Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imedhibiti utiririshaji wa majitaka kwa uondoaji wa majitaka na taka ngumu zilizokuwa zimepelekea chemba kuziba katika eneo la Posta.
Mamlaka inasisitiza matumizi sahihi ya miundombinu ya majitaka kwa kuepuka kutupa taka ngumu katika mifumo hiyo ambapo hupelekea kuziba mara kwa mara.
Kwa huduma za uondoshaji majitaka tafadhali wasiliana nasi kupitia namba 0735 451 879.
Everlasting Lyaro
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
DAWASA