KERO DAWASA wanafungulia maji kwa upendeleo maeneo ya Goba Matosa (kwa Bishilingi na Br Hotel)

KERO DAWASA wanafungulia maji kwa upendeleo maeneo ya Goba Matosa (kwa Bishilingi na Br Hotel)

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Nina kero yangu, Wakazi wa Goba Matosa maeneo ya kwa Bishilingi na Br hotel, DAWASA wanafungulia maji kwa upendeleo, baadhi ya nyumba zetu hatuna maji huu ni mwezi wa pili na cha kushangaza tunaketewa bill za maji kama kawaida.

Ukiwaambia wale wasoma mita wao hawatoi majibu ya kueleweka,kwa kweli tumechoka na hali hii kwanini baadhi ya nyumba ya natoka na nyumba nyingine hayatoki.Tunaomba tufikishie kero hii kwa wahusika. Ahsante

Tuliwasilisha kupitia wajumbe wetu wa mtaa ,wajumbe walimpigia meneja wa dawasa alawatuma mafundi wake waangalie tatizo ma mafumdi walikuja walasema kuna valve imejaribika lakini mpaka leo hawajaja tena na bado maji hayatoki
 
Back
Top Bottom