Dawa ya kumrudisha mpenzi, mume/mke mliyeachana inawezekana kweli?

Kuna mkitabu niliwahi usoma unaitwa Forbidden Education mkubwa una page nyingi tu basi kuna vitu viingi kama hivyo na vingine zaidi hata ya hivyo japo nilishindwa ku practice kujua yaliyomo ni kweli au lah?
Moja kwa Moja naenda kuutafuta huo mkitabu nianze kufaidi mafini yaliyomo
 
Nimecheka sana 😂😂😂
 
Nasikia watu wakijinadi kuwa kuna dawa za kurudisha mke/mme aliyekuacha ili hali bado unampenda? Wenye ushuhuda na hii mambo lete mrejesho hapa.
 
Ni kazi bure tu mkuu, kumbuka kuna sababu kwanini mliachana mwanzo. Sikushauri utafute suluhu ya mahusiano ambayo yameshavunjika.

Ni kama vile ujaribu kumfufua mtu ambaye amekwisha kufa.
 
Nasikia watu wakijinadi kuwa kuna dawa za kurudisha mke/mme aliyekuacha ili hali bado unampenda? Wenye ushuhuda na hii mambo lete mrejesho hapa.
Sema tatizo lako tukushauri
Usitafute msaada kwa shetty
 
Angalia chanzo cha tatizo lilofanya muachane rekebisha na aone kabisa umejirekebisa. Atarudi. Asiporudi basi huyo hakupangwa kua wako.

Kama tatizo liliosababisha muachane ni yeye, mpotezee. Kwanini umng'ang'anie mtu ambae amekukosea na hajutii kosa lake? Kuna wakati acha nature ifanye maamuzi and learn to let go.

NB: Nipo getto hapa nasikiliza ngoma ya Marioo - Inatosha[emoji445][emoji445][emoji445]
 
Kimbisa kwa ID mpya pole kwa haya unayopitia lakini yangu ni haya

Zipe muda hisia zako zipumzike.. Nothing last forever.. We are living in the very impermanence world.. Sisi wa jana sio sisi wa leo na hatutakuwa wa kesho.. Its just a realm of eternity in the repeated circle!
Najua maumivu ya hisia za mapenzi yalivyo.. Moyo unakuuma mpaka unatamani uung'oe au uutapike! Kichwa kinapasua mpaka unatamani ukifunge kamba, ukisikia YOU STOLE MY HEART AND FEELINGS ndio hii sasa! Kila unachokiwaza unamuona yeye, si harufu, si rangi, si chakula nknk.. Na kila simu ikiita ama msg ikiingia unatamani awe yeye! Mlango ukigongwa unatamani ukifungua ukutane na sura yake
We truly love only once in lifetime! Na hakuna kitu kibaya kama love at first site! Yanatesa sana haya mapenzi LAKINI
Huyu unayeteseka juu yake hana hisia tena na wewe! Hisia zina roho huja na kuondoka, huzaliwa hukua na hatimaye hufa! Kama kuna mganga ama mchawi aliwahi kufufua mfu basi watakuwepo wenye uwezo wa kurudisha hisia zilizokufa
Usidanganyike kuambiwa kuna tiba ya kumrudisha mpenzi ambaye hisia zake kwako hazipo tena zimekufa kifo cha asili! HAKUNA! Out of frustrations utakutana na madalali wa ulozi na kukushuhudia kwwmba hili linawezekana na watakupeleka kwa wataalam waliokwisha kuwapanga! Huko utaliwa pesa na kupewa matumaini hewa ili kuvuta muda ukate tamaa
Kuna mazingira ya kufanya akarudi kama umeporwa kwa nguvu ya juju, lakini kama ni natural death SAHAU!

Ni lazima utafakari ulikotoka ulipo na uendako.. Hasa kesho yako ni muhimu kuliko hisia zilizojeruhiwa
Hakuwepo kwako kabla, halafu akaja kwako akakuteka mazima kishapo akaondoka.. Usiumie sana kwakuwa hakumaanisha kuwa wako milele.. Kuna hiki kipindi cha maumivu makali na kumhitaji sana

Acha uumie kadiri iwezekanavyo ili uchungu na nguvu ya maumivu viishe! Usijaribu kuyakimbia ama kuyazuia maumivu kwa hali yoyote ile maana unaweza kujidhuru.. Kikubwa ni kuilinda afya yako kwakuwa nje ya yeye kuna wengine bado wanakupenda na kukuhitaji sana

Only time can heal broken heart.. Muda pekee ndio tiba ya hisia za mapenzi zilizoumizwa na kujeruhiwa kabisa.. Jitahidi sana majeraha hayo yasije kuleta kifo ama ulemavu MTUMAINIE MUNGU WAKO WAGANGA WATAKUPOTOSHA NA WENGINE WATAKUPOTEZA

Nakuombea upite salama kipindi hiki na mwakani tukipewa kibali cha uzima na afya tukutane tena kwenye hii mada

 
Pole sana hamna haja ya kutafuta Dawa ya kumrudisha kuwa busy na mambo yako utamsahau na maisha yataendelea kama kawaida.
 
Unamshauri mwenzako kwa vitu vilivyokutokea wewe. Kama mwenzio alitikisa kiberiti ili ajue kama anapendwa ni yeye, sio wengine
 
Potezea bwana. Mbona hata mimi aliniacha nikawa nampigia simu hapokei hata leo hii nikipiga simu hapokei ila nmeshakubaliana na hali na nina tamba tu. Kubembeleza ndiyo nilishagashindwa
 
Bro nitafute pm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…