tatizo kubwa ambalo huwa naliona kwa watz wanaozamia nje ya nchi, ni ushamba tu. yeye anaona raha sana kukaa sehemu anaona mazingira mazurii, hajui wenzake waliyajenga kabla yeye hajaenda, hata kama hana hela anajiona yuko juu, kumbe unaweza mkuta mtz amebaki hapahapa bongo ametengeneza hela balaa lakini anaishi zake kibaha au chaline, moro etc tu hapo.
huko ulaya mnapata shida sana, rudini nyumbani, mnadharaulika kwanza kwa rangi yenu, dini zenu, na umasikini wenu. mnashinda kutitisha/kutawaza vizee vya kizungu na matahira tu huko, kubeba mabox na kujifanya mko juu wakati mnaishi maisha magumu balaa.
halafu, mbona tukija huko mnatuomba sana hela wakati nyie ndo mko ulaya sisi tunatoka bongo? mmepauka kam ahamko ulaya..hahaa. hakika nakuambia, kati ya vitu vya kuepuka ukitembelea ulaya au america, ni kuwa karibu na mtz mzamiaji. wanakuwa tegemezi hadi kwa wanafunzi. mtu amekuja zake kusoma tu huko lakini mababa mazima yanaomba hela ya kula yanatia huruma, rudini home, acheneni na utumwa huo. dah.