Dawa aina ya Amoxicillin, Zinki na ORS ni bure kwa watoto chini ya miaka 5

sunguramjinga

Senior Member
Joined
May 11, 2023
Posts
175
Reaction score
227

Picha: Ummy Mwalimu

Serikali imesema dawa za kidonge myeyuko cha Amoxicillin, Zinki na ORS kwa ajili ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano, haziuzwi, zinatolewa bure kwa wananchi, kwa sababu zinanunuliwa na serikali kwa kushirikiana na wadau.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu wakati akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara ya Afya kwa mwaka 2023/2024, Bungeni, Jijini Dodoma ambapo amewaelekeza Waganga Wakuu wa mikoa na Halmashauri wasimamie suala hilo kwa ukamilifu.

Source: ITV
 
Dawa zenyewe zipo kweli mahospitalini? Hizi ni ofa Tu za kisiasa hazina ukweli ndani yake
 
Duka gani tukachukue
 
Njoo filed sasa [emoji23][emoji23][emoji23], utajua hujui
 
hakuna cha bule ,hapo watumishi wa hospital ndo wamepatapo pa kupigia...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…