Dawa za Kulevya: Freeman Mbowe akamatwa na Polisi; ahojiwa na kuachiwa

Dawa za Kulevya: Freeman Mbowe akamatwa na Polisi; ahojiwa na kuachiwa

Kuizushia CHADEMA na viongozi wake uzushi wa uzito wowote (eg wa tani 10) sio kosa nchini mwetu na dola itakulinda ila kusema ukweli mchungu dhidi ya CCM au serikali hii au kuizushia uzushi au uongo japo wa kilo 5 CCM au serikali hii ni kosa kubwa saaaaana kwa dola na watatumia resources zao zoooote kukusaka
 
Na Tundu Lissu usiku huu:

Waheshimiwa habari za usiku huu. Naomba kutoa updates juu ya kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chama Mh. Freeman Mbowe. Mimi na Katibu Mkuu Dkt. Vincent Mashinji tumeshuhudia sehemu ya sachi iliyofanyika nyumbani kwa Mwenyekiti kati ya saa tatu unusu na saa sita usiku huu. Kama nilivyosema kwenye ujumbe wangu wa awali, hii sio vita dhidi ya wafanya biashara ya madawa haramu bali ni vita ya kisiasa dhidi ya sisi wapinzani wa CCM na Rais Magufuli. Kwa uthibitisho wa kauli yangu naomba niwapatie orodha ya vitu walivyokamata polisi nyumbani kwa Mwenyekiti Mbowe. Vitu hivyo vimeorodheshwa kwenye fomu na. DCEA 003 inayoitwa 'Hati ya Ukamataji' iliyotolewa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kama ifuatavyo:
(1) Hati moja ya CHADEMA CHASO kwenda kwa Mwenyekiti ya tarehe 16/7/2013
(2) Picha mbali mbali nane za matukio ya uhalifu - picha za wahalifu wanaoharibu mali
(3) Hati moja ya Rasimu ya Kwanza ya CHADEMA kuhusu uundwaji wa Red Brigade
(4) Hati moja ya kurasa 13 inayoongelea mambo ya Muungano.

Hivi ndivyo vielelezo vilivyokamatwa nyumbani kwa Mwenyekiti vinavyothibitisha kwamba yeye ni muuza unga!!! Kama isingekuwa ukweli kwamba hivi ninavyoandika Mwenyekiti wangu yuko mahabusu Central, hiki kingekuwa kichekesho cha mwaka. Lakini Mwenyekiti anasota mahabusu usiku huu. Huu ndio ushahidi ambao Kamanda Sirro na polisi wake wamekuwa wanamtafutia Mwenyekiti wetu kwa amri ya Paul Makonda. Hatuna budi, katika hali hii, kuomboleza - kama alivyofanya Mwalimu katika kitabu chake 'Uongozi Wetu na Hatma ya Tanzania' - juu ya mahali ilikofikishwa nchi hii yetu. Nitawatumia picha ya orodha hiyo shortly.

Update: Mwenyekiti Mbowe aachiwa

Kama tulivyowajuza kwamba iwapo itatokea jambo lolote la umuhimu kujuzana kabla ya asubuhi tutafanya hivyo, tunapenda kuwatangazia wanachama wetu,wadau,wapenzi, na wapenda haki,amani na demokrasia ya kwamba Mwenyekiti Freeman Mbowe ameachiwa huru punde tu mnamo majira ya SAA saba na robo usiku huu.

Tunawashukuri wote kwa sala,maombi na subira na hivyo kuhitimisha salama SAA KUMI za Mwenyekiti wetu kuwa chini ya Jeshi la Polisi nchini katika kituo kikuu cha Polisi jijini Dar es salaam.

Taarifa za ziada juu ya jambo hili zitatolewa kesho.

Salum Mwalim
Naibu Katibu Mkuu
Chadema
Ameeeeeeen tunamshukuru sana mwenyezi mungu kumsimamia mwenyekiti wetu
 
For what is worth regardless of one man's power kuna taasisi za 'human rights', Tanganyika Law Society and several home and international watchdogs watu awawezi kukaa kimya wakati infringement of 'civil liberty' is being promoted in the day broad light by the government agents.

