David Kafulila na Zitto Kabwe ndio watu Pekee waliokuwa wanaibeba CHADEMA katika Hoja zote za Masuala ya Uchumi.

David Kafulila na Zitto Kabwe ndio watu Pekee waliokuwa wanaibeba CHADEMA katika Hoja zote za Masuala ya Uchumi.

Mimi sio Chadema na Wala Sina chama Ila Kama kaijenga Chadema Sasa hivi Yuko act mbona ameshindwa kujenga na kutegemea wanachama waliotoka Cuf
Kumbuka ACT-WAZALENDO ilijengwa na wahanga toka Chadema, hivyo CUF ni wahamiaji je angewazuia kuingia au kujiunga na ACT-WAZALENDO? Hacha kuwa na akili za maharage za kukalilishwa
 
😂😂😂

Hakunaga Bure hii Dunia hasa kwa Umri mdogo kama wako

Kwa namna unavyomfagilia Kafulila au Kijana mwenzako kwa majukumu ambayo hata Wewe unaweza kuyafanya kwa Elimu Yako ni Kujilaani na Kujilaanisha Wewe mwenyewe

Wasanii wanaelewa hii Kanuni ndio Sababu Diamond anajisifia yeye hamsifii Hamornize

Sifia sifia ndio anasemaga RC Chalamila unakuta Vijana wa kiume wanaolewa🐼
Kwani lazima wote muwe viongozi.kwani ni dhambi kusema mtu fulani anafaa katika nafasi fulani ukiona mtu huyo kama Mheshimiwa David Kafulila anaweza nafasi fulani?
 
Kafurila hawezi kufanana na ZZK, ZZK ni born talent, Kafurila ni wakawaida sana aka wa kawaida na Kwa kiasi kikubwa anachoelezea ni kile ambacho kiko kwenye makaratasi tayari na hakuna input yake.

ZZK angalau ana kitu kipya kwenye Kila anachokizungumza au kuchambua, ZZK ana nguvu ya ushawishi inayomuwezesha kusimama peke yake kama jeshi la mtu mmoja.
 
Kwani lazima wote muwe viongozi.kwani ni dhambi kusema mtu fulani anafaa katika nafasi fulani ukiona mtu huyo kama Mheshimiwa David Kafulila anaweza nafasi fulani?
Nimekupa tu angalizo

Wanasiasa Wengi wanatumia ndumba hivyo akienda tu kwa Ngwezukulu Jilala akaambiwa Nyota yake na Yako zinaendana hapo bwashee Unaolewa bila kujali wewe ni wa kiume Ili umsifie Vizuri

Dunia hii ina mengi Dogo Lucas 🐼
 
Ameshindwa vipi kuijenga ACT wazalendo wakati unaona upande wa Zanzibar ipo katika serikali ya Umoja wa kitaifa?
Zanzibar waliokuwa na nguvu ni Cuf na baada ya kuhamia ACT wakaondoka na nguvu zao kuhamishia ACT hivyo Zitto hajaijenga ACT na tungeona nguvu yake bara.
 
Kumbuka ACT-WAZALENDO ilijengwa na wahanga toka Chadema, hivyo CUF ni wahamiaji je angewazuia kuingia au kujiunga na ACT-WAZALENDO? Hacha kuwa na akili za maharage za kukalilishwa
Wewe ndio una akili za kukalilishwa, hao wahanga wa Chadema walichukua Jimbo lolote zaidi ya kupata majimbo ya Zanzibar kwa nguvu za wanachama waliotoka Cuf
 
Zanzibar waliokuwa na nguvu ni Cuf na baada ya kuhamia ACT wakaondoka na nguvu zao kuhamishia ACT hivyo Zitto hajaijenga ACT na tungeona nguvu yake bara.
Ila mawazo yako ni mafupi sana .kwani wote waliopo CHADEMA na walioipa umaarufu walianzia hapo hapo CHADEMA? Unaelewa maana ya chama cha siasa? Unaelewa namna ya kujenga chama?
 
Ila mawazo yako ni mafupi sana .kwani wote waliopo CHADEMA na walioipa umaarufu walianzia hapo hapo CHADEMA? Unaelewa maana ya chama cha siasa? Unaelewa namna ya kujenga chama?
Ungekuwa unalelewa usingekuwa chawa, yanapokuja Mambo ya siasa wewe ni mtoto wa nursery kwangu.
 
Kafurila hawezi kufanana na ZZK, ZZK ni born talent, Kafurila ni wakawaida sana aka wa kawaida na Kwa kiasi kikubwa anachoelezea ni kile ambacho kiko kwenye makaratasi tayari na hakuna input yake.

ZZK angalau ana kitu kipya kwenye Kila anachokizungumza au kuchambua, ZZK ana nguvu ya ushawishi inayomuwezesha kusimama peke yake kama jeshi la mtu mmoja.
Unamfahamu Kafulila au unamsikia? Unafahamu ya kuwa hata ukiitishwa mjadala na CHADEMA na Kafulila akawa peke yake hakuna anayeweza mshinda Mheshimiwa Kafulila kwa hoja? Kafulila ni kichwa kwelikweli.
 
