Habari wana JF! mimi si member mpya katika kijiwe chetu pendwa ila nimeweka ID mpya sababu ya kulinda kujulikana ni nani maana wengi wananifahamu ID yng humu JF
Jamani wakuu naombeni msaada tumekwazana na mpenzi wangu km yalivyo mapenzi ila amebadilika ghafla yaani ninavyosema ghafla namaanisha maana hakuaga na hanaga tabia km hizi alizonazo kuna muda anabadilika mara anakaa sawa...nimekaa nae chini kiupole sana kumuuliza tatizo ni nini hana cha maana anachojibu yaani kiufupi amekua haeleweki kibaya zaidi ananiambia tuachane....yawezekana na sound km mjinga ila kiukweli moyo wangu unakataa kabisa kabisa kumuacha aende tumekua kwenye mahusiano kwa muda mrefu tumefanya vingi hii haki imenifanya siwezi kabisa kumsahau nimejitahidi nashindwa.
Nalala usiku naweweseka...nashindwa kula kabisa imefikia hatua kichwa kinauma upande mmoja naenda hospitali jupima nikidhani ni ugonjwa daktari akaniambia nina msongo wa mawazo(depression) nimejaribu sana kufanya uchunguzi kujua labda huyu mwenza wangu kapata mtu mwingine kwa uchunguzi wa awali kwenye simu yake kwa siri sijapata baya lolote na kwa nje hivi pia sijasikia loloteo nimehama hadi mazingira niliokua naishi nae lakini wapi hali inasidi kua mbaya kiupande wangu! Kichwa hakiachi kuniuma...nashindwa kula kulala yaani kuna muda natamani kua km watu wengine wenye furaha ila kwangu ni tofauti nimejaribu kubadili mazingira...kukaa na watu lakini haijasaidia! Nimepiga magoti nimeomba mno lakini wapi..
Sitegemei mtu anijudge ila kiukweli nilipofikia nimesikia mengi kuhusu mambo ya wataalamu(mafundi) au waganga wa kienyeji kama kuna mtu ambae aliwahi kusaidiwa au anamfahamu mtu aliewahi kusaidiwa jamani anisaidie PM au kwenye comment mi ntamfata PM kwa details zaidi maana natamani hadi kufa wakuu!
Haya mambo yapo na hayajaanza jana wala leo jamani namuhitaji sana bado mpenz wangu nashindwa ht kuendesha vzr shughuli zng za kila siku sababu ya maumivu niliyonayo moyoni mwenye msaada anisaidie natamani arudi tena kwangu maisha yaendelee km kawaida
Nawaombeni sana[emoji1431][emoji24]
Kimbisa kwa ID mpya pole kwa haya unayopitia lakini yangu ni haya
Zipe muda hisia zako zipumzike.. Nothing last forever.. We are living in the very impermanence world.. Sisi wa jana sio sisi wa leo na hatutakuwa wa kesho.. Its just a realm of eternity in the repeated circle!
Najua maumivu ya hisia za mapenzi yalivyo.. Moyo unakuuma mpaka unatamani uung'oe au uutapike! Kichwa kinapasua mpaka unatamani ukifunge kamba, ukisikia YOU STOLE MY HEART AND FEELINGS ndio hii sasa! Kila unachokiwaza unamuona yeye, si harufu, si rangi, si chakula nknk.. Na kila simu ikiita ama msg ikiingia unatamani awe yeye! Mlango ukigongwa unatamani ukifungua ukutane na sura yake
We truly love only once in lifetime! Na hakuna kitu kibaya kama love at first site! Yanatesa sana haya mapenzi LAKINI
Huyu unayeteseka juu yake hana hisia tena na wewe! Hisia zina roho huja na kuondoka, huzaliwa hukua na hatimaye hufa! Kama kuna mganga ama mchawi aliwahi kufufua mfu basi watakuwepo wenye uwezo wa kurudisha hisia zilizokufa
Usidanganyike kuambiwa kuna tiba ya kumrudisha mpenzi ambaye hisia zake kwako hazipo tena zimekufa kifo cha asili! HAKUNA! Out of frustrations utakutana na madalali wa ulozi na kukushuhudia kwwmba hili linawezekana na watakupeleka kwa wataalam waliokwisha kuwapanga! Huko utaliwa pesa na kupewa matumaini hewa ili kuvuta muda ukate tamaa
Kuna mazingira ya kufanya akarudi kama umeporwa kwa nguvu ya juju, lakini kama ni natural death SAHAU!
Ni lazima utafakari ulikotoka ulipo na uendako.. Hasa kesho yako ni muhimu kuliko hisia zilizojeruhiwa
Hakuwepo kwako kabla, halafu akaja kwako akakuteka mazima kishapo akaondoka.. Usiumie sana kwakuwa hakumaanisha kuwa wako milele.. Kuna hiki kipindi cha maumivu makali na kumhitaji sana
Acha uumie kadiri iwezekanavyo ili uchungu na nguvu ya maumivu viishe! Usijaribu kuyakimbia ama kuyazuia maumivu kwa hali yoyote ile maana unaweza kujidhuru.. Kikubwa ni kuilinda afya yako kwakuwa nje ya yeye kuna wengine bado wanakupenda na kukuhitaji sana
Only time can heal broken heart.. Muda pekee ndio tiba ya hisia za mapenzi zilizoumizwa na kujeruhiwa kabisa.. Jitahidi sana majeraha hayo yasije kuleta kifo ama ulemavu MTUMAINIE MUNGU WAKO WAGANGA WATAKUPOTOSHA NA WENGINE WATAKUPOTEZA
Nakuombea upite salama kipindi hiki na mwakani tukipewa kibali cha uzima na afya tukutane tena kwenye hii mada