CM 1774858
JF-Expert Member
- May 29, 2021
- 6,157
- 5,451
Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kung’ara kama kiongozi wa mfano barani Afrika, akibadilisha taswira ya Tanzania kupitia uongozi wenye dira, maono na vitendo vinavyogusa maisha ya wananchi moja kwa moja. Kupitia uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya mawasiliano, elimu, afya, maji, nishati na barabara, Rais Samia ameifanya Tanzania iwe kinara wa mageuzi ya maendeleo na chachu ya ustawi wa wananchi. Ameweka msisitizo katika uwazi, diplomasia ya kiuchumi, uwezeshaji wa wanawake na vijana, huku akihakikisha kuwa kila shilingi inayowekezwa inaleta matokeo yanayoonekana. Hatua zake za kuboresha huduma za jamii na kuimarisha uchumi zimeongeza heshima ya nchi kimataifa, na leo Tanzania inatambulika kama taifa lenye uthabiti, matumaini na mustakabali imara chini ya uongozi wake thabiti na wenye dira.==
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha ubia nchini Tanzania PPPC Bwana David Kafulila akihojiwa katika kituo maarufu cha runinga cha ITV kwenye kipindi cha DK 45 alikuwa na haya ya kusema,
Ukiachilia mbali Usambazaji wa Umeme kwenye vijiji elfu 12 Tanzania ilisafirisha Umeme umbali wa kilometa 6,000 tangu tupate uhuru mwaka 1961 December laki leo tumefikia kilometa 800.
Maajabu ni haya Kwa kipindi kifupi Cha miaka minne Cha Rais wa awamu ya sita Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan yeye amesafirisha Umeme kwenye zaidi ya kilometer 2,000 ambazo ni sawa na 33.333% ya kilichofanyika awamu zote tano zilizomtangulia,
Hakika Mama huyu anastahili pongezi kweli kweli,
===
Msikilize kwa umakini kwa faida yako kwa ufahamu wa mambo mengi zaidi.
,