Kwa hiyo Zitto na Kafulila walivyokuwa wanaibeba CHADEMA mlikuwa mnaumia sana mukaona mfanye kweli ili wawabebe CCM?.
 
Uwezo wa mtu hatupimi Kwa kujua kuongea na kutusomea data ambazo tayari zipo au kuelezea yale ambayo Kila mwenye taalum yake anaweza kuyaelezea/kuyahadithia.

Uwezo wa mtu tunaupima kupitia michango mipya yenye kuleta matokeo chanya mahala, mipango, mikakati, uthubutu na utekelezaji unaoleta matokeo ndio vinaonyesha uwezo wa mtu na si blah blah.

Leo hii ukimuita engineer akuelezee aliyosamoea na kuyafanyia kazi basi utamuona ana akili sana, ukimuita mganga wa kienyezi akuelezee matunguli yake na uganga wake utamuona genius sana, ukimuita Mwanasheria akuelezee Sheria yake kama TL utamuona genius kwelikweli.

Ugenius ni kuyatumia yale uliyosomea kuleta matokeo chanya na pia kuongeza ufanisi kwa kuleta ubunifu wako ambao wengine hawawezi.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa Wafuatiliaji wa siasa za Nchi hii mtakubaliani nami kuwa Mheshimiwa David Kafulila pamoja na Mheshimiwa Zitto Kabwe ndio watu Pekee waliokuwa wanaubeba Upinzani hasa CHADEMA katika masuala na hoja zote zinazogusu na kuhusu Uchumi.Ndio maana CHADEMA mpaka sasa huwezi ukaona au kumuona mtu yeyote akizungumza masuala ya uchumi au sera za uchumi au mbadala wa sera fulani.

Ndio maana ilifika wakati CHADEMA ikawa inashindwa hata kuandaa tu bajeti mbadala Bungeni,na ikiandaa ilikuwa ni bajeti yenye vichekesho vingi sana.kwanini? Kwasababu ilikosa watu wenye uelewa , weledi na wasomi wa masuala ya uchumi.Ndio maana ikabidi wampe Mheshimiwa Halima Mdee kama waziri kimvuli wa Fedha ,Kiongozi ambaye alikuwa hana uelewa mpana wa masuala ya kiuchumi kwa kuwa yeye alikuwa amesomea masuala ya sheria.kwa hiyo mambo mengi ya kiuchumi kwake yalikuwa mageni na magumu kuyatengenezea sera na hoja na kuelezea kwa ufasaha na akaeleweka vyema kwa watu.

Ikumbukwe kuwa Uchumi ni kanuni na wala uchumi hauhitaji siasa siasa au blaa blaa au maneno maneno.ukiukosea uchumi katika kanuni zake ni lazima Ukuadhibu na kukuumbua. kwa sababu kuna mambo unaweza kuficha na kudanganya ,lakini huwezi kudanganya na kuficha matokeo ya sera zako za uchumi ,kwa sababu matokeo yake ya sera zako yataonekana katika maisha halisi ya watu. Ndio maana ya kusema uchumi una kanuni zake ambazo ukikosea tu ni lazima kilio kisikike kutoka katika vinywa na midomo ya watu hata kama hawajasomea Uchumi.

Hivyo basi kuondoka kwa watu aina ya Mheshimiwa David Kafulila na Zitto Kabwe, ndio maana Upinzani hasa CHADEMA umepwaya sana na umeshindwa kuwa na sera mbadala wala hoja zenye kumgusa mwananchi wala kuwa na uwezo hata tu wakumshawishi mwananchi wa kule kijini akawaelewa.ndio sababu unakuta CHADEMA inakuwa inakimbilia sana na kuendesha siasa zake kwa kufuata matukio na kuokoteza vihabari visivyo na mashiko .ndio maana unaweza ukakuta viongozi wa CHADEMA eti wapo Bize na hoja ya kujadili kwanini kiongozi fulani haonekani hadharani.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Siyo lazima tukubaliane na wewe. Futa kauli ya mwanzo
 
Unamfahamu Kafulila au unamsikia? Unafahamu ya kuwa hata ukiitishwa mjadala na CHADEMA na Kafulila akawa peke yake hakuna anayeweza mshinda Mheshimiwa Kafulila kwa hoja? Kafulila ni kichwa kwelikweli.

Kushinda kwenye mjadala kubishana ndio kigezo chako kumbe na si uelewa mpana wa kiasi cha kutoa solution ya matatizo na hata kudesign structure na operations zinazotoa majibu ya matatizo?
 
Kushinda kwenye mjadala kubishana ndio kigezo chako kumbe na si uelewa mpana wa kiasi cha kutoa solution ya matatizo na hata kudesign structure na operations zinazotoa majibu ya matatizo?
Hicho unachokisema ndicho anachokifanya Mheshimiwa Kafulila kutoa hoja zenye suluhisho na majibu.
 
Back
Top Bottom