Dawa ya wadudu wanaokula mbao ni ipi?

Dawa ya wadudu wanaokula mbao ni ipi?

Kuna jamaa aliniuzia kitanda pale mpakani, wale wanouza vitanda pale mpakani,
Sasa nimekaa nako mwaka sasa ndio nasikia hizo kelele, nikamuliza akaniambia niende kwenye duka la hardware niulizie dawa inaitwa dudu killer nafikiri.
Nitaenda itafuta nitawapa mrejesho.
 
Habari wana JF
Nimetoka kumtembelea ndugu yangu kwa bahati mbaya dari lake lina shambuliwa na mdudu ambaye anapiga kelele kama msumeno. Nilishtuka kidogo na huyo mdudu naambiwa anachoronga mbao within short time unakuta unga unga hivi. Je dawa ya huyo mdudu ni ipi, tafadhali hili ni jambo la kufa na kupona.
Ampulizie Rungu, ile dawa ya mbu, au brand nyingine yoyote ya spray inayoua wadudu ili mradi iwe ni ile kali
 
Kuna jamaa aliniuzia kitanda pale mpakani, wale wanouza vitanda pale mpakani,
Sasa nimekaa nako mwaka sasa ndio nasikia hizo kelele, nikamuliza akaniambia niende kwenye duka la hardware niulizie dawa inaitwa dudu killer nafikiri.
Nitaenda itafuta nitawapa mrejesho.
Dudu killer haiwezi saidia kama ni wale wanaopenya bila kutoboa mbao.
 
Si kweli, wakishaingia ndani ya mbao hakuna unachoweza fanya. Labda utoe mbao kama mdau alivyosema hapo. Mimi nimejaribu diesel lakini wapo hai wanapiga mzigo.
Hawa wadudu ni baraa wanaouwezo wa kula paa lote la nyumba, utakachosikia ni pale wakikwangua ubao kwa ndani na kutoa unga waliotafuna!!! Wanashambulia mbao changa na all softwoods!!!
 
Nununua mbao zilizopakwa dawa, ila milango na fremu jitahidi uweke mninga .
 
Kuna mwana jf alitoa solution 2017.
Screenshot_20210909-205012.jpg
 
Ipi kiongozi itasaidia?
Mimi mpaka leo nmekosa siluhisho nimeuza tu baadhi ya furniture nikanunua mpya. Kwa sababu nyumba ni ya kupanga wa kwenye dali atadili nao mwenye nyumba mimi nitahama.
 
Hawa wadudu ni baraa wanaouwezo wa kula paa lote la nyumba, utakachosikia ni pale wakikwangua ubao kwa ndani na kutoa unga waliotafuna!!! Wanashambulia mbao changa na all softwoods!!!
Mninga hawali? Maana nilitengeneza kitanda cha mninga ila nimeanza kumsikia. Au anakula chaga?
 
Kuna yoyote aliyefanikiwa kuondoa wadudu wanaokula mbao darini maaní
 
Anafananaje? Kwa kingereza anaitwaje nimgoogle nimjue?
Kadudu flani kaajabu. Anafanana na mbao.

Kwa mbele kichwani kachongoka kama katapila. Siku alipishana na mimi kwenye paa nilishtuka sana japo ni mdogo.

Ni nadra sana kuonekana. Maisha yake ni ndani ya mbao. Akitoka ni dharura tu
 
Mtakuwa Mmejengea kwa Mbao za Kula... sasa Mdudu ataachaje Kula...

Wekeni Mininga au Milingoti hailiki even Mchwa wanavunja tu meno yao

Kwenye Matundu mule pulizia dawa ya Mbu kisha ziba vitundu kwa Chelewa au kijiti kigumu Mdudu hufia humo humo kila ukisia mlio Tafuta vitundu Pulizia spray ya Mbu Dudu Killer
ngja nkajalibu hii showcase yngu wanaishambulia sana nlishapulizia dawa y mbu ila ckusiba bdo wanaendelea tu
 
Back
Top Bottom