David Mwaibula, aliyebuni mistari ya daladala Dar es salaam yupo wapi?



Mzee David Mwaibula almaarufu "Makofia" aliyekuwa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Leseni za Usafiri Dar es Salaam (DTLA) ndiye mbunifu na muasisi wa mfumo huu wa kupaka daladala mistari.

Ubunifu wa Mzee David Mwaibula uliigwa hata na Mamlaka zingine za Miji na Majiji Tanzania Bara.

Mara ya mwisho kuonekana hadharani Mzee David Mwaibula ilikuwa mwaka 2016 kipindi ambapo Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa alipotembelea mradi wa Mabasi yaendayo kwa haraka (DART).

Hakika Mzee wetu David Mwaibula anastahili pongezi za dhati kwa ubunifu huu ambao umeweza pia kuzinufaisha Mamlaka kama VETA.

Tuwaenzi Wazee wetu.

Kona ya Wahenga.
 
Kwa sasa yupo wapi kama mara ya mwisho kuonekana ilikuwa 2016?
 
Tangu lini mkurugenzi au mwenyekiti akawa ndiye mbunifu wakati analetewa proposal mezani kutoka kwa wabunifu?

Mambo kama haya ndiyo hukatisha tamaa wabunifu kujitokeza
 
YUPO ila kwa TANZANIA ukimaliza Muda wako unatupwa jalalani
 
hebu tupe wewe hizo njia unazoona zinafaa tujirekebishe
 
Apongezweee
 
Kuna hii tabia ya makondakta na madereva kukatisha safari, hawafiki mwisho wa safari husasan katika Jiji la Dar es Salaam.

Jana nilipanda daladala ya kutoka mbagala kwenda muhimbili. Nilivyoingia ndani nikamsikia Mzee Moja, miaka yake kama zaidi ya 60 hivi, analalamika kwa nini konda amechukua ela ya abiria alafu anasema hafiki muhimbili

Kumbe yule Mzee akawa wanabishana na konda, hakutoa ela yake na kusema hii gari isipofika muhimbili sikupi nauli na alikuwa sawa kabisa na wengi wa wale abiria walikuwa wanaelekea muhimbili, ila wao wakawa wamenyamaza kimya yule Mzee ndo walikuwa wanabishana na konda nikasema ngoja na Mimi nitulie nione mwisho wa hii safari nikawa mkimya tu Wala sikuzungumza mle.

Safari ikaendelea tulivyofika pale mataa ya kamata dereva akakunja kuelekea mnazi, yule Mzee kwa sauti kubwa akatoa kichwa dirishani akamuita trafiki kwa sauti hii ni gari ya muhimbili ila konda hataki kutupeleka mwisho (muhimbili). I mwisho akapaki daladala kwenye kituo Cha gerezani konda akasema hapa ni mwisho abiria wote wakashuka yule Mzee akasema anaenda kumuita trafiki[emoji1],wale abiria wote wa muhimbili wakawa wanalalamika, ila wote wakashuka na Mimi nilikuwa mle nikawa nimetulia,

Nikamuita yule Mzee naomba usiende Rudi hapa, akawa amenielewa, nikazunguka nyuma nikapiga Ile plate namba ya daladala ikanyanyua simu yangu na kupiga Moja kwa Moja kwa yule askari aliyekuwa pale mataa. Nikamwambia naomba askari Moja afike hapa Kuna sitofahamu, nikawaambia wale abiria naombeni wote mrudi kwenye gari hii daladala itawafikisha muhimbili pamoja na Mimi nikiwa humu, yule konda alikuwa mjanja sana baada ya kuona hapa hali ya hewa haitakuwa salama,nikamfuata dereva nikamwambia mwisho wa safari ya hii daladala ni wapi ,akasema Muhimbili.

Nikamwambia naomba utufikishe Muhimbili, kwa usalama wako na konda wako.

Akawasha gari, nikawa mkimya tu namtazama jinsi alivyokuwa anaendesha taratibu akatupitisha nyuma ya faya kule kwa ajili tu ya kutuchelewesha, kumbe anajichelewesha mwenyewe.

Tulivyofika muhimbili sikushuka kwenye gari nikamwambia geuza hii gari na ukimuona askari wa barabarani naomba usimama, tulivyofika fire akasimama na nikamuomba atoe maelezo, nikamwambia askari umemuelewa konda na dereva wake,akasema ndio ikamjibu fanya kazi ya serikali juu yake, na nitafuatilia kama hii namba imepigwa faini.

Tujenge nchi kwa maendeleo endelevu
 
Unauzalendo kamanda kweli kweli ila sisi wengine tutakuvunja mwoyo, mimi naonaga ma konda wengi ni wehu sina mda wao na wachiaga Mungu, na hiyo nauli ya 400 naiona kama Sadaqa
 
".. nikazunguka nyuma nikapiga Ile plate namba ya daladala, nikanyanyua simu yangu na kupiga Moja kwa Moja kwa yule askari aliyekuwa pale mataa .."

Uliijuaje namba ya simu ya huyo askari mataa?

Au alikuwa poti?
 
".. nikazunguka nyuma nikapiga Ile plate namba ya daladala ,nikanyanyua simu yangu na kupiga Moja kwa Moja kwa yule askari aliyekuwa pale mataa .."

Uliijuaje namba ya simu ya huyo askari mataa?

Au alikuwa poti?
Huwezi kunielewa,labda nikwaambie tu siyo kila nilichozungumza niseme. Nikusaidie tu kidooogo. alinijibu tu naomba unisaidie plate namba, ila sikuridhika nikasema ngoja tu nilibebe
 
".. nikazunguka nyuma nikapiga Ile plate namba ya daladala ,nikanyanyua simu yangu na kupiga Moja kwa Moja kwa yule askari aliyekuwa pale mataa .."

Uliijuaje namba ya simu ya huyo askari mataa?

Au alikuwa poti?
Tukio huenda likawa la kweli, Ila mzungumzaji ni takataka.
 
Nafasi yako ndoimekubeba oelse ungenyanyasika tu kama sisi abiria wengine hii nchi usipokua unamjua mtu mkubwa au wewe kuwa na wadhifa flani utanyanyasika tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…