Mkuu mada haihusiani na haya uliyoandika, na wala mimi sijakuuliza haya. Nashangaa unaniambia haya na wala hayahusiani na kile nilichoandika.
Mimi nimemjibu mtoa mada kulingana na kero yake, mambo ya watawala kufaidi angeandika pengine na haya ndio tungekuwa na mjadala huo. Sijaona alipoandika labda unionyeshe vinginevyo nitakuwa naharibu uzi wake kuleta vitu ambavyo hajavileta.
Mimi niliandika sehemu kubwa ya Dar, wewe ukaja na mara Ikulu sijui st Peters na vitu vingine unavyovijua wewe, sehemu kubwa ya Dar haimaanishi ni yote, nadhani hapo ndio hatukuelewana, sasa mambo ya logic na watawala mkuu nadhani umeyaleta sehemu ambayo hayahusiani mkuu.