DAWASA yatoa ufafanuzi kuhusu changamoto ya maji Malamba Mawili

DAWASA yatoa ufafanuzi kuhusu changamoto ya maji Malamba Mawili

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Eneo la Malamba Mawili ambalo lipo kata ya msigani linahudumiwa kupitia mtambo wa Maji Ruvu Juu.

Kutokana na maeneo hayo kuzungukwa na vilima vikali na hupata maji siku ya Jumanne, Alhamis na Jumapili, lakini baadhi ya maeneo kushindwa kupata maji pindi msukumo wa maji unapokuwa mdogo.

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) inaendelea na jitihada mbalimbali za kufanya maboresho ya huduma za Maji katika eneo hili kwa kufanya mradi wa kuongeza msukumo wa maji kwa kulaza bomba lenye kipenyo cha inchi 8 kwa umbali wa KM 3.5 katika maeneo hayo lengo ni kuboresha huduma.
photo_2024-05-19_10-32-38.jpg

photo_2024-05-19_10-32-37.jpg
Kwa sasa utekelezaji wa mradi huo umefikia 48% na kazi inaendelea. Hata hivyo wakati tukiendelea na utekelezaji huo tutaendelea kuratibu upatikanaji wa uhakika wa huduma za Maji ili kuhakikisha maeneo yote yanapata huduma ya maji.

Everlasting Lyaro
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
DAWASA

Malalamiko ya awali - KERO Maji Malamba Mawili ni mgao mkali, baadhi ya Wakazi walio kwenye miinuko wana miezi hawapati maji kutokana na kasi ndogo ya maji yanayotoka
 
Back
Top Bottom