Wakuu msaada nimemaliza dawa ila panya hawapungui
Kuna kiboko nyingine
Tumia vidonge fulani fulani hivi vya tiba ya mifupa kwa binadamu. Vidonge hivyo vinaitwa kwa jina la "Androgen", kama sijakosea jina.
Vidonge hivyo ni sumu nzuri sana ya kuulia panya kwa sababu:-
1. Ni rahisi Sana kuitumia, unawachanganyia kwenye chakula kama vile unga wa sembe.
2. Panya wanakufa wakiwa wamekauka, hivyo hawatoi harufu mbaya.
3. Vidonge hivyo siyo sumu kwa wanyama wengine wa kufugwa kama vile kuku, paka, au mbwa ambao watakula mizoga ya panya waliokufa kwa sumu hiyo.
4. Vidonge hivyo havitoi harufu kali ambayo itawafanya panya waweze ku-detect uwepo wa sumu kwenye 'chakula Cha mtego.', n.k.
NOTE:-
Ukiwatega panya kwa kutumia mtego huo hakikisha kwamba unafunika kabisa ndoo za maji zote kabisa ili panya wakose kabisa kunywa maji baada ya kula chakula cha sumu. Wakipata nafasi ya kuweza kunywa maji basi hawataweza kufa.
Huu ni ushuhuda kutokana na uzoefu wangu binafsi kuhusiana na suala kama hili.