Dawa hizi zinaponesha fangasi?

Dawa hizi zinaponesha fangasi?

Et ndugu kuna MTU Alie wahi kuugua fungas sugu akatumia izi sindano zikamsaidia gentamicin injection au seftriason injection kama yupo aseme


Wewe sema fungus tu wala usiweke neno "sugu" kwani kitu kikishakuwa sugu hicho kinakosa dawa.
 
Duh sizan kama ntapat tiba bro naangaika sana


Usikate tamaa hakuna ugonjwa wa kawaida kama fungus ukakosa dawa, kwani umetumia dawa zipi za hospitali??

Juu ya yote usafi wa nguo za ndani ni muhimu, kila unapotumia dawa unatakiwa uvae nguo ya ndani safi iliyofuliwa kwa maji ya moto na kupigwa pasi baada ya kukauka ili kuua fungus zilizo ganda kwenye hizo nguo.

Dawa nyingine ya fungus ni asali mbichi, unapakaza sehemu husika kila asubuhi baada ya kuoga. Inshallah kwa uwezo wa Mungu utapona.
 
Duh sizan kama ntapat tiba bro naangaika sana
Unaamini tibambadala??yapo majani yanaitwa mziwaziwa yapondeponde pakaa apo kwenye fangasi Tena ikibidi pakaa usiku weka mengi vaa na chupi Ili yasitoke alafu asubuhi angalia utaona fangasi sugu zimekauka.Tumia angalau siku 5,na vizuri zaidi mengine ukashemsha utumie kama chai inatibu mpka fangasi zoote na minyoo.Dozi yake kwakunywa ni ujazo wa kiganja Cha mkono tumia bila mizizi
 
Kwenye korodan mkuu
Kama ni sugu kweli tafuta dawa hii Amphotericin B.

Ila pia jaribu kubadili mfumo wa usafi wako. Fungus wanapenda sana unyevunyevu. Epuka mno kuvaa nguo za kubana, kuvaa nguo baada ya kuoga bila kujikausha maji. Weka mfumo wa kubadili boxer safi at least kila siku.
Ukilala usilale na nguo za kubana, acha dhakari ipate hewa, ikiwa unaishi mwenyewe ama na mama watoto tu basi ni bora ukalala uchi kabisa tena hii itaimarisha ndoa yenu maana shemeji atakuwa hapati tabu kujihudumia.

Pia tafuta powder ya miconazole, kabla ya kulala nyunyuzia pumbuni na maungio yake yote.
Ndani ya wiki utakuwa brand new.
 
ni bora ukalala uchi kabisa tena hii itaimarisha ndoa yenu maana shemeji atakuwa hapati tabu kujihudumia.

Yeye anasema anaugua fungus sugu sasa haya mambo ya "shemeji kijihudumia" (self service) yamekujaje??? -- au shemeji kujihudumia ni dawa ya fungus ??!!😏😏

Katika hali ya huo ugonjwa mimi nadhani hata hiyo huduma (kama ipo) ya tendo inabidi aisitishe kwa muda kwani yawezekana nayo ikawa inachangia pakubwa kwenye ugonjwa..
 
Yeye anasema anaugua fungus sugu sasa haya mambo ya "shemeji kijihudumia" (self service) yamekujaje??? -- au shemeji kujihudumia ni dawa ya fungus ??!!😏😏

Katika hali ya huo ugonjwa mimi nadhani hata hiyo huduma (kama ipo) ya tendo inabidi aisitishe kwa muda kwani yawezekana nayo ikawa inachangia pakubwa kwenye ugonjwa..
relax hebu punguza shobo basi bibie. Katika comment yote umeona kwa shemeji tu?

Alieambiwa kakaa kimya wewe unaleta ushawishi. Tulia basi bibie, maisha ni mafupi mno kuchukulia kila kitu so seriously.
 
Back
Top Bottom