DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Tunakaa masiku kadhaa bila maji, siku yakitoka hayana presha kabisa!! fanyeni mipango kuongeza presha ya maji
 
Sijaelewa maana ya mgao. Kama wiki inapita maji hayajarudi huo ni mgao au mmekata huduma ya maji????
 
Bei ya maji kwa cubic meter moja Ni sh ngapi kwa Dar es salaam?
 
Mnachokifanya halina afya hata kidogo! Just imagine hii ni wiki ya tatu imeanza bila Bomba za kunduchi mtakuja kutoa tone la maji! Hii siyo haki hata kidogo. Kama Kuna mgao basi uwe Kwa wote na siyo kuuelekeza mgao upande mmoja!

Sijui hiyo management yenu inawaza Nini pale shule zote za msingi zinapokosa huduma ya maji ya kunywa na kufanyia usafi vyooni!

Nakushauri manager utembelee shule zifuatazo; Mtakuja beach secondary, matuja primary na mtongani primary uone watoto Hawa wadogo wanavyohangaika mchana kusaka maji angalau ya kunywa kwasababu ya joto but hakuna maji for three weeks and you're still in the office!

Mnataka Hawa watoto wapate magonjwa ya kuhara na kipindupindu? Hebu wajibikeni Kwa haki na acheni kukata maji mashuleni kwani msije tengeneza mauaji ya kimbari!
 
Itakuwa jambo zuri iwapo waziri pamoja na CEO watatoa updates regularly kuhusiana na hili tatizo. Tunasikia kuwa pia kuna hitilafu kwenye mitambo na siyo uhaba wa maji peke yake. The CEO is said not to command respect from his juniors . Ni personal choice ya Waziri.
 
NAOMBA KUJUA KAMA KUNA MGAO WA MAJI KIMARA NJIA YA KWENDA BONYOKWA SIKU YA NNE LEO HATUNA MAJI,TUMEPIGA SIMU KIMARA WANASEMA HAWAJUI NINI TATIZO
 
NJIA YA KWENDA BONYOKWA MAARUUFU KWA MZEE MAJI WAMEKATA MABOMBA HATUPATI MAJI NA KAJIUNGANISHIA MAJI KUTOKA KWENYE MAMBOMBA YETU ANATUMIA MAJI KUJENGEA BILA KULIPIA,NI KABLA YA DARAJA LA KWENDA BONYOKWA TUNAOMBA MFUATILIE TUPATE MAJI
 
Afadhari wewe umejileta kuwasikiliza wadau, b
 
Huku Kisarawe, Pugu Kajiungeni baada ya kuanza mgao wa maji, sasa kila yanapotoka maji yanakuwa na rangi ya njano! Hii imekaaje au madawa ya Water treatment nayonyamekuwa ya mgao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…