Dawa za meno ambazo ni nzuri kwa ulinzi wa meno

Troll JF

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2015
Posts
7,804
Reaction score
12,237
Wakuu mimi binafsi natumia colget Advanced whitening kina ujazo wa 75mil si nyingi ila bei yake ni Tsh. 4,500 hii nzuri sana watoto wa Arusha utawakamata sana si unajua yale meno yao.

Je wewe unatumia Dawa gani? ili niweze ku shift kama ni nzuri zaidi! kuna hizi wanaziita sensodine naona zipo za aina nyingi na sijazikubali ni vigumu kugundua feki.

========



Dawa ya kusugulia meno ni kemikali inayotumika pamoja na mswaki wa kisasa kusafishia meno yazidi kupendeza na kuwa na afya.

Inasaidia kuondoa harufu mbaya, utambo wa meno na mabaki ya chakula katikati yake, pamoja na kuacha aina ya kinga (hasa ya floridi, kwa Kiingereza "Flouride") dhidi ya maradhi ya meno na ya ufizi (nyama inayoambatana nayo) (kwa Kiingereza "gingivitis").

Hata hivyo kwa kiasi kikubwa ufanisi wa usafi unategemea zaidi matumizi ya mswaki wenyewe kuliko ya dawa hiyo.

Badala ya dawa ya meno vinaweza kutumika chumvi na magadi.

Dawa ya meno hayatakiwi kumezwa kutokana na floridi iliyomo. Ikimezwa kidogo si hatari sana, lakini kama ni kiasi kikubwa ni lazima kuomba msaada wa daktari.

Dawa ya meno iliyotengenezwa kwa kusaga mifupa au chaza ilianza kutumika katika Ugiriki wa Kale na Roma ya Kale.

Matumizi yake yalienezwa hasa katika karne ya 19.

Nchi mbalimbali zimekataza aina kadhaa za dawa ya meno kutoka China kwa sababu zina sumu aina ya diethylene glycol (kifupi diglycol au DEG).

Michango ya wadau

----
Me natumia colgate maxfresh ambayo ina box kama la redbrown (kuna zenye box la blue)hivii au ukisema maximum spiced unapatiwa iwe dukani kwa mangi au supermarkets zinapatikana 3500-4000 ,hizo sensodyne ,ile aloe hamna kitu japo dr wanashauri
----
----
 
Kiukweli nilijua izo sensodine ni nzuri but hovyoo ni kama AHA ya buku tu, ila kuna Colgate moja nzuri niliitumia kipindi flani ina viparticle kama vya srcub ivi ilirudisha weupe wa meno yangu sana na ufresh wa mdomo unauhisi kabisa.
 
Troll JF

Aina hii ya colgate mpaka supermarket nini maana huku mtaani sizioni?
 
Sensodyne, very good!
Sensodyne very good vry good Mkuu usiache kuitumia hii na huta juta... huuwa vijidudu....unajua unatakiwa kutumia dawa sio tuu inawesafisha meno yawe meupe lakini zaidi iuwe vijidudu vilivyobakia.

Pia msisahau akama mna muda kutumia hata listerine kwa kusukutua mara moja moja.
 
Dr kanishauri nitumie SENSODYNE, cha ajabu humu inapondwa! Daah.
Tumia sensodyne hutojuta Mkuu
Sensodyne very good vry good Mkuu usiache kuitumia hii na huta juta... huuwa vijidudu....unajua unatakiwa kutumia dawa sio tuu inawesafisha meno yawe meupe lakini zaidi iuwe vijidudu vilivyobakia.

Pia msisahau akama mna muda kutumia hata listerine kwa kusukutua mara moja moj....
wanaoponda hawajui na wanaogopa gharama wao wanapenda vitu cheap vya jero...
 
natumia close up mkuu ni nzur inapatikana supermakert zote bei kulingana na ujazo unaoutaka lakn minimum price 2500
Mm mwenyewe naipenda sana hii dawa, cjawahi kutumia dawa ambazo ni expensive ila kwa hizi za mid range-price naona hii ni nzuri sana, japo kwenye maduka ya kawaida ni ngumu kuzipata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…