DAWASA: Mradi wa Usafi wa Mazingira Afrika Mashariki wa kuchakata majitaka umefikia Asilimia 88

DAWASA: Mradi wa Usafi wa Mazingira Afrika Mashariki wa kuchakata majitaka umefikia Asilimia 88

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
WhatsApp Image 2026-09-03 at 15.43.23.jpeg

Mradi wa kwanza wa kisasa na usafi wa Mazingira Afrika Mashariki wa kuchakata majitaka Mbezi Beach unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) umefikia asilimia 88 ya utekelezaji wake huku ukitajwa kunufaisha kaya takribani 11,000 katika Wilaya ya Kinondoni.

Mradi huu unatekelezwa kwa gharama ya Shilingi bilioni 124 unahusisha, ulazaji wa mtandao wa bomba za majitaka kilomita 101, ujenzi wa Vituo viwili vya kusukuma majitaka, ujenzi wa chemba zaidi ya 2,300 pamoja na ujenzi wa mtambo wa Kisasa wa uchakataji majitaka.

Mradi huu unategemea kukamilika mwishoni mwa mwezi Oktoba,2026 utanufaisha zaidi ya kaya 11,000 katika kata nne za Kawe, Kunduchi, Mbezi Juu na Wazo wilayani Kinondoni, huku ukitegemewa kutoa bidhaa nyingine muhimu kama vile Mbolea na Gesi.
WhatsApp Image 2026-09-03 at 15.43.24.jpeg
 
Back
Top Bottom