Ni ukweli unaamini hii vita itafanikiwa kwa kupoteza muda na Wema?? ..
Hivi usalama wa taifa na polisi wanafanya kazi gani kushindwa kuipa serikali information mpaka tunahangaika na hawa akina Wema,??
Siamini kama Wema anaweza kutusaidia kukomesha madawa ya kulevya Tanzania, kama wewe ni mfuatiliaji wa JF utaelewa kwa nini nina wasiwasi na hii vita ilipoanzia....Kuna zile barua zilichapwa sana humu JF za wafungwa walioko China na zimetaja majina ya matajiri wa hao Mapunda sasa nashangaa tunapomfuata Wema ambaye sikuwahi kuona mahali popote akitajwa na kuwaacha hao ambao kila siku hutajwa na mpaka wengine kutumikia vifungo nchi za nje kwa makosa ya madawa..Intelejensia yetu inafanya kazi gani???
Ninaelewa taifa limevamiwa na shetani la madawa ya kulevya tangu enzi za raisi Mwinyi. Wakati wa Mkapa hali kidogo ikawa nafuu na kwa awamu ya nne ndiyo kabisa biashara ikawa kama imehalalishwa. Sasa Mheshimiwa raisi Magufuli anauchungu na uharibifu mwingi uliofanyika kule nyuma. Anatumia kial nyenzo aionayo inaweza kutumika.
Tatizo hawafahamu watendaji wake. Anapaswa kuwafahamu hasa waliokuwa awamu ya nne. Sasa hivi wanakimbila agenda na media kemkem ili wajitangaze, waonekana na mkuu , kisha waziharibu agenda ili zifanyike wanavyotaka wao huku wakijilinda na kuwalinda waharifu.
Katka vita hii ya madawa siwezi kusema Wema na hao wa aina yao hawahusiki. La hasha. Isipokuwa sina imani na dhamira ya Makonda, pamoja na mchakato mzima.
Kama dhamira yake ni njema, basi uwezo wake ni mdogo na hafai kushika hata nafasi aliyonayo. Hakuna kiongozi anayemaanisha ambaye atawatangaza watuhumiwa anaotaka kuwahoi kwenye vyombo vya habari kama si hekaya za Abunuasi. Ninashaka alikuwa anawapa nafasi ya kujiandaa wao pamoja na wakuu wao. Sioni kwa nii wasifanye mawasiliano usiku kwa usiku namna ya kupoteza mwelekeo wa zoezi zima kitu ambacho kiongozi lazima awe anakifahamu.
Usalama wa taifa wanafanya nini kama unavyosema ikiwa kesi kama hizi za kimatifa zinakuwa handled ki--ji--nga kijing namna hii kiasi cha kupoteza ushahidi na mwelekeo wote.
Kwa kuwa lengo halikuwa kukomesha biashara hii bali kuwalinda waharifu halisi, mwisho wa hii shamra shamra naiona ni kusema hakuna wafanya biashara wa madawa TZ, kama ambavyo mafisadi wamesafishwa, lakini hapo haopo watu wanajenga majina kwamba ni majasiri hata wamediriki kudeal n awafanya biashara wa madawa nchini!.
Ninaomba sana Mheshimiwa Raisi awafahamu watu wake kwamba wanachokifanya ni unafiki lakini wanamhujumu mwisho wa siku asiwe na kitu chochote kimefanikiwa katika hali endelevu.