David Kafulila ni Mkuu wa Mkoa Pekee Nchini ambaye amewahi kumpa Amri Mkandarasi kurudia Barabara kwa gharama zake

David Kafulila ni Mkuu wa Mkoa Pekee Nchini ambaye amewahi kumpa Amri Mkandarasi kurudia Barabara kwa gharama zake

Ndugu zangu Watanzania,

Napowaambia kuwa David Kafulila ni Chuma nakuwa namaanisha ni CHuma kwelikweli na Mzalendo wa dhati Wa Taifa letu,ambaye huwa hayumbi wala kuyumbishwa wala kutetereshwa wala kuogopa wala kupoozwa wala kuangalia ni nani anayepambana naye au aliye mbele yake.

Chuma David Kafulila ni CHuma ambacho husaga uozo wowote ulio mbele yake .Ni mtu aliyenyooka kama rula ambaye huwezi kumpindisha kwa vihela vyako vya rushwa au hongo.

Sasa nisiwashoshe .ipo hivi jamaa alipoingia Mkoani Simiyu alikuta kuna barabara inajengwa na Mkandarasi,ambapo baada ya kuikagua akagundua kuwa ipo chini ya kiwango na haiwezi kudumu kwa muda mrefu ,na hivyo italeta hasara kwa serikali kwa kuanza kuirudia kwa gharama na kodi za watanzania wanyonge.

Baada ya kugundua uozo huo uliofanywa na Mkandarasi ,alitoa amri kali na maagizo mazito kwa mkandarasi kwa kumtaka arudie barabara hiyo ya urefu wa KM 20 inayogharimu takriban Billion 40 kwa gharama zake mwenyewe Mkandarasi na ikamilike kwa ubora unaohitajika na kwa wakati muafaka. Maagizo hayo yalitekelezwa haraka sana na mkandarasi kurudia ujenzi kwa gharama zake na kuwa fundisho kwa wakandarasi wengine.

Hii maana yake nini ndugu zangu? Hii inamaanisha kuwa kama barabara hiyo ingepokelewa katika ubovu wake huohuo, maana yake ingeshuhudiwa mvua kidogo tu ikinyesha barabara inaanza kukatika na kumomonyoka kila sehemu,lakini pia ingeshuhudiwa barabara hiyo ikianza kuwa na mimashimo mashimo kila sehemu na hivyo kusababisha hata ajali za barabarani.

Lakini kubwa na baya ni kuwa serikali yetu ingeingia hasara ya kuanza kutoa pesa zingine mamilioni kwa mamillioni kurudia na kurekebisha barabara hiyo .pesa ambazo zingeweza kutumika kujenga miradi mingine kama vile shule,vituo vya afya, zahanati,ununuzi wa madawa na vifaa tiba, usambazaji wa maji safi na salama n.k.

Lakini Chuma Kafulila kwa uzalendo wake na unyoofu wake kimaadili na uaminifu wake kwa Taifa letu akaokoa gharama hizo na pesa hizo. Hii ndio maana tunasema hiki chuma ni habari nyingine,ni CHuma cha moto kwelikweli ambacho hakijawahi kuwa na huruma na mafisadi,wezi na wala rushwa.

Hii ndio maana nampongeza na kumuunga sana mkono Mh kafulila.ndio maana natamani kuona akirejea Bungeni hapo Mwakani,ndio maana nina kiu ya kuona akiendelea kuwepo Serikalini kwa kuwa chochote kinachokuwa chini yake na mikononi mwake kinakuwa kipo mahali salama na penye usalama,tofauti na wengine ukiwakabidhi nafasi fulani wanaigeuza kuwa mrija wa kufyonza pesa na kodi za watanzania kama mchwa wenye njaa .

Naweka kalamu yangu chini ili andiko lisiwe refu kupita kiasi hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa watanzania ni watu wavivu sana katika kusoma vitu na ndio maana ukitaka kumuibia mtanzania basi muwekee jambo hilo katika maandishi na mahali pa kusaini.uone namna atakavyo saini haraka haraka bila kujuwa kilicho andikwa.halafu kesho unaona hata yeye anaanza kushangaa na kutoa macho anapo ambiwa kile alichokisaini.

Kazi iendelee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Mkuu hongera kwa kupata shavu la ppp baina yako na Kufulila, sasa usilete kwa kupayuka, usimsifie mshirika mwenzio mpaka ukamharibia!!!
 
