Dawa ya wadudu wanaokula mbao ni ipi?

Dawa ya wadudu wanaokula mbao ni ipi?

Kanunue oil chafu .....nenda kapake vizuri kabisa wakirudia tena Kula hapo kuna mkono WA MTU........kwenye vile vitobo vyao imimine kabisa utakuja kureta mrejesho........maana kuna fundi aliwai kuniingiza chaka kwenye gypsum nikaweka ambazo sio treated ,mbona zoezi lilifanyika mpaka wakaacha kutafuna maaana nilipaka oil Kira weekend siendi popote nipo nao tunaoneshana mahaba Niue .......SASA hivi kimyaaa sijui kafa kiongozi wao........maana wakitafuna hata kidogo Tu napaka Kira sehemu narudia rudia ......mpaka SASA hivi kimyaaaaaa....hakuna anayethubutu
 
Itakuwa kamanda wao anaumwa akipona atarud Tena mpambane hao wadudu n wabishi sana

Binafsi napambana na mchwa mkuu Hawa wanataka kunilaza nje kabisa wameshusha gypsum chumba Cha watoto

Msaada wa dawa Kama unaijua

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Twiga gama 20000 1ltrs hiyo hata ukichimba mtaro wa urefu wa 1ft kwenye mzunguko wa eneo/kiwanja unanyunyizia huko kwenye mtaro alafu unafukia fasta(ili harufu ibaki ardhini) hutakaa uone mchwa eneo lako
 
Itakuwa kamanda wao anaumwa akipona atarud Tena mpambane hao wadudu n wabishi sana

Binafsi napambana na mchwa mkuu Hawa wanataka kunilaza nje kabisa wameshusha gypsum chumba Cha watoto

Msaada wa dawa Kama unaijua

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Mimi nimekwambia paka oil chafu Tu.......yaani Yale mafunza yanayo Kura mbao ukiyaona uwezi amini Lina Meno meusi mbele lakini mbao haichezi kwake .....SASA hivi sisikii chochote kimyaaaa
 
bora.jpg

Katika kufanya utafiti mitandaoni hii kitu ndio inaonekana kufaa, Tatizo sijui kama TZ inpatikana
 
Wallah kama leo ningepata mgeni ningejua ni wewe.
Mimi najua ndo mchwa kumbe si hao, wakianza kula utafkiri wanasaga mahindi mashineni yaani hao wadudu ni noma, wanapiga kelele sana ,chumba kimoja wametafuna mbao mpaka wameangusha gypsum, chumba kingine mlango wa chooni ukiugonga hivi unatoka unga unga na ni mwepesi sana na umeshatoka, chumba kingine mlango umeliwa sehemu ya kati.
Nasubiri dawa na mie.
Uo mlango upake diesel wote na unaweza ukaimix na mafuta ya taa utasaau kabla awajaumaliza

Sent from my TECNO LB6 using JamiiForums mobile app
 
Maji ya moto sana mwagia kwenye mbao yenye mdudu, hutaona tena, rudia baada ya mwezi mmoja, hutawaona tena, iwe mdudu wa mbao au hata Kunguni, papasi maji ya moto kabisa ndio dawa yao ya milele, kisha kausha godoro au mbao juani.

Chemsha maji lita 15 au 20 yakichemka kabisa, anza kuchota unamwagia kwenye mbao za kitanda, au godoro au coach, watakufa wote kabisa, alafu weka juani, fanya kazi hii mapema saa 2 hv asubuhi ili uanike juani.
Wadudu wako juu ya dari kwenye mbao zilizopaulia nyumba hayo maji ya moto unayamwagaje bila kuathiri gypsum boards?
 
Wallah kama leo ningepata mgeni ningejua ni wewe.
Mimi najua ndo mchwa kumbe si hao, wakianza kula utafkiri wanasaga mahindi mashineni yaani hao wadudu ni noma, wanapiga kelele sana ,chumba kimoja wametafuna mbao mpaka wameangusha gypsum, chumba kingine mlango wa chooni ukiugonga hivi unatoka unga unga na ni mwepesi sana na umeshatoka, chumba kingine mlango umeliwa sehemu ya kati.
Nasubiri dawa na mie.
Wakimaliza mbao wataanza kukula na wewe
 
Salaam,

Kichwa cha habari cha husika, nilinunua mbao nikaezeka na nishafunga gypsum lakini kuna wadudu wanapekecha mbao usiku ni kelele.

