David Kafulila: Wakati wa Rais Samia hati safi zimefikia 99% kutoka 89%

CM 1774858

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2021
Posts
6,157
Reaction score
5,451
==
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia nchini Tanzania PPPC Bwana David Kafulila katika ukurasa wake wa tweeter ( X ) amemtetea na kumpongeza Rais wa Tanzània Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kupata ripoti nzuri ya CAG kwa jumla,

Bwana David Kafulila anasema Rais Samia na katika Kipindi chake hiki kifupi na kwa mujibu wa ripoti ya CAG ameongeza zaidi hati safi kutoka hati safi 800 za wakati wa Hayati Dkt John John Magufuli hadi hati safi 1,295 za sasa wakati wa Dkt Samia.

Mkurugenzi David Kafulila anaendelea kwa kusema vilevile Dkt Samia Suluhu Hassan amepunguza hati chafu kutoka hati chafu 10 za Wakati wa Hayati Dkt Magufuli hadi hati chafu moja (1 ) ya wakati huu wa Dkt Samia.

Wakati hati zenye mashaka nazo zikipungua kutoka hati zenye mashaka 81 za Wakati wa Hayati Dkt Magufuli mpaka hati zenye mashaka 5 za Wakati huu wa Rais Samia Suluhu Hassan

Kwa matokeo haya na Kwakuwa namba hazidanganyi basi huenda Rais Samia hapigi sana kelele kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake ila yeye Sasa anatenda kazi zake kupitia kalamu kimya kimya kama alivyowahi kukaririwa na vyombo vya habari wakati flani.


==

​



==
 
Samia ni mzuri zaidi ya wote
 
Ujinga ni ku-promote mataahira kama Kafulila kutwa yanaongea ujinga tu.

Mbaya zaidi ni kujiaminisha ujinga ni facts.

Labda umaskini wa Africa ni fate, bara zima weruvu hawawezi kukubali kuongozwa na wajinga.

Umaskini wa Tanzania ni uwezo mdogo wa viongozi wa nchi, na kuna waelevu wengi ambao wame-give up na kuwaachia siasa mapoyoyo.
 
Huyu Mwanza ni mbobevu wa takwimu
 
Si kweli. Angekuwa mkali chawa kama Kafulila angekuwa keshatumbuliwa na kusahaulika zamani gani?
 
Sasa unalalamika kwani Kafulila ndio CAG?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…