Responded DAWASA yaelezea sababu ya kuyumba kwa huduma ya maji Goba River view

Responded DAWASA yaelezea sababu ya kuyumba kwa huduma ya maji Goba River view

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) inapenda kutoa ufafanuzi wa changamoto ya huduma ya Maji katika mtaa wa River view katika eneo Goba iliyorepotiwa hivi karibuni.

Hoja ya Mdau ~ Mgao wa maji Goba - Mtaa wa River View (Dar) haufuati ratiba, tunauziwa maji Tenki Sh elfu 40

Ni kweli tumekuwa na changamoto ya huduma ya maji katika eneo hili iliyotokana na hitilafu kwenye mfumo wa umeme kwenye pump ya kusukuma Maji iliyopo eneo la Changanyikeni, hitilafu hiyo ilipelekea pump kuzimwa mara kwa mara na hivyo kusababisha kukosekana kwa huduma ya Maji kwa Wananchi wanaotegemea maji kupitia Pampu hiyo.

Changamoto hiyo imefanyiwa kazi na sasa Pampu ya kusukuma Maji katika eneo hilo inafanya kazi na ratiba ya huduma ya Maji inaendelea kufuatwa huku Wananchi wakiendelea kupata huduma. Ratiba ya upafikanaji wa Maji kwa eneo hili kama hakutakuwa na hitilafu ni siku ya Alhamisi na Ijumaa

DAWASA inawaomba radhi Wananchi kwa hitilafu hiyo na inawaahidi kuendelea kuboresha huduma na kuongeza mawasiliano zaidi ili kutatua changamoto za kihuduma pamoja.

Mamlaka pia inawakumbusha Wananchi wa Goba kuwa ofisi zao za kihuduma sasa zipo DAWASA Ubungo na sio Makongo kama walivyoreport awali.

Everlasting Lyaro
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
 
Huduma kwa wananchi kama hizi mtoe taarifa kama kuna changamoto sio mpaka yaufike kooni tuongee
 
Back
Top Bottom