Dawa za Kulevya: Freeman Mbowe akamatwa na Polisi; ahojiwa na kuachiwa

Huu upuuzi wa kukamata viongozi wa upinzani, unafikia Mwisho kwa kupitia Mbowe!

Hii nchi ingetakiwa isitawalike tena! Sema huu upole wa viongozi wa upinzani ndio unasababisha maelewano yanakuwa magumu!
 
Nina hakika na taarifa hii. Sijawahi kuleta habari ya uongo hapa
Lakini mkuu mbona vyombo vingine vya habari vimeripoti kuwa katiivsheria bila shuruti kaenda kuripoti kituo cha kati huko ostabay ndo nasikia kwako saa hivi
 
Kama Mbowe atakamatwa kwa kufanya biashara na R-1 awepp, kama ni kwa kutumia Ra- C na Chi B n.k. wakamatwe, kama ni kwa ajili ya kikataa kuripoti polisi na Mtoto wa Mkulima akamatwe
NADHANI AMEKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUTUMIA NA SI VINGINEVYO. BASI WASISAHAU KUMKAMATA NA MWANAMZIKI CHID BENZ.........!
 
Kama ni kweli basi Mbowe anajimaliza kisiasa, kwa nini ajifiche kama hana dosari?
Yaani unaamini kauli ya Lizaboni kuwa Mbowe amejificha! Hizo ni akili ndogo, Mbunge na kiongozi wa upinzani amejificha! Angetaka kukwepa angeenda kwenye Ubalozi wa nchi yoyote hapa Dar na wasingemkamata.

Za kuambiwa changanya na zako-JK.

Vv
 
Kama ni kweli basi Mbowe anajimaliza kisiasa, kwa nini ajifiche kama hana dosari?
unakaribia kuamini taarifa nyepesi sana zilizoletwa kinazi,hivi mbowe anaweza kuhama mafichoni hasa kama kweli ni maficho kirahisi rahisi hivyo?
 
Sumu itamwagika nyumban kwenu mfe nyie...ila watanzania kwa sasa tunaomba mvua tu inyeshe watu tuingie mashamban tuzalishe nyie wafia siasa kazi mnayo...wenye akili tunajua pumba na mchele hvo msitegemee kutudanganya tena upinzan ni ficho la wapigia debe tumbo
 


Kumbe [HASHTAG]#Mbowe[/HASHTAG] naye ni mwoga wa polisi? Sasa kama hajihusishi na madawa ya kulevya kwa nini aliogopa kwenda lock-up?
 
Mbowe hana tuhuma zozote,chuki za matajiri zinawasumbua sana utawala wa awamu ya tano lakini mwisho wa siku matatamani Dunia iapsuke mwingie ndani yake??

Mmefanya haya sababu ya kesi ya kesho ili muikimbie,na hamtaikimbia.
Tutajazana kesho tuone ataswekwa lupango au la
 
Kama kiongozi mkubwa kama mbowe haitikii wito wa vyombo vya usalama vya nchi akina sie tufanyeje.? Kwa hilo mbowe ni mfano mbaya katika jamii
.. Kama wito haujatolewa kwa kufuata taratibu why bother? Hivi umeshawahi kupewa samansi kwa TV?
 
Polisi gani waliomuita Mbowe?
 
Acha kupotosha umma mkuu. Wengi tumeiangalia hiyo taarifa ya ITV...hakuna sehemu ndugu mtangazaji alisema "Ameshushwa kwa Lazima na kupandishwa kwa lazima kwenye gari ya Polisi"...ukizingatia ITV wameripoti taarifa hii kwa weledi bila kuamsha hisia za upande wowote.
 
Acha kupotosha umma mkuu. Wengi tumeiangalia hiyo taarifa ya ITV...hakuna sehemu ndugu mtangazaji alisema "Ameshushwa kwa Lazima na kupandishwa kwa lazima kwenye gari ya Polisi"
Weka walisemaje! Maana video zipo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…