DAWASA: Huduma ya Maji imerejea maeneo ya Shekilango NHC na Ubungo

DAWASA: Huduma ya Maji imerejea maeneo ya Shekilango NHC na Ubungo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876


Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imesema huduma ya maji katika maeneo ya Shekilango NHC na Ubungo Magufuli Hosteli imeanza kuimarika na huduma kuwafikia Wananchi.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa DAWASA, Everlasting Lyaro amesema wamehakikisha upatikanaji wa Maji umerejea kuwa kawaida ambapo mafundi walifika maeneo husika na kuanza kufanya ukaguzi ikiwemo katika Mita kwa kuwa maji yanaingia moja kwa moja kwenye matenki.

Awali, Mdau wa JamiiForums.com alitoa wito kwa mamlaka husika kutatua kero ya ukosefu wa huduma ya maji kwa Wakazi wa maghorofa ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) yaliyopo Shekilango, akieleza hali hiyo inahatarisha afya za Watu na kwamba inasababisha harufu kali kutoka kwenye makazi hayo.


Pia soma ~ Maghorofa ya Shekilango NHC - Dar yananuka sababu ya kukosa maji
 
Back
Top Bottom