M-mbabe
JF-Expert Member
- Oct 29, 2009
- 13,203
- 23,027
Taarifa nilizopata kutoka kwenye chanzo changu cha kuaminika ni kwamba, Mwenyekiti wa CHADEMA, FREEMAN MBOWE ametiwa nguvuni na Jeshi la Polisi baada ya jitihada za kukimbia na kujificha kushindikana.
Mbowe amekamatwa maeneo ya Mikocheni ambako alienda kujificha ili asikamatwe na Jeshi la Polisi.
Kwa sasa wapo njiani kuelekea Central ambako atahojiwa kutokana na tuhuma za kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya pamoja na kulisababishia usumbufu na gharama jeshi la polisi.
Taarifa zaidi zinasema kuwa Mbowe amekamatwa akitolewa kwenye Appartment Moja kwenda nyingine akitumia gari Nyeusi, Tinted yenye namba za usajili T 830 DEW aina ya VX. Wamemkamata akiwa nje ya geti ya Appartment hiyo ambayo ni miongoni mwa majengo ya siri ( Safe House) yanayomilikiwa na CHADEMA
unless my brain is playing me up, nimeona na kusikia kwenye taarifa ya habari saa 2 usiku huu ITV wamesema Mbowe amekutana na mapolisi njiani wakati akielekea mwenyewe kituoni. baadae wakarudi naye nyumbani kumpekua - huyu mleta thread hii ni dhahiri kaanzia story yake ya "kukamatwa Mbowe" walipomaliza kumpekua.
mods tafadhali ondoeni hii distortion ya kwenye hii thread.