Unamuita mtu kwa mahojiano tena na kumkamata kwa nguvu maana yake tayari unaushaidi wa awali; akifika huko ni wewe sasa umpe huo ushahidi wako yeye hana ulazima wakushirikiana na wewe kama yuko tayari kwenda mahakamani mfungulie kesi.

Kama hauna ushahidi wowote let the person walk free na surely wanasheria wao wanatakiwa walipazie sauti hili swala pamoja na taasisi zingine za kisheria kuendelea hivi ni kuwajengea fikra za kwamba nchi aina sheria.

Huyu ni kiongozi wa kitaifa sisi wengine itakuwaje kama polisi wanaanza tabia hizi mapema hivi wakati kila mtu anaona hii sio sahihi.
Mkuu lengo ni kuwalaza gerezani katika kuwadhalilisha, kuwavunjia heshima hata kama kufanya hivyo ni kukiuka haki za msingi za binadamu

Tulisikia mawakili wakionywa kuwa nao 'wawekwe' mahabusu. Kwa maana kuwa hakuna tena haki ila haki ni ile inayotolewa na watu kwa matakwa yao

Swala la Mbowe lina sura inayotisha ingawa wengi hawawezi kuona tatizo
Hatuongelei kama anahusika au hahusiki, tunaongelea mazingira ya siku nyingi

1. Alitafutwa kupitia Bilicana
2. Akafuatwa na Hotel zake

Ukitazama kwa umakini kuna 'political motivations' huwezi kuwaambia watu wasiamini

Tayari kuna dots watu wanaunganisha tu. Iwe kweli au si kweli wapo wanaoamini hivyo

Kinachoendelea nchini ni kitu cha hatari sana. Hivi kwanini Polisi waende kwenye TV kutangaza wanamtafuta Mbowe.

Yaani wakipewa habari za Jambazi Nyangumi wataenda kumtaka ajisalimishe kupitia TV!

Kitendo kile tu cha Polisi kukomalia kinashaka isiyo na shaka.

Pili, Polisi wanaweza kujua alipojificha Mbowe, hawawezi kuhakiki jina walilopewa kama lina usahihi. Hapa kuna nini?

Halafu kwanini Watangaze wasiende kukusanya ushahidi na kumfikisha mahakamani?

Hivi kama kuna kitu si ameshakificha, kazi ya Polisi itakuwa nini kama hawana ushahidi

Haya tumeona matokeo yake katika nchi za wenzetu. Gambia Rais amelezimika kuondoka

Zimbwabwe mzee yupo madarakani kuliko kaburu yoyote yule aliyewahi kutawala

Mugabe na Jameh wanatishwa na siasa walizofanya huko nyuma, siasa za visasi.

Tunazidi kugawanyika na kupoteza misingi yetu ya umoja, utu na upendo

Leo Tanzania inakuwa Taifa la wananchi wanaoishi kwa kutoaminiana, hofu na kihoro

Taifa limegawanyika, misingi iliyotuweka pamoja inabomoka.

Nani ajueaye kesho itakuja na ni?
 
Tunasafari ndefu ya kupambana na vita ya madawa ya kulevya.Naomba serekali iache siasa kwenye jambo hili na ijikite kwenye dhamira ya kweli ya kupambana na vita ya ukweli ya madawa ya kulevya.
Makondakta atahukumiwa kwa huu mkasa mzima
 
22625191e64de45afd858a9b6c9a7260.jpg
 
Nahamu sana kusikia figure za fidia... Nenda Mbowe, haiwezekani mtu mwenye umri sawa na mwanao akuvue nguo.
 
I wish to be IGP huku IGP ni Junior wako duh! Next episode loading .........
Viva Mbowe mnafiki huumbuka mchana kweupe.
 
Kwa hiyo hizo nyaraka ndio vielelezo vya madawa ya kulevya? Hii ni aibu ya mwaka kwa watawala hawa waliopo. JK na wastaafu wengine toeni semina elekezi jinsi ya kurun nchi
Unadhani huyo Katibu atamwaga mchele humu??
 
Back
Top Bottom