Yes David,

Ni miongoni mwavijana wachache ambao huwezi kuwanunua kwa namna yeyote ile.

Sisi kama vijana lazima tujifunze kujitambua na kutambua vijana wenzetu ambao ni tumaini kwaajili ya Chama chetu na Serikali yetu.

Kafulila amekuwa role model wa wengi katika Uadilifu na Utumishi.

Kafulila chapa kazi tuko na Wewe tuko na Mama yetu Kipenzi asiyekuwa na Mpinzani.

Kama umesaidia kuokoa zaidi TZS40BIL za Watanzania hawa masikini acha tukupongeze.

#VIVA SAMIA VIVA, VIVA KAFULILA VIVA

Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
Mkuu umesahau unayemsifia naye alinunuliwa na Pole Pole kama anunuliwapo mbuzi kwenye mnada!!! Kafulila, Zito na Mkosamali, ni the trio of betrayal! Upepo ukibadilika utaona usaliti wao!!!
 
Mkuu umesahau unayemsifia naye alinunuliwa na Pole Pole kama anunuliwapo mbuzi kwenye mnada!!! Kafulila, Zito na Mkosamali, ni the trio of betrayal! Upepo ukibadilika utaona usaliti wao!!!
Mheshimiwa Kafulila hajawahi kuwa na bei wala kuhongwa.
 
Yes,

Huo ndio uwajibikaji katika uongozi.

Lazma thamani ya miradi ya maendeleo isimamiwe vyema kwa weledi, kulingana na thamani ya jasho la walipa kodi waTanzania. wanaoleta mzaha na kazi za maendeleo wawajibishwe inavyostahili 🐒
Lazima Viongozi wawe proactive ili kulifanya Taifa kuwa na miundo mbinu imara
 
Mkuu hongera kwa kupata shavu la ppp baina yako na Kufulila, sasa usilete kwa kupayuka, usimsifie mshirika mwenzio mpaka ukamharibia!!!
Kwani huyu Lucas Mwashambwa anatumwa kufanya hivyo?

Kama hatumwi Kafulila anahusikaje na Sifa hizi?

Huyu kada wa CHAMA anapoamua kuwajenga makada wenzake hatuwezi kuwa victimize kwa pleasure za mtu au interest za mtu.

Acha wivu Japa kazi utasifiwa.
 
Kafulila ni Mtu jasiri hicho ndicho naweza kusema kwa uwazi kabisa
watu wanapiga kelele sana wanataka kuona viongozi wakiwajibika kwa uwazi...

cha kushangaza wakifanya hivyo inakua nongwa tena dah...

sasa unajiuliza wanataka nini watu hawa?🐒
 
watu wanapiga kelele sana wanataka kuona viongozi wakiwajibika kwa uwazi...

cha kushangaza wakifanya hivyo inakua nongwa tena dah...

sasa unajiuliza wanataka nini watu hawa?🐒
Kinachowasumbua na kuwatesa watu ni wivu Uliopitiliza.
 
Mkuu umesahau unayemsifia naye alinunuliwa na Pole Pole kama anunuliwapo mbuzi kwenye mnada!!! Kafulila, Zito na Mkosamali, ni the trio of betrayal! Upepo ukibadilika utaona usaliti wao!!!
Nadhani kuna jambo mnashindwa kuliweka sawa,

Binafsi nimemuelewa mwandishi logic yake ya kwanini Kafulila,

Mwandishi anaona Uzalendo wa Kafulila haujawahi kuwa affected na cross Party yoyote.

Unaweza ukajiuluza mtu anayekataa 2.8bl 2014 anawezaje kununuliwa 2016? na kama amenunuliwa kapewa kiasi gani?

Mwandishi anajikita kwenye Uzalendo wa Kafulila na sio haki yake ya kuhama chama toka Cha B kwenda Chama A.

Hoja ya Kafulila kununuliwa haipo na hakuna mtu mmoja kwenye Taifa hili anaweza kukuunga mkono kwamba Kuna mtu alimnunua Kafulila.

Kafulila kama mwanasiasa mwenye malengo yake kisiasa anaangalia ni wapi anaweza kutimiza malengo yake ya kisiasa hasa kuwatete hawa wanyonge.

Tanzania haina chama zaidi ya CCM kwanini mtu mwenye akili timamu asiione CCM kama daraja lake sahihi na kufikia ndoto zake?
 
Back
Top Bottom