuanzishwa CCM Nchimbi ndiye Katibu Mkuu wa ovyo kuliko wote.
 
Kama walikuwa na HOJA wasingeachwa na wake zao, halima bulembo kamuacha zitto, Jessica kishoa(COVID 19) kamuacha mume kafulila
 
Wewe ndiye wa hovyo.tena uwe na adabu kwa viongozi wetu.
MAISHA ni kama gwaride Kaka, mtu yeyote ana kibali mbele za Mungu anaweza akawa Kiongozi lakini sio Viongozi wa sasa hivi. Hawana sifa za uongozi ila wanachofanya ni kurithishana tu na nyinyi Machawa ndio mnaotoka mpaka jasho kuwatetea. Shame on you
 
MAISHA ni kama gwaride Kaka, mtu yeyote ana kibali mbele za Mungu anaweza akawa Kiongozi lakini sio Viongozi wa sasa hivi. Hawana sifa za uongozi ila wanachofanya ni kurithishana tu na nyinyi Machawa ndio mnaotoka mpaka jasho kuwatetea. Shame on you
Hatuwatetei bali tunazungumza ukweli juu ya uchapa kazi wao.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa Wafuatiliaji wa siasa za Nchi hii mtakubaliani nami kuwa Mheshimiwa David Kafulila pamoja na Mheshimiwa Zitto Kabwe ndio watu Pekee waliokuwa wanaubeba Upinzani hasa CHADEMA katika masuala na hoja zote zinazogusu na kuhusu Uchumi.Ndio maana CHADEMA mpaka sasa huwezi ukaona au kumuona mtu yeyote akizungumza masuala ya uchumi au sera za uchumi au mbadala wa sera fulani.

Ndio maana ilifika wakati CHADEMA ikawa inashindwa hata kuandaa tu bajeti mbadala Bungeni,na ikiandaa ilikuwa ni bajeti yenye vichekesho vingi sana.kwanini? Kwasababu ilikosa watu wenye uelewa , weledi na wasomi wa masuala ya uchumi.Ndio maana ikabidi wampe Mheshimiwa Halima Mdee kama waziri kimvuli wa Fedha ,Kiongozi ambaye alikuwa hana uelewa mpana wa masuala ya kiuchumi kwa kuwa yeye alikuwa amesomea masuala ya sheria.kwa hiyo mambo mengi ya kiuchumi kwake yalikuwa mageni na magumu kuyatengenezea sera na hoja na kuelezea kwa ufasaha na akaeleweka vyema kwa watu.

Ikumbukwe kuwa Uchumi ni kanuni na wala uchumi hauhitaji siasa siasa au blaa blaa au maneno maneno.ukiukosea uchumi katika kanuni zake ni lazima Ukuadhibu na kukuumbua. kwa sababu kuna mambo unaweza kuficha na kudanganya ,lakini huwezi kudanganya na kuficha matokeo ya sera zako za uchumi ,kwa sababu matokeo yake ya sera zako yataonekana katika maisha halisi ya watu. Ndio maana ya kusema uchumi una kanuni zake ambazo ukikosea tu ni lazima kilio kisikike kutoka katika vinywa na midomo ya watu hata kama hawajasomea Uchumi.

Hivyo basi kuondoka kwa watu aina ya Mheshimiwa David Kafulila na Zitto Kabwe, ndio maana Upinzani hasa CHADEMA umepwaya sana na umeshindwa kuwa na sera mbadala wala hoja zenye kumgusa mwananchi wala kuwa na uwezo hata tu wakumshawishi mwananchi wa kule kijini akawaelewa.ndio sababu unakuta CHADEMA inakuwa inakimbilia sana na kuendesha siasa zake kwa kufuata matukio na kuokoteza vihabari visivyo na mashiko .ndio maana unaweza ukakuta viongozi wa CHADEMA eti wapo Bize na hoja ya kujadili kwanini kiongozi fulani haonekani hadharani.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
David Kafulila hajawahi kuwa mbunge wa CDM
 
Back
Top Bottom