sunguramjinga
Senior Member
- May 11, 2023
- 175
- 227
Picha: Ummy Mwalimu
Serikali imesema dawa za kidonge myeyuko cha Amoxicillin, Zinki na ORS kwa ajili ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano, haziuzwi, zinatolewa bure kwa wananchi, kwa sababu zinanunuliwa na serikali kwa kushirikiana na wadau.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu wakati akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara ya Afya kwa mwaka 2023/2024, Bungeni, Jijini Dodoma ambapo amewaelekeza Waganga Wakuu wa mikoa na Halmashauri wasimamie suala hilo kwa ukamilifu.
Source: ITV