Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mtafte dudubaya A.K.A oil chafu(konki)
Habari wana JF
Nimetoka kumtembelea ndugu yangu kwa bahati mbaya dari lake lina shambuliwa na mdudu ambaye anapiga kelele kama msumeno. Nilishtuka kidogo na huyo mdudu naambiwa anachoronga mbao within short time unakuta unga unga hivi. Je dawa ya huyo mdudu ni ipi, tafadhali hili ni jambo la kufa na kupona.
Chota unga uza.Hili tatizo linawakumba wengi... Mbao za dari kuliwa na kudondosha unga. Nini tiba?
-Kaveli-
Bado MkuuMkuu, ulipata tiba ya hilo shambulio la wadudu kwenye mbao za dari?
-Kaveli-
mkuu vipi ulifanikiwa?Hili tatizo linawakumba wengi... Mbao za dari kuliwa na kudondosha unga. Nini tiba?
-Kaveli-
MhhNina Formular ya kukutengenezea Dawa Hii... Ni ya Uhakika ila Gharama Ni kubwa Ujiandae kwelikweli Dumu la Lita 20 Ni Tsh 120,000/- Haichanganywi na Maji Ni kupaka tuu. Karibu Inbox
Awa wadudu huwa wanatoka wapi mimi nawaskia kila kona ya nyumba kwenye masofa ndani na kwenye vitanda nawaskia miaka yote sijawahi pata hili tatizo limekuja ghafla ndani ni kelele kama misumeno inakatwaPaka oil chafu kwa wingi. Asipake kidogo. Then wataacha.
Kwangu ime work out. Japo nimeweka oil nyingi sana. Dawa wanazouza madukani kwangu ziligoma. It coasted me kama laki 2 kununua dawa wakatulia kwa mda mfupi then within short period wakarudia kuharibu.
But baada ya kuweka oil chafu nyingi mpaka ikavuka kwenye gipsum hatimaye wametulia. Jaribu na wewe
Kama unawaskia kwenye sofa ndani unatumia mbinu ipi?Pakaa diesel pia inasaidia inapenya ndani kenye huo unga, oil chafu ni nzuri lakini inapenya kidogo sana
Kwenye sofa ni mpaka ufumue uikute mbao mkuu haina janjaKama unawaskia kwenye sofa ndani unatumia mbinu ipi?
Awa wadudu wameingia na kwangu sijaelewa wametokea wapi nilikuta tu kabati ya vyombo inamwaga unga kwa sasa nawaskia kila kona kuanzia kwenye masofa mpaka nililala nawaskia wanakula kitanda cha ajabu nikitafuta siwaoniKuna waliosema Mafuta ya taa ama diesel... kuzipaka mbao huko darini. Hii ni tiba?
-Kaveli-
Duh aisee ni hatari...wanatokeaga wapi?Kwenye sofa ni mpaka ufumue uikute mbao mkuu haina janja
Sijui waliumbwa siku ya ngapi katika zile siku saba za kazi ya MunguDuh aisee ni hatari...wanatokeaga wapi?