David Mataka wa ATCL, ahukumiwa kulipa faini Tsh milioni 8 kwa kulisababishia hasara ya Tsh Bilioni 71 shirika

David Mataka wa ATCL, ahukumiwa kulipa faini Tsh milioni 8 kwa kulisababishia hasara ya Tsh Bilioni 71 shirika

Bosi wa zamani wa ATCL David Mataka amehukumiwa kwenda jela miaka minne ama kulipa faini ya Sh milioni 8 baada ya kukutwa na hatia ya matumizi mabaya ya ofisi na kusababishia shirika hasara ya Sh bilioni 100.
Labda tungewaomba China watusaidie kutoa hukumu!
 
Halafu utasikia mtu anawasema wapinzani eti wanafiki duh! wacha tulipe kodi mtu mmoja azitafune halafua asamehewe kiujanja ujanja kwisha habari yetu.
 
Hii nchi raha sana.
Unaiba bilioni 100 unaadhibiwa kwa faini ya milioni 8 (yaani 8/100,000).
Watu wenye madaraka juu ya fedha za umma wanapata ujumbe gani kutokana na hukumu hii?
Ujumbe wakwapue tu hakuna shida wala hakuna kubugudhiwa 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Haifikii hata deni la bodi ya mkopo wa kozi ya miaka mitatu🤣
 
Kuna mhasibu flan aliniambiaga yeye haibagi ivi vi milioni 200, au 300, yeye anaanzia milioni 500, kwani hakuna hakimu wa kukataa milioni 200.

Na keshafukuzwa makampuni mengi tu kwa wizi, na kesi anashinda.
 
K*m*mae kabsaa yani hasara 100billion alaf faini mil 8!!? Na hio bil 100 je anairudisha ama ndio imetoka hvyo?
 
Duh, Sasa kwa jamaa huo si ni mchango wa kipaimara Cha mwanae jamani...ndo Mana wageni kama waasia wanakuja na nguo mbili tu za kubadilisha hapa nchini , wanajua hata wakipiga dili ya billions of money faini ni pesa ya pikipiki aina ya boxer...
 
Kwa nini serikali isizile kuipokea hiyo fine ya huyo mfukua mitaro
 
Undava muhimu sana kwenye utawala wa hizi nchi...huyu unaweza kuta kisheria hana makosa kabisa lakini ukweli ni kwamba katutia hasara kubwa tena kwa makusudi...
Inawezekana kabisa Mtaka hana kosa lolote. Kusababisha hasara siyo kosa kisheria. Kama bodi ilipitisha bajeti naye akatekeleza bila ufisadi wala wizi, hasara ni matokeo ya wote upto the level ya juu kabisa ya waliokuwa wanapitisha maamuzi ya uwekezaji na uendeshaji.

Kama tunavyojua, mwamuzi wa mwisho wa ATCL ni bunge linalopitisha bajeti mwaka, na mamlaka ya uteuzi iliyomwacha kazini hata ilipoona hasara zinazidi kulimbikizana. Tuache siasa kwenye mambo ya kiutaalamu.
 
Back
Top Bottom