DAWASA kuzima mtambo wa Ruvu Juu kwa ajili ya matengenezo Januari 11, 2023

DAWASA kuzima mtambo wa Ruvu Juu kwa ajili ya matengenezo Januari 11, 2023

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
1673341126159.png
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imesema Mtambo huo utazimwa Januari 11, 2023 saa 12 asubuhi ili kufanya matengenezo ya Mabomba Makubwa ya Inchi 48 na 36 eneo la Mlandizi na Visiga.

Maeneo yatakayokosa Maji ni Chalinze, Mboga, Ruvu Darajani, Ruvu JKT, Vigwaza, Mlandizi, Mbwawa, Visiga, Maili 35, Misugusugu, Kongowe, Soga, Miembe Saba, Kwa Mfipa, Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias na Kwa Mbonde, Picha ya Ndege, Lulanzi, Kibaha na Kiluvya.

Maeneo mengine ni Kibamba, Mbezi, Magari Saba, Mbezi Inn, Mbezi, Kimara,Tabata, Segere, Kinyerezi, Kisukuru, Bonyokwa, Msigani, Maramba Mawili, Kimara B, Kimara Korogwe, Bucha, Baruti, Ubungo, Magomeni, Ukonga, Uwanja wa Ndege, Kiwalani, Vingunguti, Gongo la Mboto, Pugu na Kisarawe.

DAWASA imewakumbusha wananchi kuhifadhi maji ya kutosha ili kuwa na hifadhi ya kutosha kipindi chote cha matengenezo.
 
Yaan kipindi chote Cha kiangazi wametunyima maji na hawajafanya matengenezo,

Mvua zimeanza ndo mto umejaa maji ndo wanafanya matengenezo.

Hii nchi Sijui alieturoga nani[emoji26]
 
Walitukatia maji wakidai ukame ndo chanzo, wao hawajazuia mvua kunyesha.

Mvua sasa zinanyesha wanasema wanafanya matengenezo.

Yaan Sijui wanatuchukuliaje watanzania[emoji848]
 
Hii idara ya maji sawa TU na idara ya nishati.

Kule nishati Sinema Ilianza hivi
[emoji117]Kutakua na mgao kwa miez 6 tunafanya ukarabati, awamu ilopita hawakufanya service

Miez 6 imepita,
[emoji117]Mgao utaendelea kwasababu hatuna crane ya Tani kubwa kuinua mlango wa Bwawa ili kujaza maji

Mlango wa Bwawa umeletwa
[emoji117]Mgao utaendelea kwasababu ya ukame bwawa halina maji, awamu iliyopita ilikata mamilioni ya miti.

Mvua zimenyesha,
[emoji117]Mgao utaendelea kwasababu bwawa linahitaji misimu miwili ya mvua kujaa.

Baada ya minongono mingi,
[emoji117]Hata baada ya misimu miwili haiwezi kua suluhisho,bwawa litazalisha megawatt 2000+ wakati mahitaji ya nchi yetu Ni mega wat zaidi ya 15,000

Minongono ilipozid
[emoji117]kwanza umeme wa maji haufai na hautaburiki, tuhamie TU kwenye umeme wa gesi tuongeze kinyerezi phase za kutosha.

Unabaki unajiuliza Hizo kinyerezi tunaziongeza kwa gesi ipi, Kama gesi yenyew ya mtwara tulishapigwa tayar[emoji848]

Anyway,
tujiandae kwa episode zaidi .....
 
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imesema Mtambo huo utazimwa Januari 11, 2023 saa 12 asubuhi ili kufanya matengenezo ya Mabomba Makubwa ya Inchi 48 na 36 eneo la Mlandizi na Visiga...
Kuna mtu anadeni sehemu anataka kufidia. So anakata watu wanunue hill mambo yasonge kidogo. Akishalipa deni lake awaachie wanywe maji ya water guard
 
Matengenezo yatadum kwa muda gani? Taarifa tafadhali
 
Back
Top Bottom