MDANGANYIKAJI
Member
- Jan 27, 2011
- 77
- 59
Mbowe ameachiwa saa 7 na dk 20 usiku, asubuhi hii saa 3 anaelekea mahakamani kumfungulia kesi Makonda
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Amedhalilishwa sana na udhalimu huu aliofanyiwa malipo ni hapa hapa. Time will tell!Sawa nimekuelewa lakini amedhalilishwa
Ameeeeeeen tunamshukuru sana mwenyezi mungu kumsimamia mwenyekiti wetuNa Tundu Lissu usiku huu:
Waheshimiwa habari za usiku huu. Naomba kutoa updates juu ya kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chama Mh. Freeman Mbowe. Mimi na Katibu Mkuu Dkt. Vincent Mashinji tumeshuhudia sehemu ya sachi iliyofanyika nyumbani kwa Mwenyekiti kati ya saa tatu unusu na saa sita usiku huu. Kama nilivyosema kwenye ujumbe wangu wa awali, hii sio vita dhidi ya wafanya biashara ya madawa haramu bali ni vita ya kisiasa dhidi ya sisi wapinzani wa CCM na Rais Magufuli. Kwa uthibitisho wa kauli yangu naomba niwapatie orodha ya vitu walivyokamata polisi nyumbani kwa Mwenyekiti Mbowe. Vitu hivyo vimeorodheshwa kwenye fomu na. DCEA 003 inayoitwa 'Hati ya Ukamataji' iliyotolewa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kama ifuatavyo:
(1) Hati moja ya CHADEMA CHASO kwenda kwa Mwenyekiti ya tarehe 16/7/2013
(2) Picha mbali mbali nane za matukio ya uhalifu - picha za wahalifu wanaoharibu mali
(3) Hati moja ya Rasimu ya Kwanza ya CHADEMA kuhusu uundwaji wa Red Brigade
(4) Hati moja ya kurasa 13 inayoongelea mambo ya Muungano.
Hivi ndivyo vielelezo vilivyokamatwa nyumbani kwa Mwenyekiti vinavyothibitisha kwamba yeye ni muuza unga!!! Kama isingekuwa ukweli kwamba hivi ninavyoandika Mwenyekiti wangu yuko mahabusu Central, hiki kingekuwa kichekesho cha mwaka. Lakini Mwenyekiti anasota mahabusu usiku huu. Huu ndio ushahidi ambao Kamanda Sirro na polisi wake wamekuwa wanamtafutia Mwenyekiti wetu kwa amri ya Paul Makonda. Hatuna budi, katika hali hii, kuomboleza - kama alivyofanya Mwalimu katika kitabu chake 'Uongozi Wetu na Hatma ya Tanzania' - juu ya mahali ilikofikishwa nchi hii yetu. Nitawatumia picha ya orodha hiyo shortly.
Update: Mwenyekiti Mbowe aachiwa
Kama tulivyowajuza kwamba iwapo itatokea jambo lolote la umuhimu kujuzana kabla ya asubuhi tutafanya hivyo, tunapenda kuwatangazia wanachama wetu,wadau,wapenzi, na wapenda haki,amani na demokrasia ya kwamba Mwenyekiti Freeman Mbowe ameachiwa huru punde tu mnamo majira ya SAA saba na robo usiku huu.
Tunawashukuri wote kwa sala,maombi na subira na hivyo kuhitimisha salama SAA KUMI za Mwenyekiti wetu kuwa chini ya Jeshi la Polisi nchini katika kituo kikuu cha Polisi jijini Dar es salaam.
Taarifa za ziada juu ya jambo hili zitatolewa kesho.
Salum Mwalim
Naibu Katibu Mkuu
Chadema
Mkuu lengo ni kuwalaza gerezani katika kuwadhalilisha, kuwavunjia heshima hata kama kufanya hivyo ni kukiuka haki za msingi za binadamuFor what is worth regardless of one man's power kuna taasisi za 'human rights', Tanganyika Law Society and several home and international watchdogs watu awawezi kukaa kimya wakati infringement of 'civil liberty' is being promoted in the day broad light by the government agents.
Unamuita mtu kwa mahojiano tena na kumkamata kwa nguvu maana yake tayari unaushaidi wa awali; akifika huko ni wewe sasa umpe huo ushahidi wako yeye hana ulazima wakushirikiana na wewe kama yuko tayari kwenda mahakamani mfungulie kesi.
Kama hauna ushahidi wowote let the person walk free na surely wanasheria wao wanatakiwa walipazie sauti hili swala pamoja na taasisi zingine za kisheria kuendelea hivi ni kuwajengea fikra za kwamba nchi aina sheria.
Huyu ni kiongozi wa kitaifa sisi wengine itakuwaje kama polisi wanaanza tabia hizi mapema hivi wakati kila mtu anaona hii sio sahihi.
Mmmmmmh!! Umesahau yale MAAGIZO eeeh? Yale ya WAPIGA DEKI GARI na WAIMBA MAPAMBIO eeeh?Wameogopa mafuriko ya wana CHADEMA ambao wangejaa leo kisutu na bendera zao .SIASA INATUFANYA TUJADILI MATUKIO
Katika post yote hiyo wewe ulichoona ni "kunyanyaswa" tu? Hujaona "kuachiwa?"Wapinzani kunyanyaswa ni good news hebu fafanua
Makondakta atahukumiwa kwa huu mkasa mzimaTunasafari ndefu ya kupambana na vita ya madawa ya kulevya.Naomba serekali iache siasa kwenye jambo hili na ijikite kwenye dhamira ya kweli ya kupambana na vita ya ukweli ya madawa ya kulevya.
OK nimekuelewa mkuu nilidhani uvccmKatika post yote hiyo wewe ulichoona ni "kunyanyaswa" tu? Hujaona "kuachiwa?"
Kwa wao huo ni bonge la ushahidiOoh good news kwa CHADEMA. Kwa hiyo alificha ushahidi huo uliokamatwa.
Cc:LizaboniKwa style hii ya kunyanyasa wapinzani...
Nchi inatarajia kupata Viwanda vingi sana.
Ccm hukumu yenu ipo kwa mwenyezi munguKatika post yote hiyo wewe ulichoona ni "kunyanyaswa" tu? Hujaona "kuachiwa?"
Unadhani huyo Katibu atamwaga mchele humu??Kwa hiyo hizo nyaraka ndio vielelezo vya madawa ya kulevya? Hii ni aibu ya mwaka kwa watawala hawa waliopo. JK na wastaafu wengine toeni semina elekezi jinsi ya kurun nchi