Naombeni msaada ni dawa gani ninunue nipande juu nikaspray maana vifaa ninavyo.
Ingia gharama nunua oil chafu tafuta kijana au wewe mwenyewe hiyo Kaz ufanye kupaka oil chafu mbao zote juu na Nina uhakika itakuwa mwisho hakikisha tu mbao inanyonya oil nyingi wakat wa kupaka na kama Kuna matundu yaliyo Anza kutoboloewa tumia kikopo Cha mafuta ya cherehani kuweka oil chafu na nyunyizia kwenye hayo maeneo ya tobo ili oil ikafikia wadudu

Jitahid upake muda wa asubuhi Sana au jion wakat jua limepoa maana darini huwa Kuna joto

Kingine Zingatia wakati unapanda juu usichafue tu gypsum hakikisha kila hatua unaweka kitu ili kuzuia oil isije kumwagia kwa Wingi juu ya gypsum na kuharibu
 
Mimi nimekwambia paka oil chafu Tu.......yaani Yale mafunza yanayo Kura mbao ukiyaona uwezi amini Lina Meno meusi mbele lakini mbao haichezi kwake .....SASA hivi sisikii chochote kimyaaaa
Atumie hii hii kwel
 
Mdudu anaetafuna mbao na kutoa milio kama msumeno unakata mbao badae unakuta mbao zinayoa unga ni mdudu hatari sana jamii ya mende wa mbao. Mdudu huyu hutaga mayai yake kwenye nyuso za mbao, mayai yake huwezi kuyagundua kwani yana asili ya maji maji. Baada ya hapo mayai huzama ndani ya mbao nakubadilika kupitia hatua za ukuaji za mdudu(insects)akiwa katika hatua ya lava hapa anakua kama mnyoo na meno mawili makubwa magumu sana kama yale ya mchwa hapa ndio wanaanza kushambulia mbao wakiwa ndani na huwezi kuona tundu walipoingia maana waliingia katika hali ya majimaji.
Hatua hii ndio hatari zaidi kwani ndio hatua ambayo mdudu huyu hula hivyo kufanya uharibifu mkubwa wa mbao zako iwe ni furniture au dari ya nyumba yao Italian na kua kama mabua tu kwani utakuta mbao zinavunjika na kumwaga unga wa njano. Baadae mnyoo hugeuka hatua za mwisho na kua mdudu kamili hapo sasa hutoka nje kama mdudu kamili na ndipo utaona tundu lake alipotoka ila hatua hii uharibifu utakua umekamilika. Akishatoka kama ni jike ataanza kutaga mayai tena upya na kurudia mzunguko uleule.

Kwanini wanakula mbao?
Wadudu hawa wanakula mbao ambazo 1.hazina dawa
2Hazijakomaa(laini)
3.Hazijakauka vizuri
Wauzaji wengi wa mbao sikuhizi sio waaminifu watakwambia mbao zina dawa kumbe wamezipaka maji ya rangi kupunguza gharama au kama wameweka dawa warakua wamezichovya tu juu juu ili kuziwahisha sokoni hawana muda wakupika maelefu ya mbao kwenye maji yanayo chemka dawa. Hivyo wengi huchimba shimo na kuweka dawa kidogo bila kufatauwiano wa dawa na maji na kisha wanachukua mbao moja moja wanafanya kuichovya na kutoa kama wanabatiza vile. Hivyo sio rahizi kumzuia mdudu huyo anaekula kuanzia ndani ya mbao.

Namna ya kumdhibiti mdudu huyu
Kama ilivyo kwa wadudu wengi ngozi yao imetengenezwa kwa matirio isiyoweza kuhimili baadhi ya kemikali ndio maana ukimwagia nyoka mafuta ya taa ataanza kuchubuka chubuka.
Hivyo mafuta jamii ya petrol yanasaidia sana kuangamiza wadudu hawa yaani
Petrol, diesel, .mafuta ya taa na hata oil chafu.

Njia ya kutumia mafuta ya taa ikichanganywa na turpentine kwa uwiano maalumu ni nzuri.
Angalizo: baadhi ya mafuta ni hatari kwani yanasapoti uwakaji wa moto pia
Na baadhi ya mafuta yanaharufu kali hasa unapopata ndani ya nyumba yako na mengine yana haribu rangi ya mbao na samani ndani ya nyumba yako kama yatadondokea. Japo unaweza kutumia kumdhibiti mdudu huyu wakutafuna mbao

Dawa nduzi ambayo nimeitumia kwa nyumba kadhaa zenye shida hizi na hata kwenye furniture zenye wadudu hawa au kuzilinda zilizobaki zisishambuliwe tena na wadudu hawa ni dawa zenye kiambata sumu cha pareto hapo utakua umemshinda kabisa mdudu huyu na utafurahia nyumba na furniture zako

:Kumbuka si kila dawa ya kuua mdudu inaweza kuwaangamiza wadudu hawa

Kama hujapata utatuzi na ungependa kuwasiliana nasi tutafute kwa simu/whatsapp 0717 040 837 . Engineer Mkuuu
 
Back
Top Bottom