Jabali la Siasa
JF-Expert Member
- Jul 10, 2020
- 3,629
- 3,015
Kafulila: Taasisi Inayoongozwa na Mwanamke Huleta Mafanikio zaidi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia nchini Tanzania (PPPC), Bwana David Kafulila, akihutubia katika Tengeru Institute of Community Development (TICD) jijini Arusha, amesema kuwa taasisi yoyote itakayoongozwa na mwanamke kwa kiasi kikubwa huongoza kwa mafanikio.
Kafulila alieleza kuwa mafanikio ya taasisi na maendeleo ya taifa yanategemea uwiano sahihi kati ya sekta binafsi, serikali na jamii. Alisisitiza kuwa sekta binafsi ikikua na kuwa kubwa, huku serikali ikibaki ndogo na yenye jukumu la kutunga sera na kusimamia kanuni, ndipo ustawi wa wananchi unaweza kufanikishwa.
“Tunapaswa kuwa na serikali ndogo, sekta binafsi kubwa na civil society yenye nguvu. Hiyo ndiyo fikra ya kizazi kipya cha utawala — small government, bigger civil society. Serikali inapaswa kuongoza kwa sera na udhibiti, lakini ustawi wa watu unapaswa kubebwa na sekta binafsi na jamii yenyewe,” alisema Kafulila.
Akiendelea, Kafulila alionya kuwa serikali ikijikita kumiliki kila kitu — kuanzia stendi za mabasi hadi biashara ndogo ndogo — mzigo wa kodi unakuwa mkubwa mno na hauwezi kuhimili mahitaji ya kisasa. Badala yake, alihimiza kukuza sekta binafsi na kuimarisha civil society ili kuchochea uzalishaji na ustawi wa wananchi.
Aidha, Kafulila alitaja mfano wa viongozi wa kimataifa akisema: “Hii ndiyo fikra ambayo viongozi kama David Cameron waliita the next age of governance — serikali ndogo, sekta binafsi kubwa, civil society kubwa.”
Kwa kumalizia, Kafulila alisisitiza kuwa ili kufikia maendeleo endelevu, Tanzania inapaswa kuwekeza katika sekta binafsi yenye nguvu, kuimarisha civil society, na kuhakikisha serikali inabaki ndogo na yenye jukumu la sera na udhibiti pekee.
===