Shekaina Glory
JF-Expert Member
- Jun 18, 2025
- 207
- 116
Dar es salaaam, Akiongea mbele ya wachambuzi wa habari na uchumi, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia Nchini (PPPC), Bw. David Kafulila amesema moja ya sekta inayofanya nchi ikue kiuchumi ni pamoja na Rasilimali za nchi.
Aidha, Kafulila alisema kuwa mbali na maji, Awamu ya Sita imefanya makubwa katika sekta ya utalii, hasa upande wa watalii wa ndani, na hili limekuwa chachu ya ukuaji wa mapato ya Taifa. Ongezeko kubwa la mapato linaonesha wazi kuwa ubora wa vivutio na huduma za utalii nchini umeimarika.
Mafanikio ya Serikali ya awamu ya Sita,

- Watalii wameongezeka kutoka milioni 1.4 mwaka 2020 hadi zaidi ya milioni 5.3 mwaka 2024.
- Mapato ya utalii wa nje yameongezeka kutoka dola milioni 700 hadi dola bilioni 3.9 (zaidi ya Sh. trilioni 10).
- Mapato ya utalii wa ndani yameongezeka kutoka Sh. bilioni 46.3 hadi bilioni 209.8.
Kuhusu mjadala wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), Kafulila alifafanua kuwa kuna tofauti kati ya accounting loss (hasara ya kihasibu) na economic loss/profit (faida au hasara halisi ya kiuchumi).
Kwa mujibu wake, hata kama kihasibu ATCL inaonekana kupata hasara, ndege zake zimekuwa zikileta maelfu ya watalii walioliletea Taifa faida ya zaidi ya dola bilioni 3.9. Hii ni faida ya kiuchumi kubwa mno kuliko hasara ndogo ya kimaandishi inayotajwa na CAG.

“Kwa mtazamo wa kiuchumi, ndege zetu hazina hasara – zinafungua milango ya utalii, na watalii wanatuingizia mapato makubwa mno kuliko hasara ndogo ya kihasibu. Hiyo ndiyo faida ya kweli kwa Taifa,” alisema Kafulila.